Oyaa!! - Usionyeshe Salary Slip Yako!

miwatu mingine bana!! sasa maendeleo yanatoka wapikama hampangi pamoja? na mtapangaje kama hakuna anyejua mwenzie ana bei gani? kuna vijihela ambavyo kila mmoja anaweza asiseme kama amepata, unaweza kupata vihela kidogo ukaamua kuweka mfukoni.kwa ajili ya vikao vya jioni kwenye ze pub n.k na wife vilevile kama kapata ka mchongo ka 50,000 kwani lazima akwambie? si anaweza kununua anachotaka bila kugusa budget kubwa jama.

Miwatu mingine bado inaishi 1800!!
 
kama mimi ndio mwenye kipato na mama watoto hana kitu,hii nayo imekaaje?nimuoneshe salary slip?
 
Hapa zaidi inategemea na watu wanaishi vipi kama baba kwa mfano anawake wanne tuseme atamuonesha yupi na apange hiyo bajeti na yupi?
Hapo ni usawa wa kuacha za matumizi huku umegeukia ukutani.
 
kama mimi ndio mwenye kipato na mama watoto hana kitu,hii nayo imekaaje?nimuoneshe salary slip?
Yeah, muonyeshe maana ni mkeo na inabidi umshirikishe kwenye kupanga bajeti. Hivyo mtapannga bajeti yenu kutokana na kipato ulichonacho.
 
...haya, ukiandika wosia je, ...utamuonyesha jinsi ulivyoigawanya mali?



Interesting...hivi are u supposed to share the details of your will na mkeo? and vice versa? ama kama mke anayo mali iloyoko katika jina lake, mume ana haki gani hapo? ama yatakuwa yale mambo ya surprise za JM na Diana Ross??

mnapoandika will mnashirikiana ama ni kimya kimya tu?
 
kwa mtazamo wangu mimi sioni kama kuna tatizo la kuonyesha ni kiasi gani unakivuna huko unapotumika kwa maana kama ni mkeo basi mlishakaa na kujuana vizuri na mko hapo kwa maisha yenu pamoja na watoto wenu, lakini kama bado ndo mambo ya uchumba hapo ni noma mwanawane
 
kuna jamaangu alipata kusema kwamba "ndugu yangu ukimwonyesha mkeo `salary slip` umekwisha!, maana atazua matumizi yasiyo ya lazima, hadi ahakikishe fedha zote zimeisha"!

lakini pia, kwa uchunguzi wangu binafsi kumekuwa na tabia ya watu wengi kuficha kwa wake zao (au waume zao), figures halisi za mishahara yao.

ukiacha mishahara, pia kuna marupurupu lukuki ambayo huenda mume au mke anaweza akawa anayapata, lakini yote haya hayasemwi kwa uwazi kwa mwenza.

kuna vitu kama overtime, tips, bakshishi, commission za manunuzi, allowances kadha na safari packages ambazo wanaume wengi hawaziweki wazi kwa wake zao pindi wazipatapo.

je kuna ukweli gani kuhusu jambo hili?

ni halali kuweka hadharani mafao haya kwa mwenza, au ni salary slip tu inayotakiwa kuonyeshwa?


wenye lugha yao wanita pay slip
 
Interesting...hivi are u supposed to share the details of your will na mkeo? and vice versa? ama kama mke anayo mali iloyoko katika jina lake, mume ana haki gani hapo? ama yatakuwa yale mambo ya surprise za JM na Diana Ross??

mnapoandika will mnashirikiana ama ni kimya kimya tu?

...unadhani watajibu? mnh, 'wanaogopa' kuzungumzia mambo ya vifo hawa! :D
 
Spouse kuona salary-slip yako nadhani sio issue. Inaweza ikawa na manufaa zaidi kwani anaweza pia kukushauri mawazo kiasi gani kiende wapi na wapi kwani anajua ukweli.

Ubaya unakuja pale ndugu (wakwe, wajomba, dada, kaka etc) wanapojua unakunja ngapi exactly kila mwisho wa mwezi. Hawakawii kuanza kukupigia mahesabu ya pesa yako
 
Je haiwezekani kuteleza ukawa ulimwonyesha wakati wa uchumba? Sasa mkiishaingia kwenye ndoa inakuwaje?
 
