Padri Tunda aikemea CCM na Serikali

Kisanduku

JF-Expert Member
Jul 9, 2009
284
482
Wakuu JF,
Nimeletewa gazeti moja la Kanisa Katoliki linaloitwa MWENGE nikisisitizwa nisome makala ya padri mmoja anaitwa Baptiste Tunda. Sina kawaida ya kusoma gazeti hilo lakini nikamuheshimu aliyeniletea. Niliposoma makala hiyo sikuamini niliyosoma ambapo huyu padri bila kumung'unya maneno amebeza ule ushindi wa kishindo wa CCM iliyoshindwa kwa kishindo kupambana na ufisadi. Inaelekea gazeti lilitoka mwezi wa nne (Toleo. Na. 851) na huku kwetu likachelewa kufika. Atakayeona toleo la sasa (Toleo. Na. 852) asisitie kutumwagia jamvini.
Faidi utamu wa maka hiyo na wale wasioamini haraka scan yake imeweza kupatikana kama kiambatanisho:

$ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $:

Toka mwaka jana tulianza kusherehekea Jubile ya Mmisionari na Mtume wa kimataifa, yaani Paulo. Mtume Paulo hakuwa kati ya mitume 12 wa Yesu kama alivyowaita yeye mwenyewe. Mtume Paulo aliitwa kivyake kwa njia ya kuanguka barabarani na farasi wake kule Dmascus na ndipo akasikia sauti ya Bwana wake anayemdhulumu.

Mtakatifu mtume na mmisionari huyu shujaa anajulikana sana kwa misimamo yake mbalimbali. Kwa sababu ya kuanzisha makanisa mengi kama ya Wakorinto, Waefeso, anajulikana kwa barua zake kwa makanisa hayo. Ninaweza kusema kwamba “wongofu wa Paulo ulikuwa ni wa kishindo, na hivi kazi zake zilikuwa za kishindo pamoja na kifo chake kilikuwa cha kishindo.

KARAMA YA UNYENYEKEVU:

Baada ya kukutana na Bwana hakutaka kusikia upuuzi mwingine tena. Hata hivyo Paulo alijifunza karama ya unyenyekevu na akabaini kuwa sisi sote ni wadhambi. Kwa njia hiyo kusiwepo majivuno ya aina yoyote ile. Paulo anasema kwamba, “Aliyesimama ajiangalie asije akaanguka”.

Tangu uchaguzi wa mwaka 2005 Chama Cha Mapinduzi kimekuwa na semi nyingi na majigambo mengi sana ya kwamba CCM ilipata ushindi wa kishindo. Sina uhakika huo, lakini ninachojua ni kwamba CCM ilishinda na ikaunda serikali ya awamu hii ya nne. Ushindi wa kishindo aliupata Yesu siku ya ufufuko, umeleta ushindi kwetu waamini wote wanaomfuata. Yesu ni mshindi na mtawala, ni mfalme wa wafalme hakika.

Sasa ufalme wa Yesu na ushindi wake umemuondoa mwanadamu katika utumwa mbalimbali. Ushindi wa Yesu umeleta uhai mpya, matumaini, na jinsi ya kuishi upya.

Sasa ushindi wa CCM umeleta nini kwa maisha ya watanzania? Kauli mbiu ilikuwa “Maisha Bora kwa Kila Mtanzania”, watu tumebaki kuhoji, je, yamefika au bado?

Ushindi wa kishindo maana yake nini? Unapothubutu kusema ushindi wa kishindo, wakati rushwa imekithiri kila kona, umaskini umeongezeka, ajira kwa vijana Hakuna, utapeli umezidi, mikataba ya ovyo inaendelea kusainiwa, viongozi wa juu kujihusisha na ufisadi wa mabilioni ya pesa za wananchi, tena walalahoi, makabwela. Huu ushindi wa kishindo unamaanisha nini?

SERIKALI YA AWAMU YA NNE:

Kilichonikera ni hasa baada ya miaka 3 na uchaguzi kupita, bado wana-CCM wanaimba wimbo wa “Ushindi wa Kishindo” majukwaani. Imefika mahala sasa tuanze kuiona hali halis na kuikubali. Je, tunaweza kusema serikali ya awamu ya nne imeshinda? Imeshinda nini?

Mimi kwa Mawazo yangu ningetaka kuutafakari ushindi wa wapinzani. Maana wamefanikiwa kuufukua ufisadi na wizi wa mabilioni ya pesa za wananchi maskini katika sekta mbalimbali, EPA ya Benki Kuu, Richmond, Kiwira n.k.

Na hadi sasa ni kesi tu zinafunguliwa, hakuana aliyehukumiwa kwa kisingizo cha kwamba tunataka ushahidi, ni ushahidi gani unatafutwa?
Watuhumiwa wengi wa ufisadi bado wana nyadhifa zao kama wabunge na kadhalika.

Wenzetu Ulaya na Amerika, mtu akituhumiwa mara moja anasimamishwa kazi bila kujali cheo ama uhusiano wake na rais na mara moja anaanza kuchunguzwa. Lakini sisi hapa kwetu “Kisiwa cha Amami” kama ipo, watu ni ving’ang’anizi kweli. Unasikia wanasema “Siondoki, sijiudhuru NG’OO!! Tena kwa kiburi na jeuri”. Hii ni hatari kubwa sana kwa taifa letu.

Je, kwa mtindo huu utasema serikali imeshinda au imehindwa? Kwa mtindo huu serikali inapoteza imani kila siku kwa wananchi wake hata kama hawajasema “tumepoteza imani nawe serikali ya awamu ya nne’.

Lakini tuache unafiki na kujifanya umbuni wa kuficha kichwa mchangani na kiwiliwili chote nje na kujidanganya kuwa hawakuoni. Yesu alikuwa anatumia usemi kuwa “Mwenye masikio na asikie”.

Kuendelea kujidanganya mmeshinda kwa kishindo si kweli. Kuwafanya watanzania wote ni wajinga kwamba hawajui kinachoendelea katika nchi yetu ni kujidanganya wenyewe kwa wenyewe.

Nenda sokoni, nenda kilabuni, ndani ya basi, ndani ta teksi, sikiliza waumini wakitoka kwenye ibada zao, waalimu, wafanyakazi wa ngazi za chini, mapolisi, manesi na watumishi wengine utabainisha mwenyewe.
Yesu anasema “Ukwelu utawaweka huru”.

Itaendelea tolea lijalo.

$ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $ $:
 

Attachments

  • Padri Tunda-01.pdf
    464.1 KB · Views: 113
  • Padri Tunda-02.pdf
    597.6 KB · Views: 53
Sema wewe Mapumba, Maana wapinzania wakisema watasema kuwa ni Wapinzania, Mimi nataka watu kama hawa ndio wajitokeze hadharani na kusema kuwa Serikali ya yetu imeshindwa kabisa.
 
Astghfilulah. Naona sasa wanachokitaka kinatokea. Wameanza masheikh sasa wanafuata mapadri, tena hawa sumu yao ni kali kweli na hawana utata sana. Ukiwapa jukwaa they know how to talk the talk, leave alone walking the walk. Amepiga moja kwa moja kwenye kichwa cha msumari. Sina hakika kama kweli toleo lijalo litatoka, na sina hakika kama ataachwa aendelee kuongea naye anaweza "kunyamazishwa" kiaina. Lakini at least mtu asiyetoka kwenye chama amesema, sasa tusubiri.
 
Padiri amesema kweli kabisa kwa wananchi wengi wa Tanzania ushindi wa CCM sasa hivi hauna maana yoyote.Hali ya maisha imeendelea kuwa ghali sana huku serikali yao ikiwa haifanyi jambo lolote la maana kuibadilisha hali hiyo.

Sukari,mafuta ya kupikia,mchele,unga,maharagwe,mboga mboga vyote bei juu na sio wananchi wote wanaoweza kupata milo miwili kwa siku,si mijini wala mashambani,huduma za afya ni mbovu,barabara mbovu,elimu inazdi kushuka kila kukicha.Sasa kwa hali hii kweli kuna dalili zozote za maisha bora kwa kila mtanzania.

Wadanganyika wamedanganyika kweli lakini sasa umefika mwisho wa maneno yote karibuni tuu ukweli utajulikana.
 
kweli alichosema Padri watu wote tumekata tamaa tuliitegemea sana awamu ya nne lakini sasa basi hao tunajiondoa polepole
 
Huyu ametema cheche.. safi sana.

Mkuu kama kumkoma nyani 'Father' amethubutu! Yesu wako akushindie na ujumbe wako ufike kwa wengi na kuamsha mioyo ya watanzania wengi walio kata tamaa ili waweze kufanya kweli 2010 kulikomboa taifa letu!
 
Hawa si ndo waliotuambia ni chaguo la Mungu? sitaki kuwasikiliza tena kwa sababu hawajui wafanyayo

Kama Paul alivyo andika pumba kwenye Bible na wafuasi wake wanfuata pumba hizohizo.

Nitaamini maneno ya Yesu lakini sio ya Paul anaejiita nabii na wafuasi wanfuata bila ku-question, si ndo huyu alikua haramia dhidi ya Yesu? niambie maneno ya Yesu sio Paul.
 
JF tuliwahi kuhoji kwanini viongozi wa dini wapo kimya wakati nchi inateketea. Sasa wachungaji na Mashekh, Imam wameamka tunaanza kubeza. Tunataka nini.

Wameona Serikali ya CCM inawahadaa ahadi ilizotoa kwa waumini wao na wao hazitekelezeki sasa wanahoji.
 
Hawa si ndo waliotuambia ni chaguo la Mungu? sitaki kuwasikiliza tena kwa sababu hawajui wafanyayo

Kama Paul alivyo andika pumba kwenye Bible na wafuasi wake wanfuata pumba hizohizo.

Nitaamini maneno ya Yesu lakini sio ya Paul anaejiita nabii na wafuasi wanfuata bila ku-question, si ndo huyu alikua haramia dhidi ya Yesu? niambie maneno ya Yesu sio Paul.

Dhambi ya kututangazia CHAGUO LA MUNGU haitafutika kirahisi hata waombe msamaha kwa njia zipi.

Ni kama dhambi mbaya ya kumfunga Galiei Galileo kwa ukweli wake kwamba dunia ina revolve around the sun hadi Galiei akapofukia kifungoni. Dhambi hiyo imeobewa msamaha tangu mwaka 2000 lakini kanisa linajisahau kwamba ilikuwa dhambi mbaya ambayo itakumbukwa na kuzungumzwa kila wakati kana kwamba imetokea jana tu.

Kwa kweli tuliwaamni waliposema CHAGUO la Mungu tukidhani wamefanya hivyo baada ya mafungo, novena na rosari.
 
Hawa si ndo waliotuambia ni chaguo la Mungu? sitaki kuwasikiliza tena kwa sababu hawajui wafanyayo

Kama Paul alivyo andika pumba kwenye Bible na wafuasi wake wanfuata pumba hizohizo.

Nitaamini maneno ya Yesu lakini sio ya Paul anaejiita nabii na wafuasi wanfuata bila ku-question, si ndo huyu alikua haramia dhidi ya Yesu? niambie maneno ya Yesu sio Paul.

Mkuu kwani wakristo peke yao ndiyo waliyo mchagua Kikwete? Watu wa dini zingine hawaja mchagua?

Sasa hapa Paul anaingiaje kwenye thread hii? Halafu mkianza kujibiwa hoja mtaanza kusema Wakristo wadini au sijui Wakristo ni hivi. Hapa kulikuwa na swala la kuingiza udini? Sema tu mkuu kama unataka kujibiwa ila tujibiana kiustarabu na mtu asikimbilie kusema anaonewa.
 
Jamani watu wa mungu masheikh na Mapdre ,Maaskofu na Wachungaji kama mumeshindwa kuhubiri dini kaeni kimya mambo ya siasa tuachie wananchi.Kwenu kazi imewashinda Tafadhali musituletee balaa nchini.Tafadhali ya Kaisari tuachie sisi tulumbane na serikali na SISIM.Labda dhambi zimewazidi ndio maana hamuyaoni mazuri ya serikali ya Nne.Kama wazungu na wamarekani wanatusifia ninyi hamuoni basi kaeni kimya.Acha SISIM ipete.
 
Back
Top Bottom