Paja la kuku

mpaka sasa hivi kuna baadhi ya sehemu kama kuna sherehe flani flani wanaume wanapewa mwanzo wanawake mnaambiwa wasubiri wanaume kumaliza kula vitavyobakia ndio mwala nyie.........
 
utamaduni mbovu kweli huu,yani wanawake waliohangaika jikoni ndo wale makombo lol
 
hahaha hapo umenena ni kweli kabisa,hata kama kiporo cha wali kimebaki wengine kesho yake mtakula ugali na baba atapashiwa.Aisee i hated that life

Mbaya sana. Sasa usije ukawalea watoto wako hivyo Kaby. . .

Alafu hii mada ngoja niombe ihamishiwe MMU. . . Inahusu sana.
 
siwezi kuja fanya hivyo,madhara yake nayafahamu!Haya mamie fanya hivyo.
 
unajua hili limewafanya hata watoto ambao walikuwa wanaona baba yao anampiga mama utashangaa nao wakioa wanaendeleza tabia hiyo kwa kweli mbayaaa
 
LAT kisa cha kunishtukiza hivyo jamani?

Hujaona pale "this post have been deleted by Lizzy" ??
Niliweka picha zikawa zinazingua nikafuta. Kama unataka nikuwekee maelezo tu niambie maana yapo tayari alafu picha ntaangalia namna hata baadae.

okay, nasubiri kule kule
 
Kwa wale ambao maisha yao ya utoto hayakutofautiana na yangu watapata picha halisi.
Nilizaliwa kwenye familia yenye kipato cha chini na kula kuku mpaka xmax.Na kuku akipikwa utamsikia mama 'hilo paja ni la baba' kwa hiyo sisi tunakula vipande vingine.
Hii tabia imeendelea kujijenga kichwani mwangu kiasi kwamba na utu uzima wangu kula paja kwangu ni mwiko, hata nikila na mtu nitakula vipande vingine nikwepe paja.
Hili ni tatizo ama?

Ni paja tu au paja lingine linakutisha?
 
Mama Ngina alikuwa na hako katabia kakuniwekea Paja la kuku na Firigisi yake, nikaikemea tabia hiyo mpaka akaacha kabisa..................Ukweli ni kwamba wengi malezi yametuathiri sana. kama ukijifunza Utambuzi, utaondokana na maisha ya mazoea...............Mimi nilishaondoka katika maisha hayo siku nyingi.
 
imenikumbusha niliadithiwa na mama walikuwa hawali kidari ni cha baba na chakula kikipikwa na nyama hakuna kula nyama mpaka baba aanze kupewa kwanza kama amechelewa kutoka kilabuni basi watakula chakula bila nyama...........chai ya maziwa ya baba lile jeusi la watoto daaaahh ilikuwa zaidi ya unyanyasaji
 
unajua hili limewafanya hata watoto ambao walikuwa wanaona baba yao anampiga mama utashangaa nao wakioa wanaendeleza tabia hiyo kwa kweli mbayaaa

watu wana vichwa vigumu hawajui kujifunza lipi la kuchukua lipi la kuacha
 
Kwa kina Rweye na TaMuganyizi enzi hizo akina mama walikuwa hawaruhusiwi kula kuku kabisa ni kwa wababa tu.Wewe unasema paja tu?
 
Mama Ngina alikuwa na hako katabia kakuniwekea Paja la kuku na Firigisi yake, nikaikemea tabia hiyo mpaka akaacha kabisa..................Ukweli ni kwamba wengi malezi yametuathiri sana. kama ukijifunza Utambuzi, utaondokana na maisha ya mazoea...............Mimi nilishaondoka katika maisha hayo siku nyingi.

hongera mkuu,huyo mama ngina atakuwa ametokea kwenye familia kama yangu
 
imenikumbusha niliadithiwa na mama walikuwa hawali kidari ni cha baba na chakula kikipikwa na nyama hakuna kula nyama mpaka baba aanze kupewa kwanza kama amechelewa kutoka kilabuni basi watakula chakula bila nyama...........chai ya maziwa ya baba lile jeusi la watoto daaaahh ilikuwa zaidi ya unyanyasaji

yani ni utamaduni ambao haufai kuigwa,,vipi umepona lakini?
 
Watajuaje lipi la kuchukua na lipi la kuacha wakati wanaowategemea ndivyo walivyowafundisha?

hapana lizzy napingana na wewe!Hivi ukiona mtu anafanya jambo baya ni lazima kuiga?hata kama ni mlezi wako?ndio maana tumetofautiana na viumbe wengine.tumepewa ufahamu!
 
Kwa wale ambao maisha yao ya utoto hayakutofautiana na yangu watapata picha halisi.
Nilizaliwa kwenye familia yenye kipato cha chini na kula kuku mpaka xmax.Na kuku akipikwa utamsikia mama 'hilo paja ni la baba' kwa hiyo sisi tunakula vipande vingine.
Hii tabia imeendelea kujijenga kichwani mwangu kiasi kwamba na utu uzima wangu kula paja kwangu ni mwiko, hata nikila na mtu nitakula vipande vingine nikwepe paja.
Hili ni tatizo ama?

yeah ni tatizo, mazingira na maisha uluyoishi huko nyuma yamejengeka akilini mwako, ila ukiamua kusahau na kubadilisha inawezekana
 
hapana lizzy napingana na wewe!Hivi ukiona mtu anafanya jambo baya ni lazima kuiga?hata kama ni mlezi wako?ndio maana tumetofautiana na viumbe wengine.tumepewa ufahamu!
Atajuaje ni baya kama mzazi wake alikua anapigwa na kuvumilia? Mtu anajifunza kwamba hiyo ndio namna ya kuishi. Ndio maana bado wapo wanaume wanaosema wanawake wanahitaji kuadabishwa sometimes, kwamba bila kipigo kama ni kosa wamefanya watarudia. Hii inatokana na kukulia kwenye mazingira ambayo kipigo ndicho kilichokua solution. Kama ambavyo mtu anaweza akakua na hii mentality ya "paja ni la kuku, baba kwanza" n.k
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom