Fahamu kuhusu matumizi ya OverDrive (OD) kwenye gari automatic

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
sddefault.jpg

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU
Wakuu naomba kufahamishwa, ni mahala au muda gani natakiwa kutumia OverDrive funcionality kwenye auto transmission. Ni kwa Ufahamu tu

Nawasilisha
---
Hello GREAT THINKERS!
Nimekutana na huu ubishani kuwa ni wakati gani Over drive facility inatumika katika gari? Je ikiwa off inaonekana vipi kwenye dashboard? Thanks
---
wakuu

ni nini hasa matumizi ya Over Drive kwenye gari yenye automatic gear (transmition), je hutumika wakati gani haswa yaani ni wakati gani na speed gani inatakiwa iwe on au off... what are the pros and cons?

Ahsanteni
---
Wadau naomba msaada kwa anayejua au kufahamu matumizi sahihi ya O/D, Haya Magari yetu ya kisasa, (Automatic) yana vitu vingi nahisi watu wengu atufahamu.

Hasa Matumizi sahihi ya Over Driving itumike au inatumika wakati gani,na wakati gani inakuwa on na wakati gani inakuwa off.Wadau naombeni msaada wenu, hii O/D inakuwa on pale taa ya O/D Inapoonyesha O/D OFF au isipoonekana kabisa?

Na hii O/D itumike muda gani napoendesha gari?

Naomba msaada wenu wadau.

UFAFANUZI WA JUMLA WA MATUMIZI YA OD

Overdrive ni nini?
Overdrive ni gia katika mfumo wa gari ambayo uifanya gari kuwa katika spidi kubwa huku mzunguko wa injini ukiwa mdogo. Kwa lugha rahisi, OD ni gia ya mwisho inayokupa mwendokasi ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

Over drive ni kama gia ya ziada itakayokupa mizunguko mingi ya driving shaft kwa mizunguko michache ya engine yako. Unapaswa kuitumia ukiwa unatembea na mwendo mkubwa. Faida zake utatumia mafuta kidogo mana gari inakwenda kasi kwa mizunguko michache ya engine. Mfano katka gari ya kawaida yani 180km/h ili ufikishe speed 120km/h basi rpm inaweza kua 4000rpm. Katka barabara tambarare. ila ukiweka over drive unaweza tembea speed hiyo hiyo kwa rpm 2000 katika barabara tambarare.

Utajuaje kuwa Overdrive ipo On au Off?
Pindi uonapo kitaa cha overdrive kwenye dashboard ya gari yako inamaanisha kuwa Overdrive ipo off na pindi Kitaa cha overdrive kisipoonekana basi overdrive ipo on. Overdrive imewekwa Kama option yakutumia wakati ukiwa unatembelea speed chini ya 60km/h.

1592113600875.png


Matumizi ya Overdrive ni yapi?
Unaweza kuitumia pia ikiwa unataka kuipita gari nyingine, mathalan, kwenye kilima ambapo nawe gari yako inakuwa imepungua nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4), na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka ukisha maliza tena matumizi yake.

Eneo lingine, ni mara gurudumu la motaklaa yako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa motokaa pia.

Watu wengine katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa motokaa, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea motokaa kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lilipasuka, nikiwa na maana kwamba hapo motokaa itakuwa inaacha njia na au kupinduka.

Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo.

Kitaa cha Overdrive kikiwa hakionekani kwenye dashboard yako maana yake Overdrive ipo Automatic au On na hivyo ndivyo inavopendekezwa na wataalam gari iwe automatic pindi upo mjini na unatembelea speed tofauti (sometimes less or more than 60)..kwa vile overdrive inatumia gear kubwa na speed less than 60km kwahio unaweza kutumia wakati unashuka milima mikubwa.

UFAFANUZI NA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU WA JF
Keizer, Ndege ya Uchumi salaam!

Kwa lugha rahisi, OD ni gia namba 5 ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

Unaweza kuitumia pia ikiwa unataka kuipita motakaa nyingine, mathalan, kwenye kilima ambapo nawe motakaa yako inakuwa umepungua nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4), na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka uklisha maliza tena matumizi yake.

