Our eternal ambassadors

Tusipinge vyote vilivyoelezwa na Adamu kama alivyosema Kafara,lamsingi ni kulifanyia kazi.Kaangalie baadhi ya watoto waliopo Foreign affairs ni watoto wa akina Lwaitara,Lowassa.Sio kama hawana sifa lahasha lakini uwepo wao pale unaweza sukumwa na nyazifa za wazazi wao.
Ni kweli kuna baadhi ya Balozi ni kama zimesahaulika.Niambie Balozi wa Tanzania nchini Japan anamiaka mingapi?Inaweza isifike 16 lakini miaka 6 nakwenda juu inafika na madhara yake ni kuwa anajenga uzoea.Na wapo wengine ambao hawajaguzwa na mabadiliko yoyote na wapo Ubalozini kwa muda mrefu.
Anaposema kuwa Watu wengi walikuwa wanakimbilia kufanya kazi Foreign Affairs ni kutokana na maslahi ikiwemo kwenda kusaidia Balozi fulani nchi fulani hizo ni miongoni na faida za kufanya kazi foleini.
Tunapoengelea Tanzania sasa hivi ukiwauliza watu wengi watakuambia wanataka kazi TRA,Wizara ya Fedha na BOT ambako kunavifaida vya kukaa huko.Hauwezi msikia mtu akasema nitaenda fanya kazi Liwale,Kasuru,Pangani,Kigoma,Rukwa kwani wanajua hali ya kimaendeleo sio safi.
Lamsingi hii ni challange kwetu kuweza tafuta evidence ya aliyoyaandika Adamu.
 
Dua,

Taking the beast by its horn with a totally toothless tired article?

As stated above, my beef is not with the subject matter but the way he squanders the subject by a cooloquially nonchalant delivery coupled with data free overgeneralizations.It is worse than hadithi za babu, clearly you cannot excuse that too.

Tunaposema kumkoma Nyani giladi inabidi kumkoma kuwe kumkoma kweli na sio a self defeating weak attempt which put anybody who is anti-establishment to shame.

Adam huwa anaweka e-mail kwenye hoja zake sasa kama wewe unaona ameongopa au anazusha weka ukweli hapa kwa sababu hata mimi nawafahamu wengi tu ambao wamekuwa nje ya nchi kwa miaka zaidi ya minne. Je, sheria ile ya wao kukaa miaka minne imefutwa? Kama imefutwa nani alifanya hivyo na kwa madhumuni gani? Vile vile ni ukweli usiopingika kwamba huko kwenye balozi zetu kumeoza sana kwa kuajiriana kundugu n.k.

Ukianza kuchunguza utaona hakuna hata chembe ya uongo kwenye hoja iliyotolewa. Sasa kwa kuanzia naona kuna haja ya kweka majina ya wanaofanya kazi kwenye balozi zetu zote hapa ili tuone ukweli wa mambo.

JF members walio Foreign waanze kutuwekea vitu hapa tukianzia kwenye ofisi zetu kubwa za USA, UK, n.k.
 
Adam huwa anaweka e-mail kwenye hoja zake sasa kama wewe unaona ameongopa au anazusha weka ukweli hapa kwa sababu hata mimi nawafahamu wengi tu ambao wamekuwa nje ya nchi kwa miaka zaidi ya minne. Je, sheria ile ya wao kukaa miaka minne imefutwa? Kama imefutwa nani alifanya hivyo na kwa madhumuni gani? Vile vile ni ukweli usiopingika kwamba huko kwenye balozi zetu kumeoza sana kwa kuajiriana kundugu n.k.

Ukianza kuchunguza utaona hakuna hata chembe ya uongo kwenye hoja iliyotolewa. Sasa kwa kuanzia naona kuna haja ya kweka majina ya wanaofanya kazi kwenye balozi zetu zote hapa ili tuone ukweli wa mambo.

JF members walio Foreign waanze kutuwekea vitu hapa tukianzia kwenye ofisi zetu kubwa za USA, UK, n.k.

Dua,

1. Upendeleo haupo tu foregn na ajira za vimemo ni endemic serikalini na institutions zake!

2. Waliopo foreign waweke basi majina ya wafanyakazi walioajiriwa kwa utata- yaani not based on qualifications, influence za wazazi n.k
 
Kafara

Kama unaweza hebu weka miaka waliyokuwa posted London au nje ya nchi kama unayo.

