Out of Touch: Madhara ya kusafiri mara kwa mara?

Kwanza anashangaza sana. Yani Mkulu aliweza kuhairisha siku kadhaa kwenda KUHAFALIKA na PhD fake kwa ajili ya kuepusha ngumi ndani ya NEC, lakini kaondoka wakati Watanzania wasio na hatia wameuawa kule Musoma. Si shangai kwani hata Kilosa walipo pata janga la mafuriko, jamaa alikuwa ana Watch gemu la Ivory Coast V/S Taifa gizas.
Wataalam wa kumbukumbu tuhabarisheni, hivi jamaa hajaingia kwenye Ginness Book kwa kuvunja rekodi ya kusafiri kuliko Marais wote duniani!!!? Halafu eti anawaambia Mabalozi wa Afrika nchini Uturuki eti wahamasishe kupata misaada. Hajui wenzake sera zao ni za kujitegemea na sio UMATONYA wa kutembeza bakuli duniani!!!
 
Ukweli mimi niko bongo nawambia ndugu zako mambo si shwari wala bongo si tambarare kama wanasiasa wanavyowataka nyie muamini huku tuna mambo mengi kwanza mfumuko mkubwa wa bei na vitu vinavyokwaza lukuki...........
 
Ni siasa tu nakumbuka hata Tarriq Aziz aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Iraq alikuwa akisema ole wao wamarekani waingie huko watazikwa huko huko lakini kumbe alikuwa akijua kuwa saddam anachimba mtaro atakamo chificha.

So hata JK anajua kabisa kuwa issue ni noma lakini akiwa nje lazima aonyeshe eti naye ni kidume.
 
Jamani Rais ni Mwanasiasa. Na Mwanasiasa yoyote mwerevu hawezi kuwapa hofu kirahisi watu wake. Sasa mlitaka awaambie 'Chonde chonde hali ni mbaya sana nyumbani ndio maana napakimbia. Jamani msirudi kabisa hapakaliki kule, yaani ni migogoro mpaka tunalia vikaoni!' Shabash! Mwacheni Mwanasiasa awe Mwanasiasa!
 
Kukaa sana nje kuna madhara...we stop living in the world of reality and start living in the world of fantasy.
Ukiona mtu mzima anasema shwari wakati kuna mambo mengi hayaendi sawa maana yake nini? Inawezekana anafuata nyayo za Hitler wakati amejificha kwenye banker akiamini nje ya banker kuna askari wanaopigana kwelikweli ili kumnusuru.
Angekuwa anaenda mwenyewe nje kujionea naamini hali ingekuwa tofauti na vile alivyokuwa anafikiri.
 
Mimi ningewaambia kila kitu shwari Elimu yetu inazidi kukua kila Mwaka, si mnaona wenye matokeo ya Kidato cha nne yalivyo

Division I + II + III = 42,627 sawa na Asailimia 17.85

Divisheni IV = 130,651 sawa na Asilimia 54.66

Divisheni 0 ( Sifuri) = 65,708 sawa na Asilimia 27.49

Kwa hiyo msiwe na wasiwasi kwa maana hao Vijana Veri suni watawajoini huku Ugaibuni kukata shule ya Juu
 
Kila kitu ni 'shwari' Bandari ya Salama kama bango hili na utitiri huu wa magari unavyojieleza!​

IMG00010-20100217-1721%5B1%5D.JPG
 
Companero,

Hilo bango liko wapi? Linatangaza nini haswa? Nani analilipia?
 
Injinia maswali mengi ya nini, jali kuwa umeshatengenezewa mazingira 'shwari' ya biashara Bongo!
 
Si hivyo p53 (by the way which tumour are you preventing? - inside joke)

Ni kwamba Rais ametuangusha wengi tuliokua na matumaini mengi kwake.
Hasa mimi. Mwanzoni alikua ananisisimua kwa ari yake. Sasa hivi, mh!

Mimi ninachosema ni hivi, kwa nini asiwe mkweli aawambie tu wananchi hali ya kisiasa ni hivi na vile, na sio kusema ni shwari wakati sote twajua sio. Hayo mambo ya "kila kitu shwari" ni ya kusema kwa watu wa nje, watoto wa nyumbani unawaambia ukweli bwana

Yaani Injinia upo serious ulikuwa na matumaini mengi kwa rais? pole sana
 
Mind your own business, LOL!

That wasn't very nice! What goes on in my country is my business!!
I am asking because all I can see on that billboard is a picture of the president tying the shoe laces of a school boy. Unless you tell me it is a kind of "watch this space" advert or that it has some abstract meaning, I just don't get it.

Au unahusika na uwekaji wake ndugu? Nimegusa pabaya?
 
Yaani Injinia upo serious ulikuwa na matumaini mengi kwa rais? pole sana

Asante bwana, kweli nilikuwa na matumaini naye pale mwanzo alianza na ari flani hivi ya kusisimua, niliona kama ni mwanamapinduzi flani hivi. Lakini hapa nazungumzia mwaka 2006, mind you!!
 
Injinia hiyo picha imekwa tu hapo kukuonesha jamaa ana maana gani anaposema nchi iko 'shwari'. Kama nchi ina hela za kutosha kuweka hayo mabango, kununua migari ya nguvu mpaka kunakuwa na foleni za kufa mtu kwa nini awaambie vijana huko Uturuki kuwa hali ni mbayanyumbani? Naam kwa nini awaambie wateule wenzake wanaoweza kuja kuitumia hali hii ya 'shwari' kununua hisa kwenye Bariki Dhahabu na kuwekeza kwenye Kilimo Kwanza na Ukandarasi wa Umeme? Yuko sahihi kabisa maana nchi iko 'shwari' kabisa kwenu wateule!
 
Back
Top Bottom