Eneo lingine, ni mara gurudumu la motaklaa yako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa motokaa pia.

Watu wengine katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa motokaa, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea motokaa kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lilipasuka, nikiwa na maana kwamba hapo motokaa itakuwa inaacha njia na au kupinduka.

Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo.
---
Kwa ninavyofahamu mimi, overdrive ni kama walivyoeleza waliotangulia ila, kama iko off maana yake unaifanya gari iweze isiweze kwenda mpaka gear ya mwisho. Kama ina 7 speed itaishia 6. Kama ni 4 speed itaishia 3. Ukiangalia kweye gear lever yako kutegemea na gari lako utagundua yafuatayo. P R D 4 3 2 L AU 1. Mengine P R D 2 L AU

1. Ukiweka kwenye L means gari itakuwa kwenye gear ya 1 na haitaruka hapo. Hapo ni kama unavuta gari au unashuka mteremko mkali sana ili kupata engine braking au kupanda mlima mkali sana au kutoka kwenye matope kama umezama. Ukiweka 2 inakuwja inaishia hapo kwenye gear ya pili na haiendi zaidi.

Hapo ni kama upo kwenye barabara mbaya sana na unajua huhitaji gear zaidi ya hiyo. Hapa unaipunguzia kazi gear box yako na hata kuiongezea maisha. Ukiweka 3 the same inaishia hapo. Wameweka hivi makusudi kwa kuwa ikiwa D itakuwa inajaribu kufanya kazi sana ya kutafuta gear kutokana na motion ya gari.

Hapa sasa kuna makundi mawili. Hilo la P R D 2 L ndiyo common hapa na ndiyo zenye kidude cha kubonyeza. Kikiwa OFF taa itakuwa inawaka kwenye dash na kikiwa ON Haitowaka. Kama iko OFF maana yake gari haitokuwa inapata support ya engine kwenye kusimama kama vile kupangua kwa wale wenye manual transmission.

Ni brake tu itatumika. Advantage ya kutumia overdrive ni kwamba gari inatumia mafuta kidogo kwa kuwa ukiachia mafuta gari litakuwa neutral. Kama lingekuwa kwenye OD OFF litakuwa kwenye gear likijipangua lenyewe na hapo maana yake mafuta yatatumika mengi. Kundi hili mara nyingi transmission zake hazizidi 4 speed na kama itazidi ni 5 but ni chache sana. Zenye P R D 4 3 2 L AU 1 ni zenye hadi 7 speed. Nyingi ni za kisasa na zenye mambio mengi.

Hizi wamekurahisishia. Badala ya kile kiswitch cha OD wamekuwekea hizo 4 3 nk. Hazina hako kadude tena. Na sina uhakika kama hiyo button ina mahusiano na kuongeza nguvu ya gari zaidi ya haya maelezo niliyotoa. Ila kwenye magari baadhi kuna buttons kwa ajiri ya kazi hiyo na imeandikwa Power/ Normal.

Ukiibofya itaaeika kwenye dash pia. Power kwa maana ya kwamba, kama gear ya kwanza ingechange katika speed 10 kwa mfano, then itachange katika speed 30. Hapa ni kwamba unataka mbio. Bei ya mafuta tunaifahamu kwa sasa nadhani. Hayo ni maelezo kwa jinsi mimi nijuavyo jamani.
---
Niliwahi kureply hii post kuhusu OD. Baada ya kuwa na project ya kubadilisha engine kwenye gari na kuweka engine tofauti na ile ilokuja na gari ndio nikapanua uelewa wangu kwenye overdrive.

OD ni highest gear. Kwaio kama gearbox yako ina gear nne za kuendesha, ile namba nne ndio over drive (ON). Kuna baadhi ya magari pale kwenye shifter utakuta P R N D 3 2 L.

Ukiweka kwenye 3 maana yake OD iko Off, ukiweka kwenye D manake OD ipo ON na gari inaweza kuchanga kutoka 3 kuingia gear ya 4. Gari zenye mfumo huo, huwa hazina button ya overdrive wala kwenye dashboard hakuna taa ya OD off.
---
Ndugu yangu Overdrive ni GEAR ya mwisho katika gearbox. usiangalie hapo juu unapoendesha, sisi tunazungumzia ndani kabisa ya gearbox kuna gea ya mwisho .km ni 4 au ni 12 kwa Scania ndio huitwa Over drive gear. kuna mahali tulizungumzia humu ndani tukamaliza. labda nirudie
View attachment 1473280
kwenye engine kuna gear namba 1 mpaka ya mwisho km ni 3,4 au 12 ile ya mwisho huwa ni ndogo kuliko mzunguko wa Crankshaft (Driver gear) inayozungushwa na piston, kwa hiyo mzunguko wake kwa diameter uatakiwa uwe mdogo ili gari ikimbie na kutumia mafuta kidogo na sio Overdrive ni ya kuanzishia gari katika 0 km/h au kupandia milima, hata baiskeli wana overdive gear
Overdrive or OD is the highest gear in the transmission in an automatic car. It brings the RPM of the engine down at a given road speed to facilitate better speed and fuel efficiency. It also helps your car to provide the best performance in higher speed cruising. Overdrive helps when you drive at more than 50mph.
---
Nimesema overdrive ni kama gia ya ziada inayokupa mizunguko mingi ya driving shaft kwa mizunguko michache ya injini yako. Unapaswa kuitumia ukiwa unatembea mwendo mkubwa na kwenye highway huwa kwa kawaida unakuwa kwenye mwendo mkubwa. Faida zake utatumia mafuta kidogo, maana gari inakwenda kasi kwa mizunguko michache ya injini.Pia nimesema

Unaweza kutumia OD ukiwa unataka kuipita gari nyingine, mathalani kwenye milima ambapo gari yako inakuwa imepunguza nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4) na injini itabadili kasi ya mzunguko.Hii ni kwa sababu overdrive (OD) ni gia katika mfumo wa gari ambayo huifanya gari kuwa katika spidi kubwa huku mzunguko wa injini ukiwa mdogo. Kumbuka kuondoa OD
ukishamaliza matumizi yake.
So uko sahihi mkuu.
---
Kuwa makini:

(a) Kuna magari mengine taa zake za OD zinapowaka zinaashiria kuwa OD iko OFF.

(b) Kama unatumia Autotransimission, usitumie OD kwa safari za mjini ambapo unagemea kusimamasima mara kwa mara. Kufanya hivyo, utachakaza transimission yako haraka sana kwa sababu itakuwa inaruka kutoka gia ya kwanza hadi ya tano na kurudi gia ya kwanza kwa muda mfupi, jambo ambalo siyo zuri kwa hizi autotransimission. Ili uelewe jambo hilo, hebu fikiria kama unadandia mwamba wa juu wa goli; mwamba ule utapinda kidogo kabla ya kunyooka tena na kutulia. Sasa kama utaudandiadandia mwamba ule harakaharaka kwa kujirudiarudia basi baadaye mwamba unaweza kupinda kabisa usinyooke tana na hata kuvunjika.

Sielewi kwa Dar es Salaam bei zikoje, ila kwa jumla gharama za matengenezo ya autotransmission huwa ni kubwa sana.
---
1. Kuna watu wana lalamika gari halina nguvu hasa anapo kanyaga mafuta kwenye mwinuko.

2. Kina watu break zimefeli na wana shangaa kwa nini?

3. Kuna watu wana lalamika magari yao kutumia mafuta zaidi .


Sasa fata yafuatayo hutajua.

Kama speed yako ni chini ya 50KM/Hr hakikisha OD/OFF inasoma kwemye dashboard.

Kama unashuka mlima au unatumia break hakikisha OD /OFF inasoma kwenye dashboard.

Kama una kanyaga mafuta ili kuongeza mwendo wa gari hakilisha OD/OFF inasoma kwenye bashboard.

Kama unapanda mlima hakikisha OD/OFF inasoma kwenye dashboard.

Kama una overtake hakikisha onaweka OD OFF.

Wapi OD inatakiwa kuwa ON?
Ni pale tuu speed imezidi 50 na huhitaji kukanyaga mafuta wala break.

Kusave mafuta kwenye highway.

Weka od off ikisha shika speed kuanzia 80 rudisha OD ON , utahisi gari haina engine..

Onyo

Kwa watu wa automatic ambao hawajui kutumia mikono yote miwili wakati wa iuendesha unaweza ishia machakani maana garinukiibadili kwenda oberdrive inakimbia utadhani imekata roho.

Gari ikiwa kwenye OD ni zaidi ya gari manual ikiwa kwenye neutral.

Unapo tumia break wakati OD ipo ON umaziukiza break kwa sababu hazipati msaada wa engine.
---
Niliwahi kureply hii post kuhusu OD. Baada ya kuwa na project ya kubadilisha engine kwenye gari na kuweka engine tofauti na ile ilokuja na gari ndio nikapanua uelewa wangu kwenye overdrive.

OD ni highest gear. Kwaio kama gearbox yako ina gear nne za kuendesha, ile namba nne ndio over drive (ON). Kuna baadhi ya magari pale kwenye shifter utakuta P R N D 3 2 L.

Ukiweka kwenye 3 maana yake OD iko Off, ukiweka kwenye D manake OD ipo ON na gari inaweza kuchanga kutoka 3 kuingia gear ya 4. Gari zenye mfumo huo, huwa hazina button ya overdrive wala kwenye dashboard hakuna taa ya OD off.
---
Magari mengi ya automatic gear from 2000 hayana hii kitu........ni old technology

Overdrive is a term used to describe a mechanism that allows an automobile to cruise at sustained speed with reduced engine speed, leading to better fuel consumption, lower noise and lower wear. Use of the term is confused, as it is applied to several different, but related, meanings.

The most fundamental meaning is that of an overall gear ratio between engine and wheels, such that the car is now over-geared and can no longer reach its potential top speed, i.e. the car could travel faster if it were in a lower gear, with the engine turning more quickly. The purpose of such a gear may not be immediately obvious. The power produced by an engine increases with the engine's speed to a maximum, then falls away. The point of maximum power is somewhat slower than the absolute maximum speed to which the engine is limited, the "redline" speed. A car's speed is limited by the power available to drive it against air resistanceso the maximum possible speed is obtained at the engine's point of maximum power, or power peak, and the gear ratio necessary to achieve this will be the single ratio between these two speeds.

As the power needed increases dramatically at high speeds, most cars will be capable of achieving a fast cruising speed slightly less than their maximum, but with far less power being required. This power is available well below the engine's power peak and so the ideal cruising gear is an overdrive gear, a ratio higher than that for absolute top speed.

With the early development of cars and the almost universal rear-wheel drive layout, the final drive (i.e. rear axle) ratio for fast cars was chosen to give the ratio for maximum speed. The gearbox was designed so that, for efficiency, the fastest ratio would be a 'direct-drive' or 'straight-through' 1:1 ratio, avoiding frictional losses in the gears. Achieving an overdriven ratio for cruising thus required a gearbox ratio even higher than this, i.e. the gearbox output shaft rotating faster than the original engine speed. The propeller shaft linking gearbox and rear axle is thus overdriven, and a transmission capable of doing this became termed an "overdrive" transmission.

The device for achieving an overdrive transmission was usually a small separate gearbox, attached to the rear of the main gearbox and controlled by its own shift lever.These were often an optional extra on some models of the same car.As popular cars became faster relative to legal limits and fuel costs became more important, particularly after the 1973 oil crisis, the use of 5-speed gearboxes became more common in mass-market cars. These had a direct fourth speed with an overdrive top gear, replacing the need for the separate overdrive gearbox.

With the popularity of front wheel drive cars, the separate gearbox and final drive have merged into a single transaxle. There is no longer a propeller shaft and so one meaning of "overdrive" can no longer be applied. However the fundamental meaning, that of an overall ratio higher than the ratio for maximum speed, still applies. Although the deliberate labelling of an overdrive is now rare, the underlying feature is now found across all cars.
---
O/D, hii ni function inayokupa uchaguzi. Au gari iwe nyepesi na kwenda haraka ama iende kawaida. Unapoendesha gari na kuhisi imekuwa nyepesi basi angalia kwenye dash-board ili ujue je, gari iko kwenye O/D au la. Utajuaje?

Fanya mazoezi ukiwa ktk mahegesho swicht on kisha bonyeza button ya O/D (itabonyea ndani) na angalia dashi bodi inaonyesha nini. Utakachokiona ndicho kitakachokuambia gari iko kwenye O/D.

Ikiwa imebonyea. kisha ibonyeze tena ile button (itachomoza nje), angalia dashi bodi inaonyesha nini. Hii itaonyesha gari haiko kwenye O/D. Matumizi ya O/D. ni kuifanya gari iwe nyepesi na kwenda haraka.

Ideal kama unasafari za high way na siyo misongamano kama ya Dar. Kwa hiyo ukigundua kuwa uko kwenye O/D sehemu kama Traffic jam za Dar unashauriwa kuiondoa O/D. Kuhusu wese: O/D inakula wese dogo mno kuliko hata la AC.
---
Overdrive (OD) is a term used to describe a mechanism that allows an automobile to cruise at sustained speed with reduced engine RPM, leading to better fuel economy, lower noise and lower wear.

Use of the term is confused, as it is applied to several different, but related, meanings.The most fundamental meaning is that of an overall gear ratio between engine and wheels, such that the car is now over-geared and can no longer reach its potential top speed, i.e. the car could travel faster if it were in a lower gear, with the engine turning more quickly. In some cases this implies a second definition is also true, that the gearbox output driveshaft is rotating faster than the original engine RPM. This later definition was common in the past, but many cars no longer have a driveshaft and it is not technically correct

In the era of front-engine, rear-wheel drive layouts, the device for achieving an overdrive transmission was usually a small separate gearbox, attached to the rear of the main gearbox and controlled by its own shift lever or electrical actuation button. These were often an optional extra on some models of the same car. As popular cars became faster relative to legal limits and fuel costs became more important, particularly after the 1973 oil crisis, the use of 5-speed gearboxes became more common in mass-market cars, with the 5th gear being an overdrive, eliminating the need for a separate gearbox.

With the popularity of front wheel drive cars, the separate gearbox and final drive have merged into a single transaxle. However the fundamental meaning, that of an overall ratio higher than the ratio for maximum speed, still applies. Although the deliberate labeling of an overdrive is now rare, the underlying feature is now found across all cars.

Source: Overdrive (mechanics) - Wikipedia, the free encyclopedia
---

Overdrive (OD) ni gia katika mfumo wa gari ambayo huifanya gari kuwa katika spidi kubwa huku mzunguko wa injini ukiwa mdogo. Kwa lugha rahisi, OD ni gia ya mwisho inayokupa mwendokasi. OD hukupa mwendo wa kasi, uliotulia lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (revolutions per minute rpm). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

Overdrive ni kama gia ya ziada inayokupa mizunguko mingi ya driving shaft kwa mizunguko michache ya injini yako. Unapaswa kuitumia ukiwa unatembea mwendo mkubwa. Faida zake utatumia mafuta kidogo, maana gari inakwenda kasi kwa mizunguko michache ya injini.

Mfano katika gari ya kawaida yaani 180km/h ili ufikishe spidi 120 basi RPM inaweza ikawa 4000rpm katika barabara ya tambarare. Lakini ukiweka overdrive unaweza kutembea spidi hiyo hiyo kwa rpm 2000 katika barabara ya tambarare.

Utatambuaje kama Overdreive (OD) ipo on au off?

Pindi uonapo kitaa cha overdrive kwenye dashboard ya gari yako, inamaanisha kuwa overdrive ipo off na pindi kitaa hicho kisipoonekana basi tambua kuwa overdrive ipo on. Overdrive imewekwa kama chaguo (option) la kutumia wakati ukiwa unatembelea spidi chini ya 60km/h.

Unaweza kutumia ukiwa unataka kuipita gari nyingine, mathalani kwenye milima ambapo gari yako inakuwa imepunguza nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4) na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka ukishamaliza tena matumizi yake.

Eneo lingine, ni mara gurudumu la gari lako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa gari pia.

Katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa gari, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea gari kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lililopasuka, nikiwa na maana kwamba hapo gari itakuwa inaacha njia na au kupinduka.

Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo

Kitaa cha Overdrive kikiwa hakionekani kwenye dashboard yako maana yake Overdrive ipo Automatic au on na hivyo ndivyo inavopendekezwa na wataalam gari iwe automatic pindi upo mjini na unatembelea speed tofauti (sometimes less or more than 60)..kwa vile overdrive inatumia gia kubwa na mwendokasi chini ya 60km kwahiyo unaweza kutumia wakati unashuka milima mikubwa

Chanzo: Mwananchi
 
Mkuu Over drive inakuja unapotaka kwenda speed zaidi ya 80,so gari inakuwa na uwezo wa kuingia gia no 5
 
Kwa hiyo mkuu utaona kuwa kwa mazingira yetu ya Dar mara nyingi OD inabidi iwe on (na ikiwa off huwa inawaka taa either kwen dashboard) kuonyesha kuwa iko off na u have to think kwa nini iwe off.

Mi binafsi naiweka off kama ninataka kuachieve speed kubwa kama kuovertake chap chap kisha kuirudisha on. Ikiwa off inakula sana wese.

Source: Wikipedia.
 
Keizer, Ndege ya Uchumi salaam!

Kwa lugha rahisi, OD ni gia namba 5 ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

Unaweza kuitumia pia ikiwa unataka kuipita motakaa nyingine, mathalan, kwenye kilima ambapo nawe motakaa yako inakuwa umepungua nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4), na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka uklisha maliza tena matumizi yake.

Eneo lingine, ni mara gurudumu la motaklaa yako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa motokaa pia.

Watu wengine katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa motokaa, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea motokaa kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lilipasuka, nikiwa na maana kwamba hapo motokaa itakuwa inaacha njia na au kupinduka.

Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo.
 
Keizer, Ndege ya Uchumi salaam!

Kwa lugha rahisi, OD ni gia namba 5 ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi...

Mkuu Mbalamwezi Shule kubwa sana hii na inabidi watu wengi zaidi waifahama maana kila kukicha bei ya Mafuta inapaa kama Ndege ya Uchumi ya EL.

Asanteni wakuu kwa maelezo yenu mazuri na Jengefu
 
mimi nilikuwa naitumia kwenye rafu roads kwani nikiweka huwa gari inakuwa zito hivyo nikitaka kuwahi huwa nazima kweli wajapani tunawahitaji kwa maelezo ya product zao
 
hii thread imenielimisha sana jamani,asante kw aalieuliza na waliotoa majibu mazuri na murua kabisa,ninatumia auto sometimes so nitaiweka OD on mda wote!!
 
Keizer, Ndege ya Uchumi salaam!

Kwa lugha rahisi, OD ni gia namba 5 ambayo inakupa mwendo uliotulia, wa kasi lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (RPM). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi....
Mkuu asante umesomeka vizuri sana.
 
hii thread imenielimisha sana jamani,asante kw aalieuliza na waliotoa majibu mazuri na murua kabisa,ninatumia auto sometimes so nitaiweka OD on mda wote!!

JF ni kila kitu, Majibu ya Maswali yako yote yako hapa Jamvini Mkuu, wewe ni sula la ku initiate, Watu si Wachoyo hapa.

Asanteni
 
Ila drive gari manual kuna raha yake. Bongo siku hizi waendeshaji ni wengi sana, madereva ni wachache. Nilikuwa na gari yangu manual kutaka kuiuza kila mtu akiiona anasema ingekuwa automatic angenunua kwa bei ninayotaka mimi, vinginvyo nipunguze bei. Nikaamua kuahirisha mpango wa kuiuza LOL!
 
huyo aliyesema ukivuka 80 kpm unatumia mafuta kidogo sidhani kama ni mkweli.unavyokanyaga zaidi ndo mafuta yanakwenda zaidi.theory hiyo inawork kama uko kwenye speed kubwa zaidi kama 140 kmp au zaidi au chini ya 80.otherwise overdrive ni kwenda gear number 5 na kwa mazingira ya day iweke off daima kwani wataalam wanasema kuiacha on saa zote ina damage engine kinamna achilia mbali suala la consumption kubwa
 


Kwa hiyo mkuu utaona kuwa kwa mazingira yetu ya Dar mara nyingi OD inabidi iwe on (na ikiwa off huwa inawaka taa either kwen dashboard ) kuonyesha kuwa iko off na u have to think kwa nini iwe off,

Mi binafsi naiweka off kama ninataka kuachieve speed kubwa kama kuovertake chap chap kisha kuirudisha on. Ikiwa off inakula sana wese.

Source: Wikipedia.

Kaizer,

Kufuatana na maelezo yako kny quote ya mwanzo kabisa, malelezo hayo hapo juu si sahihi....ni kinyume!



Huwa unakosea kama huwa unafanya hivyo kweli, unaiumiza gari yako na pia unamaliza sana wese mkuu!


Generally speaking, overdrive (OD) is the highest gear in the transmission. Overdrive allows the engine to operate at a lower rpm for a given road speed. This allows the vehicle to achieve better fuel efficiency, and often quieter operation on the highway. When it is switched on, an automatic transmission can shift into overdrive mode after a certain speed is reached (usually 70+ km/h [43+ mph] depending on the load). When it is off, the automatic transmission shifting is limited to the lower gears. For an automatic transmission, it is almost always best to select overdrive and allow the transmission to control engagement of the overdrive. (It may be necessary to switch it off if the vehicle is being operated in a mountainous area or when towing a trailer). With a manual transmission, overdrive should usually be selected when the average speed is above 70 km/h (approx. 43 MPH).


Mkuu,, asante kwa observation yako, laikini ukisoma maelezo yangu ni kuwa kwanza yamebase kwa gari automatic, na kwa mujibu wa hiyo article ya wikipedia, best practice ni kuhave your OD on, na kuiachia gari ichague yenyewe ni gia gani inafaa kulingana na mwendokasi wa gari, ila kwa hali ngumu za barabara au gari mfano kwenye rough roads, milima nk inabidi uiweke off ili kuifaya gari iwe na nguvu zaidi (kwa kuwa na mzunguko mkubwa wa engine-RPM)

Utanote kuwa unaposelect OD, RPM inashuka, ukiiweka off, RPM inakuwa juu, na nadhani unaelewa uhusiano wa RPM na ulaji wa mafuta mkuu.
 
huyo aliyesema ukivuka 80 kpm unatumia mafuta kidogo sidhani kama ni mkweli.unavyokanyaga zaidi ndo mafuta yanakwenda zaidi.theory hiyo inawork kama uko kwenye speed kubwa zaidi kama 140 kmp au zaidi au chini ya 80.otherwise overdrive ni kwenda gear number 5 na kwa mazingira ya day iweke off daima kwani wataalam wanasema kuiacha on saa zote ina damage engine kinamna achilia mbali suala la consumption kubwa

Mdudu,

acha kudhani dhani juu ya mambo ya kitaalam. motakaa katika hali ya kawaida, na kwa wastani, inatumia mafuta mafuta kidogo kabisa ikiwa kwenye mwendo wa kati ya 70 km kwa saa na 110 kwa saa. Ukizidi hapo, unakuwa kwenye matumizi ya juu kabisa.