Sometime ni vizuri ukasema ukweli wa mambo ulivyo kuliko kuhangaika na nadharia. Wengi humu wanasema ni vizuri kumuonyesha mwenza sijui salary/pay slip. Uhalisia wa mambo ni kuwa kuonyesha kipato chako halisi ni tatizo kubwa kwa sababu mwenzi ni lazima ataanza kuipangia bajeti yte na kuuacha wewe huna kilinda mfuko. Mkumbuke kuwa kilinda mfuko ni muhimu hasa ukizingatia kuwa kuna matumizi mengine huwa nje ya bajeti. Inakuwa mbaya mama akijua kipato chako halisi hata kama naye anakipato kwani UTEGEMEZi na tabia yao ya kuwa HELA yao ni yao na ya waume zao ni ya pamoja. Pindi ukiamua kuonyesha kipato chako halisi plz umeumefanya COST-BENEFIT ANALYSIS ili mbeleni isikugharimu.
 
Kuna baadhi ya wamama wana tabia hiyo, sio uongo. na wengine wanajitetea kuwa kwa kufanya hivyo ni kama kumfanya mume asiwe na hela za kuchezea hasa wakilenga kupeleka nyumba ndogo. wanaamini kuwa mume akiwa na hela za ziada basi anaanzisha matumizi yasiyo ya maana.
kwa mtazamo wangu, solution siyo kumficha mkeo salary slip, ni kuongea naye tu na kumhakikishia kuwa hizo hela huzifanyii matumizi yasiyo ya maana.
Sielewi kwa nini wamama wawafiche waume salary slip zao
 
Je mkeo naye asikuonyeshe salary slip yake? Utajisikiaje mkeo akificha kipato chake? Kuna wanawake wana kazi na mishahara mizuri kuliko waume zao. Huyo rafiki yako anasemaje kwa hili?
 
Are you people really serious, au mnafurahisha wanaJF?

Hivi si nyie ambao mnageukia ukutani hata mnapoacha hela ya mboga?

Lets speak our hearts jameni!


hili lina ukweli kabisaaaa, naona tupunguze utani hapa, watu waseme ukweli kutoka mioyoni mwao
 
Sasa si ni bora usio au usiolewe kabisa kuliko kuficha ficha vitu wakati uko mume au mke wa mtu.

Dang son,

Unajua kwenye suala la ndoa tuna analysis inayorandana sana. Nilikuwa nafikiria exactly the same thing nikaona ushaniwahi kuandika.

What is the point of marriage if you can't trust and be in harmony with your wife?

Kama huwezi kumwambia mshahara unaweza kumwambia kwenye akaunti kuna kiasi gani? Unaweza kukaa naye chini mkachonga will? Unaweza kumfanya beneficiary kwenye insurance policy? Unaweza kumpa mkeo PIN code ya ATM?

Ukifa nani atasaidia familia yako? It seems to me kuna watu wengine wameoa kwa jina tu, na wengine ambao hatujaoa tunaweza tukawa juu zaidi katika scale ya mambo ya ndoa.
 
Ndoa yenye mapenzi ya kweli lazima kuwe na transparency ya kila kitu.kama mnafichana hata mishahara then hapo hapana mapenzi kabisa.what is money by the way compared to love?
 
Tabia za Ubinafsi zinaanzia tangia Utotoni kwenye Malezi, Uchoyo uchoyo tu sasa mambo ya Uchoyo na Ubinafsi hayaishiyanaenda Mpaka kwenye Maisha ya Ndoa. Wewe unazungumzia Salary kuna wanaume wengine wana magari lakini wake zao hawajui hata kupiga starter! Huu ni Ubinafsi tu. Ndoa isipokuwa na Transparency haiwezi kuwa na Maendeleo yeyote, unless kama umeoa ili upate Mtu wa Kumega tu ila kama unataka kujenga familia iliyoendea ni Lazima muwe wa wazi kwa kila kitu na Hilo la Mapato ni Muhimu zaidi! Kuna Ubaya gani mkeo/mumeo akijua password ya ATM yako? Halafu unakuta mwanaume anataka kufahamu mshahara wa mkewe lakini wake mh ni siri yake
 
Back
Top Bottom