Paja la kuku

Kabakabana

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
5,551
1,159
Kwa wale ambao maisha yao ya utoto hayakutofautiana na yangu watapata picha halisi.
Nilizaliwa kwenye familia yenye kipato cha chini na kula kuku mpaka xmax.Na kuku akipikwa utamsikia mama 'hilo paja ni la baba' kwa hiyo sisi tunakula vipande vingine.
Hii tabia imeendelea kujijenga kichwani mwangu kiasi kwamba na utu uzima wangu kula paja kwangu ni mwiko, hata nikila na mtu nitakula vipande vingine nikwepe paja.
Hili ni tatizo ama?
 
hehehe! Kama hilo paja umemwachia mgonjwa hakuna tatizo...

Ni tatizo ndio, maneno ya mama yamekuathiri kwa namna fulani... Ntarudi tena kufafanua.
 
sio kwa mgonjwa tu,hata ukija jioni utakula wewe paja mimi nyama ya shingo.
 
na frigisi nayo ni ya baba,
na ile nyama nono ya mgongo nayo ya baba uuuuiiii.
 
Utamaduni mbaya sana huo. . .
Eti baba kwanza, watoto mwisho. . . Baba wali watoto ugali, baba mayai na maziwa watoto kiporo. Wakati watoto wanahitaji virutubisho zaidi ya baba.
 
mi silagi filigisi, (ingawa natamani)walikua wakisema filigisi ni ya baba mwenye nyumba
 
Si tatizo, anza kula mara moja hadi utazoea....mi nilijua firigisi ndo ya baba...lol
 
Kwa wale ambao maisha yao ya utoto hayakutofautiana na yangu watapata picha halisi.
Nilizaliwa kwenye familia yenye kipato cha chini na kula kuku mpaka xmax.Na kuku akipikwa utamsikia mama 'hilo paja ni la baba' kwa hiyo sisi tunakula vipande vingine.
Hii tabia imeendelea kujijenga kichwani mwangu kiasi kwamba na utu uzima wangu kula paja kwangu ni mwiko, hata nikila na mtu nitakula vipande vingine nikwepe paja.
Hili ni tatizo ama?

Hapo hukumwelewa vizuri mama PAJA LA BABA maana yake
 
na frigisi nayo ni ya baba,
na ile nyama nono ya mgongo nayo ya baba uuuuiiii.

ni kweli firigisi nayo ya baba mpaka nilivyokua sasa nikaanza kugombania firigisi na baba,nikisema ni ya mpishi saa nyingine naila huko huko jikoni
 
Utamaduni mbaya sana huo. . .
Eti baba kwanza, watoto mwisho. . . Baba wali watoto ugali, baba mayai na maziwa watoto kiporo. Wakati watoto wanahitaji virutubisho zaidi ya baba.

hata kwenu kumbe ilikuepo eeh
 
ni kweli firigisi nayo ya baba mpaka nilivyokua sasa nikaanza kugombania firigisi na baba,nikisema ni ya mpishi saa nyingine naila huko huko jikoni
Lol.. Jitahidi na paja uwe unakula huko huko jikoni mwisho utazoea... Ila usianze leo manake mgeni atakosa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom