Out of my league!

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,694
58,763
Nimejikuta najiuliza kitu ikabidi niwaulize na nyie dadaz n kakaz!!!

Hivi mtu anapomwambia mwenzake 'we huendani na mimi....mimi huniwezi wewe...mi sio saizi yako' na mengine kama hayo huwa wanatumia vigezo gani kuona kwamba huyo mtu mwingine hana UBORA sawa na wao? Ni pesa....sura au tabia?

Vyoyote vile je ni haki kumwambia mtu mwingine maneno ya aina hiyo?I mean kumdharau mwenzako...kumpunguzia kujiamini au hata kumfanya ajione duni kunakusaidia nini?

Surely wapo humu waliowahi kutenda na kutendewa hivyo..hua inatokea sana wakati wa kutongozana...hata wengine mtu akimuuliza direction tu ishakua tabu!

Nywz my point is kama unamchukia mtu au unaona mtu anakuboa why not just walk away bila kumfanya yule mtu aanze kujiskia vibaya!?

Kua mstaarabu wafanyie wenzako vile ambavyo ungependa ufanyiwe....usionyeshe dharau iwapo wewe unataka kuheshimiwa!!!

My qoute of the day: Ubora wa mtu sio kitu ni utu!!

By Lizzy

Weekend njema.....y'all be good!!!
 
Wanaume hasa ndio tunakumbwa na hiyo kadhia ya kutukanwa na wadada tunapowatongoza utafikiri kutongoza ni dhambi au kosa la jinai.

Kumbuka hata Askofu unayemuona ana mke basi mjue lazima alipitia hutua ya utongozaji ili ampate huyo mke.

Kwa uelewa wangu nadhani ni Adamu wa kwanza tu ndio hakutongoza.
 
Kabisa kaka, wadada especially wanaojifanya high maintenance ndio zao hizo.
 
Mi nianze kwanza kujibu kuwa SI HAKI.... not now, not ever

Waanaosema hivo wako makundi mawili...
1. wale wanaojiona (wazuri sana, matawi sana, classy sana, wanaelim sana), so any of these sababuz zinawafanya watu wawe na majibu yasio na busara........ontop of that utakuta katongozwa sana, so anaona what the heck?, hapa ni mtakuja, so I gat choose the "BEST", so wale wenzangu na mie wanaambulia hayo majibu....

2. Na wale wanaomanin kuwa kumjibu mtu "vibaya", "kutamfukuza", si unajua kuna watu wamejaaliwa uvumilivu wa kusubiri majibu, maana nimesikia watu wakisema, mtu ukimwambia "haiwezekani, while smiling", ye anaelewa, "am playing hard to get"... so huyu mtu anaona akimpa majibu ya kumshusha hadhi, huyo hawezi kubaki.........although its still a bad technique, maana at the end of the day, utajitengenezea maadui wangapi?????

ON THE OTHER SIDE:
Mi huwa nashangaa sana, hivi kwa nini mtu akiwa anakufatilia, ukamwambia mi nna mtu, akapress harder, akaona jibu bado lile lile, anaanza, "Kwani nani hana mtu? kwanza ana nini yule, yule kwanza hata hamuendani, kwanza sio size yako, hivi ulishawahi kupendwa, mi ntakupenda mpaka usahau kulikuwepo kiumbe kama yule, sijisifii ila mi najua sana kumpenda mwanamke", halafu ole wake awe anajua weaknesses za yule mtu atazimwaga hapo weeee... mmhhh...
 
Yeah, tunahitaji kuelimika na kukomaa kifikra katika maswala haya ya mahusiano, Mi huwa naamini kutongoza ni haki ya kila mwanaume iwe kwa nia mbaya au nzuri, wewe ongea tu halafu mimi nitakujibu sawasa kwa upendo kabisa umekuja kwa nia ya nataka kuoa nakujibu in a way kwamba utatamani kumuona na kumtokea dada mwingine ingawa kwangu hukufanikiwa, umekuja na gia ya kuchakachua nitajitaidi kukupa jibu lakukufanya ujue hicho kwangu sio sahihi ingawa kuna watu wanaweza kuona ni sawa tu kwao. Mwisho wa siku najikuta idadi ya maadui inapungua, na mtu ana uhuru kwa nafsi yake.

Kumdharau mtu kwa vigezo vya pesa na uzuri na nini nini tena material thing ni ujinga kabisa. Na utoto kabisa, jali UTU. Hicho ni kitu cha msingi sana unamporomoshea mtu matusi kisa hakutaki au amekutaka what for?? Sipendi kiburi na misifa ya ajabu ajabu.
TUJALI SANA UTU JAMANI.
 
My Dear Lizzy,

Tena wapo wengi sana wa aina hiyo lakini nikwambie tu kitu kuwa "Hayo ni maneno ya mkosaji".

Inakuwa kama hadithi za sungura vile alivyoshindwa kufikia ndizi akasema sizitaki mbichi hizi.
 
Maneno
" . . . mi sio saiz yako" au "mi sio rika lako" au " au " hatuendani kabisa" ni lugha nyingine ya mtu kusema SIHITAJI LOLOTE KUTOKA KWAKO.
Na wakati mwingine hutumia kama njia ya kukupima kujiamini kwako kama upo tayari kukabiliana na changamoto mbalimbali ktk maisha???
So usiumize kichwa kwa kumtafutia jibu la kejeli au dharau badala yake mpe jibu la kuonyesha HOW WISE YOU ARE

Na pia kukutokea mambo kama haya usione kama ni mkosi fulani ktk maisha yako, bali ni kila mtu anakutana navyo. Jaribu kuona ni namna gani utaweza kupambana na watu wa aina hiyo lakin IN A WISE WAY

Nawakilisha
 
Ukishaona mtu anasema you are in my league au siendani na wewe... ujue ana inferiority complex au tu ni mshamba; kila mtu anaendana na kila mtu akiamua
 
Ukishaona mtu anasema you are in my league au siendani na wewe... ujue ana inferiority complex au tu ni mshamba; kila mtu anaendana na kila mtu akiamua

saa nyingine ndo yale yale ya 'kusubirishana'.....leo uko out of his/her league, kesho umo ndani.....
 
Yeah, tunahitaji kuelimika na kukomaa kifikra katika maswala haya ya mahusiano, Mi huwa naamini kutongoza ni haki ya kila mwanaume iwe kwa nia mbaya au nzuri, wewe ongea tu halafu mimi nitakujibu sawasa kwa upendo kabisa umekuja kwa nia ya nataka kuoa nakujibu in a way kwamba utatamani kumuona na kumtokea dada mwingine ingawa kwangu hukufanikiwa, umekuja na gia ya kuchakachua nitajitaidi kukupa jibu lakukufanya ujue hicho kwangu sio sahihi ingawa kuna watu wanaweza kuona ni sawa tu kwao. Mwisho wa siku najikuta idadi ya maadui inapungua, na mtu ana uhuru kwa nafsi yake.

Kumdharau mtu kwa vigezo vya pesa na uzuri na nini nini tena material thing ni ujinga kabisa. Na utoto kabisa, jali UTU. Hicho ni kitu cha msingi sana unamporomoshea mtu matusi kisa hakutaki au amekutaka what for?? Sipendi kiburi na misifa ya ajabu ajabu.
TUJALI SANA UTU JAMANI.
ni wachache sana wenye akili, uelewa na mawazo kama yako LD
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom