Padri Karugendo: Spika huyu si bora kwa Bunge la Wananchi!

Hivi Padri Karugendo kama raia wa TZ mnataka kusema hana haki ya kuongea au kukemea maovu kwa vile yeye ni padri. Hivi matatizo yakitokea unafikiri yeye haadhiriki??

Yeye kama raia wa TZ ana uhuru wa kuongea ispokuwa hasivunje sheria za nchi. Sasa kama amevunja sheria then sheria ichukue mkondo wake.
 
Hao mapandri sasa wataka kuwapanda watu vichwa

hizi zote ni chuki binafsi dhidi ya mapadre. Mapadre ni Watanzania, ni wananchi huru, wanahaki zote kama ilivyo kwako kutoa maoni juu ya suala lolote katika Taifa lao.

Bravo ma-father kwa kazi nzuri, mmesomeshwa kwa pesa nyingi, isaidieni jamii yenu kufumbuka macho, ibilisi wa maendeleo amewakamata baadhi ya watu.
 
Tujadili hoja ya Padre wetu. Tusimjadili yeye. Mwanzilishi wa thread hii aisimamie. Asibandike na kulala mbele(kwa wale mliopita JKT mnanielewa).
 
Hivi ukiwa Padri huruhusiwi kukemea maovu hata ndani ya serikal?i nahisi wadau wanafikiri utendaji wa Serikali ni Siasa nini???? Hivi hakuna mpaka kati ya Serikali na siasa?? kama ndivyo basi watendaji wote ni wanasiasa.
Inaelekea wadau wengine humu hawamjui vizuri PADRE (Ingawa siku hizi hajitambulishi sana kama Padri) P.KARUGENDO.Tafadhalini msomeni kwenye Tanzania Daima na Raia Mwema ni mmoja kati ya waandishi mahiri nchini.
 
Mapadre wanakosa muelekeo, wanaingilia siasa wanshindwa kutekeleza wajibu wao makanisani, kukosa mwelekeo wanashindwa hatakuelewa kua u-gay nilaana ya mungu na kubaka watoto ni dhambi. Put your houses in order kabla ya kuingilia siasa. Malabouk


Kwakuwa umejua ni Padri ndio unamwona ana haki ya kutoa maoni yake juu ya nchi yake! Ina maana wewe ata kama ni Mkulima huna haki ya kuchangia suala lolote linalohusu wafanyakazi! Acheni mambo ya kizamani hayo
 
Sasa rudini kwenye hoja iliyopo mbele. Spika sita hatufai. Mambo ya kumjadili mwandishi/mchambuzi yanaharibu focus ya thread.
 
Wazee, kazi ya viongozi wa dini si kuongoza roho tu.Lazima uwajengee mazingira mazuri ya kuishi ili waweze kulipokea neno la Mungu. Sasa watu wa Mungu wakae kimya waachie nyangumi wahayibu mazingira ya wanakondoo wao?
 
Suala la msingi ni hoja aliyoileta au ni nani kaileta hiyo hoja? Naona kuna sehemu tunakosea. Tunataka kuwafanya viongozi wa dini kama sio wahusika wala suala la maendeleo ta TZ. Ni kweli dini haitakiwi kubeba dhamana ya siasa mfano kama leo kanisa litaamua kuwaambia waumini wake wachague wakristu tu hapo patakuwa na kasoro. Ila kama kuna wizi wakisema jamani wizi kitu kibaya halafu tuwasingizie wanachanga dini na siasa, napata mashaka. Pengine sisi ndo tunachanganyikiwa kwa sababu ya ukweli unaohubiriwa. Hii sensitivity ya kidini inakujaje kwenye masuala yasiojari nani ni dini gani? au ni mkakati wa kupoteza malengo ya hoja?
 
hizi zote ni chuki binafsi dhidi ya mapadre. Mapadre ni Watanzania, ni wananchi huru, wanahaki zote kama ilivyo kwako kutoa maoni juu ya suala lolote katika Taifa lao.

Bravo ma-father kwa kazi nzuri, mmesomeshwa kwa pesa nyingi, isaidieni jamii yenu kufumbuka macho, ibilisi wa maendeleo amewakamata baadhi ya watu.
Ni kweli kabisa. Wanayo haki kama watanzania wengine kukosoa mambo yasiyoridhisha katika jamii. Wamesoma na wanaujua ukweli kwamba majority ya wananchi sio wasomi. Wanaowajibu wa kutoa mchango wao kuiboresha hii nchi. Hizi hoja za udini zinaletwa na watu kutojiamini au kuzima jitihada zao za kutoa michango yenye kuboresha jamii zetu ilhali baadhi ya watu wachache pengine watakosa ulaji.
 
Hoja hapa ni kwamba spika wetu anaonyesha double standards na anatoa maamuzi yenye kuonyesha upendeleo.......au ndo tuseme ni kweli 2010 presha inapanda....presha inashuka?

kwa sababu kama mbunge Selelii alitumia vitabu halali vya bunge, na serikali ikakiri kuwa 'walibadili badili majina ya vitengo' bila kuliarifu bunge, kwa nini asiiambie serikali kuwa imekosea?

kama yeye yupo hivi, je anategemea wabunge wawabane kweli mawaziri kwenye bajeti? Mi nilidhani swali la kwaza ambalo wabunge wangeuliza serikali ni kuwa iweje, bajeti ya trilioni 9 na ushee, trilioni 6 na ushee ni matumizi ya kawaida, na trilioni tatu ndo matumizi ya kawaida....je hayo maisha bora kwa kila mtanzania yatakuwepo kweli? hoja ingeanzia hapa kabla hata ya kufika kwenye specifics za wizara

Lakini, kama kawaida, waliopinga walipinga mdomoni huku mmoyoni wakijua kuwa wataipitisha tu, na kweli imepita.....wenye kunywa mvinyo sasa wanakunywa, presha imeshuka!
 
Tatizo la watanzania, watu hawapendi kujadili vitu vyenye kuhoji kisheria na kutoa facts kwa manufaa ya wote na someone may even try to kill mjadala ambao ungekuwa positive kwa uelewa wa mambo yanavyotakiwa yaende kwenye shughuli zote za kiserikali, na badala yake kushambulia mtu hata kama anatoa or anajadili facts, na matokeo yake kuita udadidisi wa kisheria ' "blablah' na badala yake tunapenda when the comedy akitupa stories zake basi twafurahi, jioni twende tukalale siku ipite! we are always not serious!
 
Hawa watetea mafisadi nao wasituvuruge, nani kasema mapadre, wachungaji ama Masheikh hawaruhusiwi kuongelea ama kutoa maoni yao juu ya siasa na mwenendo mzima wa maisha iwe juu ya uchumu, siasa nk? imeandikwa wapi kuwa kuna mpaka katika wayasemayo? acheni roho zenu za kwanini, kama kuna makosa wameyabaini muhimu sana kuyaainisha
 
Je kanisani kuko-clean kiasi gani? the padres should put their house on order, umalaya kanisani, usenge, ubasha na mafisadi wengi ni congregation wao. NANI KTK NYIE NI MSAFI????

MUACHENI KAISAR NA SIASA NYIE BAKINI KWENYE DINI. KWASABABU HANTENDI KAZI YENU VIZURI NDO MAANA MNAPRODUCE UFISADI.
 
Huyu ni mwandishi wa makala za RAIA MWEMA HAMJUI nini?? Na huyu si padri maana aliachishwa upadri miaka ya nyuma huko. Huyu ni sawa na Dr Slaa. Naye alikuwa padre na akaaomba yeye mwenyewe kwa Papa kuacha updre.
Habari ndo hiyo na msikasirike bila kujua, Jina tu hilo na si padre. MSOME MAGAZETI YA TZ, MTAWAJUA WAANDISHI WA MAKALA

Tembelea Raia Mwema - Muungwana ni Vitendo

Mkuu Idumu,

Mimi nafikiri Padri naye ni raia na mwananchi katika nchi yetu na wala kuwa kiongozi wa dini hakupashwi kumzuia kutoa maoni yake na hasa anapotumia magazeti kutoa maoni hayo. Endapo Padri/Mchungaji/Shekhe atatumia madhabahu kuhubiri siasa badala ya dini hapo tunaweza kukemea. Sioni kosa la Padri Karugendo hata kama angekuwa bado hajavuliwa Upadri.

Hapa JF naona kuna ka uvamizi ka aina fulani hivi!!! Hivi chunguza na kuona hao wote waliotoa comments za mwanzo walijiunga lini JF!!! Mamluki wanaojitahidi kukwepesha hoja za msingi kama hii ya Padri Karugendo.

Shame on you!!!

Tiba
 
Mapadre wanakosa muelekeo, wanaingilia siasa wanshindwa kutekeleza wajibu wao makanisani, kukosa mwelekeo wanashindwa hatakuelewa kua u-gay nilaana ya mungu na kubaka watoto ni dhambi. Put your houses in order kabla ya kuingilia siasa. Malabouk

Hilo tatizo la mtu binafsi kama padri ni mbakaji hiyo inakuwa ni hulka yake kama ilivyo kwa maImam na masheck kwenye madrasa kila siku wanababwa kwa hicho sio kigezo cha kumkatalia Padri ambaye ni Mtanzania asizungumzie mambo yanayoiguza jamii
 
wenzangu, changieni mada ilyo mbele yenu si personality au wadhifa wa mtu, mada hii ni nyeti tuichangie mbona makatisha tamaa wachangiaji he nyie vipi, upadre upadre he awe asiwe haihusu hapa acheni uswahili
 
Siasa na dini havichanganywi, bora ajiunge kwenye siasa mja kwamoja, kwa sababu shughuli ya kanisa pekee nikazi kubwa kunauchafu mwing kule, sasa wanasiasa nao waingilie kanisa ? sinachuki anatakiwa awajibike kwake kwanza kunauchafu mwing tu, nahao wasiasa wanakuja kila J'pili awavute awekemee kama anataka kukataza maovu, He should clean his house first, asilete blablaa
Hivyo nilivyo highlight kwa red inatakiwa visomeke hivi Siasa = dini
maana wadau wao(wananchi) ni wale wale na malengo yao mara zote ni yale yale tu. Lakini ili kutufanya sisi mabwege tunaambiwa ni vitu tofauti. Naweza kukuletea mifano toka karne kabla ya Kristo na hata baada ya kristo.
Futa mawazo ya kuweka neno
NA katikati ya maneno hayo mawili. Weka =
 
Tujadili hoja ya Padre wetu. Tusimjadili yeye. Mwanzilishi wa thread hii aisimamie. Asibandike na kulala mbele(kwa wale mliopita JKT mnanielewa).

Ndo maana wanafunzi wengi wanashindwa mtihani, badala ya kujadili hoja ya Ubora wa Spika wanarukia mengine ambayo hayana kichwa miguu!!!
 
Hongera sana Padre Karugendo, Ukiwa kama Mtanzania una haki ya Kikatiba ya Kutoa maoni yako na kama mtu hakubaliani na hoja zako inapaswa kuwa hivyo kwa misingi na mantiki ya hoja zenyewe na sio sababu eti wewe ni Padre, Katiba haikuweka limitations ya nani atoe maoni, most of us here apart kujua kutype hapa hata hatujui katiba ina rangi gani, shame on us tunaotumisahmbulkia watoa hoja badala ya kuangalia minofu ya hoja

Hongera Karugendo kwa Kutumia Fursa yako ya Kikatiba
 
Back
Top Bottom