RPM (Revolution per minute) ni kiwango cha mzunguko wa injini. Ikiwa unatumia gia namba 4 hadi mwendo kasi wa 70 km kwa saa, basi inawezekana, kama injini ni nzuri, RPM ikawa kwenye 2600-2800 hivi kama uko kwenye mpango wa OD, basi motokaa yako itabadili gia na kuingia kwenye 5, ambayo ni OD, na ukizidisha hadi kati ya 80 na 90 hivi, basi RPM itapungua hadi kufikia 2200 hadi 2500 hivi.

Maana yake nini? Maana yake injini sasa itazunguka mara chache zaidi kwa mwendo kasi zaidi (70km/h hadi 110 km/h).

Ukizidisha toka 120km/h na kuendelea, basi na RPM zitaongezeka na mafuta yatanywewa mengi tu.

Auto zinafaa sana kwenye foleni kama za Dar, ambako unaepuka sana matumizi ya kilachi (clutch), maana unajikuta mguu wa kushoto unakuwa busy kukanyaga kanyaga ndani ya mita pengine 200 tu katika dk 45 pale Moroko saa mbili asubuhi.

Manual zinafurahisha long trips, unajidai na unajisikia hasa unaendesha. Unaweza kuiamuru gari kwenye milima iende upesi zaidi, si kama auto ambayo inapanga yenyewe. Unaweza kumpita mwingine kwa wepesi wa hali ya juu, si kama auto ambayo itabidi uondoe OD ndo uongeze kasi ya kumpita.
 
Ila drive gari manual kuna raha yake. Bongo siku hizi waendeshaji ni wengi sana, madereva ni wachache. Nilikuwa na gari yangu manual kutaka kuiuza kila mtu akiiona anasema ingekuwa automatic angenunua kwa bei ninayotaka mimi, vinginvyo nipunguze bei. Nikaamua kuahirisha mpango wa kuiuza LOL!
Sasa hivi magari ya manual ya kutoka Japan yanauzwa bei ghali zaidi kuliko ya automatic.
 
Mdudu,

acha kudhani dhani juu ya mambo ya kitaalam. motakaa katika hali ya kawaida, na kwa wastani, inatumia mafuta mafuta kidogo kabisa ikiwa kwenye mwendo wa kati ya 70 km kwa saa na 110 kwa saa. Ukizidi hapo, unakuwa kwenye matumizi ya juu kabisa...
Kwa mawazo yangu (nina magari yanayotumia manual na automatic), gari la automatic ni nzuri sana kwa safari ndefu. Infact unaweza kubadilisha gear, k.m.

Kama unataka ku overtake, sio kwa kutumia OD, bali kwa kukandamiza accelerator kwa nguvu ghafla. Kitendo hicho (kickdown) kitabadilisha gear na kuweka gear yenye nguvu ya kuweza kuongeza kasi na ku overtake.
 
gari la automatic ni nzuri sana kwa safari ndefu. Infact unaweza kubadilisha gear, k.m. kama unataka ku overtake, sio kwa kutumia OD, bali kwa kukandamiza accelerator kwa nguvu ghafla. Kitendo hicho (kickdown) kitabadilisha gear na kuweka gear yenye nguvu ya kuweza kuongeza kasi na ku overtake.

Ni hakika Dingi unenavyo, na kwa namna hiyo hiyo pia unaweza kubadili gia kwenda ndogo kwa kuachia pedeli ya mafuta kila kipimo cha mwendo kinapofikia mafunda ya 20, mfano ikifika 20km/hr ukiachia pedeli ghafla (kick up) itaingia namba 2, ikifika 40km/hr ukaachia pedeli ghafla itaingia namba 3, ikifikia 60km/hr itaingia 4, na ikifikia 80km/hr itaingia namba 5, OD.
 
Mkuu mbalamwezi, nashukuru kwa elimu uliyotoa, mie nilikuwa sijui hata ina maana gani,wala hata kuitumia.

Big up wazee wa humu jamvini.
 
Back
Top Bottom