Mzalendohalisi

Issue ni ile ambayo Adam Lusekelo alianzisha. Kama kumbukumbu zangu ni sahihi tuliongelea swala la TRA kwa kuwa huko kuna rushwa kubwa ndio maana ya mjadala. Vilevile pesa ya VISA hasa UK na USA inachangia sana katika mfuko wa bajeti bongo na kuna ubadhirifu wa kununua Jengo la ubalozi wa Tanzania UK ambapo swala hilo lilijadiliwa hapa. Naomba Invisible airudishe ile topic ili tuone iliishaje. Unapokaa mahali pamoja muda mrefu unaficha uvundo mwingi.
 
Lusekelo kachemsha kwa sababu ndogo tu.

Not necesarily kwa sababu msingi wa article yake ni mbovu,premises zake inawezekana ni superb.

Ni kwa sababu hajatoa data.No data no right to speak full stop.Yeye kama muandishi alitakiwa atuinform kwa kutupa data na sisi tumkome nyani.Sasa anataka kuwapa point watu wanaosema kuwa kuna majungu against watu kwa sababu article isiyo data inaonekana imekaa kimajungu majungu.Tupe names and figure kama unataka ku convince.Otherwise hata point ya kuanzia inakuwa ngumu na article inakuwa haina contribution na kwa kweli mchango wake unakuwa sifuri.


It is not the issues that I am disputing, for without data how can one dispute the isues? It is this low level of professionalism that I am protesting.
 
In short Adam alitakiwa kuwa muwazi kama ambavyo amekuwa akifanya in most cases na sio kuleta confusions.........................na hata JF kuna wakati tukampa credit ya kwamba yeye ni mserikali asiyeogopa kusema kwa uwazi na ukweli.................not in that article
 
Kwenye balozi zetu kuna maofisa usalama,waambata wa kijeshi,na wahasibu.

mabalozi peke yao ndiyo wanaobakishwa vituoni kwa muda mrefu. wa kulaumiwa hapo ni Raisi kwasababu ndiye aliyewateua.

wale wote walioko chini ya mamlaka ya Katibu Mkuu wa Wizara mara nyingi hurudhishwa nyumbani baada ya miaka 4/5.

kwa uelewa wangu hili suala la watu kukaa nje muda mrefu, au kusota wizarani muda mrefu lilikuwepo wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi.Malalamiko hayo yamepungua tangu Mkapa alipoingia Ikulu na Kikwete mambo ya nje. Sehemu ya kwanza ambayo Mkapa aliinyoosha ilikuwa wizara ya mambo ya nje.

Vilevile mtumishi akishakuwa balozi na kama umri wake wa kustaafu haijatimia basi Raisi analazimika kumhamisha kituo au kumuacha hapo alipo. Raisi akilazimika kumrudisha wizarani basi lazima ampe Ukuu wa Idara au "KAZI MAALUM."


Kikwete alipoingia Ikulu alitoa agizo kwamba Mabalozi wa-serve vipindi viwili na baada ya hapo warudi nyumbani.

Pundit,
Uingereza,Canada,USA,UAE,Oman,Kenya,Saudia,Zimbabwe,UN-Geneva, India,DRC, kote kuna Mabalozi wapya. hata makao makuu kuna mabalozi kama wanne wameteuliwa. sidhani kama Lusekelo ana hoja ktk suala hili.
 
binafsi sina ndugu wala Jamaa ktk Foreign yoyote, ila nauliza kuna kazi kama za kufagia,kupiga deki, like office Boy..hii inahitaji mtu wa Nje? au Local? kama Local kuna tatizo gani balozi akamchukua mtoto wa Mjomba kufanya nae kazi? Kama kazi za proffessional basi muhim ikatangazwa au kukawepo taratibu maalum zitakazofanya watu wengine ndani ya NCHI wanaFAIDI keki ya UHURU..
 
binafsi sina ndugu wala Jamaa ktk Foreign yoyote, ila nauliza kuna kazi kama za kufagia,kupiga deki, like office Boy..hii inahitaji mtu wa Nje? au Local? kama Local kuna tatizo gani balozi akamchukua mtoto wa Mjomba kufanya nae kazi? Kama kazi za proffessional basi muhim ikatangazwa au kukawepo taratibu maalum zitakazofanya watu wengine ndani ya NCHI wanaFAIDI keki ya UHURU..

Kwanini awe mtoto wa mjomba wake na asiwe mtoto wa mjomba wa mwambata wa uhamiaji? Unapoanza kuvunja kanuni ndogondogo ni rahisi kuvunja kanuni kubwa. Je tarishi wa TRA au Ikulu lazima awe ndugu wa mtu anayefanya kazi Ikulu? Kama wanaweza kujaza nafasi za utarishi na ndugu zao ni kitu gani kitafanya iwe vigumu wao kuajiri ndugu zao kwenye nafasi za juu?
 
