Pains Over My Sister’s Pregnancy For My Husband…

...imenibidi tu kuchangia.

Wote wanne (plus mtoto) ni waathirika kwa namna moja au nyingine.
Ukweli inabidi ukubalike kosa la uzinzi lishatokea.
Wasubirie mtoto azaliwe kisha wapime DNA.

Kuna kesi kama hii nilishawahi isikia,
"Inawezekana" vilevile hiyo mimba si ya huyo mume.
Yote yanawezekana kwa huyo 'mke' ndugu.
 
Ndio maana sisi wengine tumepigwa marufuku mashemeji hawakai ndani zaidi ya siku mbili.. huwa wanapita tu; na hilo jicho unalokatwa.... utakoma.
 
Ukweli ni kwamba familia za kiafrika kuna baadhi ya mambo zinajitakia. Utaona mtu anaoa mwanamke na baada ya miezi sita tu hata kabla hawajafaidi ndoa yao, unakuta nyumba imejaa watoto wa dada wa kila upande. wa mama mdogo wa kila upande na kadhalika. wote hawa wana kuwa ni vijana ambao damu ya moto inawatembea. Ndio maana mwisho wa siku nyumba inakuwa danguro. baba na mama wakienda ofisini huku nyuma kila mtu na wake!
Jamani, haikatazwi ndugu kutembeleana lakini usiruhusu mdogo wako anawaka kama Miss Fulani anakuja kwako anajenga kibanda. Kama unataka kumsaidia watumie hela wazazi wako wampeleke wanakotaka, lakini sio aje kujenga kibanda ndani ya nyumba. Wakati mwingine nikutafutana ubaya kama huu!!
 
...imenibidi tu kuchangia.

Wote wanne (plus mtoto) ni waathirika kwa namna moja au nyingine.
Ukweli inabidi ukubalike kosa la uzinzi lishatokea.
Wasubirie mtoto azaliwe kisha wapime DNA.

Kuna kesi kama hii nilishawahi isikia,
"Inawezekana" vilevile hiyo mimba si ya huyo mume.
Yote yanawezekana kwa huyo 'mke' ndugu.

Ni kweli kabisa! Yawezekana pia mtoto si wake. mdogo mtu ametafuta tu pa kusingizia.
 
:confused2: Pole lakini uwe makini kwa hilo. Jambo la kwanza usilifiche hilo kwa wazazi wako na wa mume. Jambo la pili ni lazima huyo mdogo wako aondoke hapo, wala usihangaike wewe kuondoka. Yeye atafutiwe kwingine. Haidhuru atafutiwe na nani. Hata kama ni baba wa mtoto(mumeo), ila la muhimu ni kuwa aondoke hapo. Amekukosea heshima uliyompa wewe. Wanaume wako wengi atampata wa kumuoa yeye. Huhitaji ugomvi na yeye kwa hilo.:confused2:
 
ningewaacha waendee na maisha na nina wac wac na undugu wangu kuendelea na huyo ndugu yangu...mume ndio ctaki hata kumuongelea coz huyo nicngempa hata sec kumruhusu kumuona mbele ya macho yangu...hili lickufike kabisa, hata ukisema unamsamehe mume bado familia ya mume haitaacha vimaneno, yani mtaonekana kama mbwa kasoro mkia.....hapana ni ngumu hii.
hilo tatizo ni zito haswa maana hata ukimuacha mmeo lakini mmezaa nae watoto lazima mtaonana tu kwa kuwa watoto wenu wapo kuna tukio litatokea mtakutana tena mara kwa mara na hata huyo mdogo wako mtakutana nae kila mara kwenye shughuli za kiukoo na kindugu hapo tatizo litakuumiza mpaka unaenda mavumbuni siku ya kifo
 
Habari wana JF
Naomba msaada maana hapa nilipo nimekaribia kuchanganyikiwa baada ya kutendwa na mtu niliyempenda na kumuamini sana hapa duniani....
Mimi ni mama wa mtoto mmoja lakini nina majonzi sana kisa kimeanza pale nilipomkaribisha mdogo wangu wa tumbo moja aje kukaa na mie kumbe mme wangu akaanza kutoka nae ...,hii imepelekea mdogo wangu kubeba mimba miezi 6 sasa nilipomuuliza ya nani akasema ni ya mtu iko siku nitamuona ..nilipomuomba amlete ili mme wangu amuone akadai ni pacha wa mme wangu..mara akaanza dharau kwangu nilipoendelea kumuhoji kwa kumtishia nimrudishe kijijini ndipo alipodai mimba ya mme wangu.....
Nilipomuuliza mme wangu alianza kulia na kudai nimsamehe sana amejaribu sana kumwambia mdogo wangu akatoe hiyo mimba ili asiniumize pale nitakapogundua lakini mdogo wangu alikataa na kudai amepata alichokua anakihitaji
Natamani kuikimbia hii ndoa iliyodumu kwa 12 years
Naomba msaada wenu ndugu zangu
NB : Sio mie FL1 na mama mwenzetu muathirika wa ndoa:A S embarassed:

Kimsingi imani kwa mume wake itakuwa imekwisha, ila atumie hekima na busara sana kwa kuangalia future plan yake na watoto wake, n ikiwezekana awashirikishe wazazi wa pande zote mbili.
 
Habari wana JF
Naomba msaada maana hapa nilipo nimekaribia kuchanganyikiwa baada ya kutendwa na mtu niliyempenda na kumuamini sana hapa duniani....
Mimi ni mama wa mtoto mmoja lakini nina majonzi sana kisa kimeanza pale nilipomkaribisha mdogo wangu wa tumbo moja aje kukaa na mie kumbe mme wangu akaanza kutoka nae ...,hii imepelekea mdogo wangu kubeba mimba miezi 6 sasa nilipomuuliza ya nani akasema ni ya mtu iko siku nitamuona ..nilipomuomba amlete ili mme wangu amuone akadai ni pacha wa mme wangu..mara akaanza dharau kwangu nilipoendelea kumuhoji kwa kumtishia nimrudishe kijijini ndipo alipodai mimba ya mme wangu.....
Nilipomuuliza mme wangu alianza kulia na kudai nimsamehe sana amejaribu sana kumwambia mdogo wangu akatoe hiyo mimba ili asiniumize pale nitakapogundua lakini mdogo wangu alikataa na kudai amepata alichokua anakihitaji
Natamani kuikimbia hii ndoa iliyodumu kwa 12 years
Naomba msaada wenu ndugu zangu
NB : Sio mie FL1 na mama mwenzetu muathirika wa ndoa:A S embarassed:

Umenishtua kweli FL1, nilitaka kuja haraka sana na timu ya wana maombi....

anyway.... ntarejea na ushauri wangu, ngoja niombe muongozo wa roho mtakatifu
 
ha ha ha ha nilijua utasema ..ila kama ni mie cjui ningefanya nn mwenzenu mpaka sasa cna jibu muafaka

Hebu fikiria hii ishu inakutokea wewe Mr. anajiexpress kabisa na mdogo wago na mdogo wako bomba kuliko wewe.
 
Au aombe talaka :A S-coffee:

FL1, hilo litakuwa kosa kubwa la kiufundi (technical error/miscalculation) kwa upande wa huyo mama. Itakuwa sawa na kuachia mali zake kwa mtu mwingine bila kuzipigania. Hata ikibidi kuwaacha baadaye lakini awashughulikie kwanza. Huyo mdogo mtu anahitaji kupewa disclipline itakayomsaidia maishani mwake.
My wife alinambia kuwa kitu cha kwanza angeanzia kwa vijana wanaona visu, then angeanza kutengeneza mishikaki toka kwa huyo binti mpumbavu kabla ya kuhamia kwa mume. Siyo lazima kumchinja ila lazima wote wapate adhabu inayolingana na kosa lao kabla ya kuamua future ya hiyo ndoa. Kwa vyovyote vile, nashauri huyo dada asivunje ndoa yake (kwani atawatesa watoto wake) ila pia asimpe hata dakika moja (nyingine) huyo mdogo wake kuendekeza upuuzi na mume wake!
 
Huwa anavua mwenyewe aisee.....
Normally mambo huwa anayaanza mdogo wako mwenyewe...sasa sababu mwili ni dhaifu...

mie nasema wa kumlaumu hapa ni wewe, kama yeye kayaanza unashindwaje kuzuia udhaifu wako na ukijua ni shemeji wa toka nikutoke na mkeo? ctakupa adhabu yoyote zaidi tu ya kutengana na wewe nakuanza maisha mapya yacyo na mume wala mdogo.
 
Mwambie mme wake afanye taratibu amuoe tu si wamependana!
Kuna jamaa sisi bush huko kaoa mabinti wa 3 nyumba moja anamega kama hana akili nzuri.

labda wamechanganyikiwa hao...yaanui mr wangu anilale mie na sis wangu, haitokaa itokee, kuna vya ku share jamani...
 
Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya wanaume huwa wanatembea na ama ndugu wa kike wa mke, marafiki wa kike wa mke, na mabinti wa kazi!! Kesi hizi ziko nyingi na zinatatuliwa ndani kwa ndani na pengine huishia kwenye kutengana au doa la ugomvi ndani ya familia lisilofutika. Hebu tuheshimu ndoa zetu na tutaepuka migogoro inayoleteleza kutengana/talaka na mbaya zaidi madhara kisaikolojia kwa watoto na wanandoa wenyewe.
 
Back
Top Bottom