jouneGwalu
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 2,687
- 1,780
Mnamo April, 1998, Mamlaka inayohusika na kulipa fidia kwa watu waliaoathiriwa na uhalifu (Criminal Injuries Compensation Authority) ilimtunukia Josie kiasi cha dola 30,000 kwa kumpoteza mama yake, dola 8,000 kwa majonzi aliyoyapata na dola 3,500 kwa mwaka kwa kukosa malezi ya mzazi wake. Hata hivyo kulikuwa na kelele nyingi kutoka kwa wananchi, bunge la nchi hiyo pamoja na vyombo vya habari kuhusiana na fidia hiyo. Waziri mmoja wa wakati huo Jack Straw alikiri kuhusu udhaifu huo wa sheria, na alisikitika kwamba hana mamlaka ya kuingilia juu ya maamuzi hayo. Lakini alimtaka baba wa mtoto Josie, Dr. Shaun Russell kukata rufaa kwa niaba ya binti yake.
Wakili wa Josie, Sarah Harman alisema watakata rufaa.
Hii ni sehemu ya msingi sana katika mifumo ya nchi za wenzetu, ambapo kwa kiasi fulani kuna kujali UTU.....
Sawa japo fedha haiwezi kurudisha uhai wa mtu ila ina nafasi katika kujenga namna ya kuonyesha kuwa "Tupo pamoja"
Naona michango mingi hapa haijagusia hilo...... Hivyo ndio mfumo wetu ulivyotufanya.... umetuaminisha kuwa "Hatuwezi , Hatuna Uwezo".....
Kitu kinachoitwa fidia katika jamii yetu kimegeuzwa maana na kuwekewa mizengwe ya hali ya juu hadi kufikia kuwa si kitu cha kufikirika katika haki za raia ......
Tuna watu wanakufa na kupoteza uwezo wao wa utendaji kwa uzembe wa serikali na idara zake na wala hamna hicho kitu kinachoitwa fidia.....
Watu wanauwawa mikononi mwa polisi wala hamna hicho kitu kinachoitwa fidia......
Watu wanapata ajali na kupoteza wapendwa wao na wala utaratibu uliowazi wa fidia juu ya walichopoteza.....
Kuna aina ya jamii ya ajabu sana inayotengenezwa hapa, watu wenye visasi na chuki na matabaka ya hali ya juu......