..by the way yuko Balozi.Maj.General Martin Mwakalindile. Nina imani ame-serve zaidi ya miaka 10. Huyu alikuwa Chief of Staff mara baada ya vita vya Kagera. Kama hajastaafu jeshi basi inakuwa vigumu sana kumrudisha nyumbani.
 
mara nyingi nafasi za "local staff" ubalozini huwa hazitangazwi. sasa kwa vile wanaojua kwamba nafasi kama hiyo ipo ni wafanyakazi wa ubalozi ni rahisi kwao kuvuta ndugu au jamaa yao ambaye yupo available. hii haimaanishi ni vizuri kufanya hivyo bali ndo hali ilivyo (inabidi niongezee kwamba inawezekana kabisa katika nchi husika wapo watz wengine ambao wangeweza kufanya hizo kazi. sasa hapo ndio kwenye shida. kwa nini hao wengine hawapewi? mimi sina jibu)

makala ya lusekelo imegusa kipindi kirefu sana yaani toka enzi alipokuwa chuoni mpaka sasa hivyo ni vigumu sana kuchangia bila kupotoka.

sidhani kama mkapa alibadili mabalozi aliowakuta. hivyo ukiacha wale waliostaafu mabalozi wengine wamekaa nje kwa zaidi ya miaka kumi (kipindi cha mkapa). sasa sidhani hapa wizara ni ya kulaumiwa.
 
binafsi sina ndugu wala Jamaa ktk Foreign yoyote, ila nauliza kuna kazi kama za kufagia,kupiga deki, like office Boy..hii inahitaji mtu wa Nje? au Local? kama Local kuna tatizo gani balozi akamchukua mtoto wa Mjomba kufanya nae kazi? Kama kazi za proffessional basi muhim ikatangazwa au kukawepo taratibu maalum zitakazofanya watu wengine ndani ya NCHI wanaFAIDI keki ya UHURU..

nadhani hapo ndio kwenye tatizo. kwa nini kufanya kazi ubalozini iwe "kufaidi keki ya uhuru" na sio sehemu ya kujenga nchi? mtu wa wizara ya nje kuhamishiwa ubalozini ni sawa na mfanyakazi mwengine wa wizara kuhamishwa kutoka makao makuu kwenda mikoani tofauti ni wa mambo ya nje anakwenda nje ya nchi.
 
1.
There is no need for guys to own our foreign missions. It is almost scandalous now. Our diplomatists have made foreign missions their homes. How do you stay at a place for 16 years? 'Eti ambassadors'? It is next to impossible. But it happens in Bongo.

So far kuna balozi mmoja tu anayeitwa Mtango, ambaye amekuwa huko kwa muda mrefu, anyeweza kujibu hilo swali ni rais peke yake, maana ni presidential political appointment, foreign hahihusiki kabisaa, unless kama Adam ambaye ninamuheshimu ana kwa kumkoma nyani sku zote, kuna something anataka kusema lakini anashindwa, kwa sababu balozi kuwepo muda mrefu mahlai pamoja nia la rais sio la wananchi walioko foreign!

2.
Okay. I know diplomatic missions have been used as a way to dump embarrassing relatives, friends and chicks; but it should be for four years only. Why should they be there for decades?
Because once there, the 'diplomats' also start building empires. The husband will employ his wife. Then he will also employ his children and 'shemejis'. I have seen it happen.

Ninafahamu only one case na ilikuwa wakati wa awamu ya kwanza kule DC, balozi wetu kule Bomani, ndiye aliyeajiri watoto na ndugu zake pale, je wapo mpaka leo hapana walishaondolewa wote, kwa hiyo unless kuna dataz au concrete evidence kuhusu balozi aliyewahi kuajiri mke wak na shemeji zake, basi asemwe specifically ni nani apewe mawe, lakini kuwa-generalize mabalozi wote kuwa ni tabia yao sio kuwatendea haki mabalozi wetu ambao wengi ni wachapa kazi hasa na waliousotea ubalozi wao!

3.
It becomes so nauseating that you tend to avoid Tanzanian embassies once you get there. First, most embassy employees think you want to ask for money. Outrageous! Then the relatives of the 'ambassador' look at you with an uncalled for hauteur. You decide that this is bullshit and leave. As I said embassies are places for friends, embarrassing buddies, girlfriends and other unqualified guys. I think we should be told if the guys are the permanent rulers of these areas.

Mkuu Adam hapa pia anakuwa sio mkweli au haelewi kinachoendelea kwenye balozi zetu, kwanza ni tabia ya wananchi wengi kwenda ubalozini na matatizo yasiyotatulika na ofisi, binafsi nimeishi nje na nimejionea hili kwa sababu nimewasaidia wananchi wengi sana waliokwama wakaenda ubalozini kuomba msaaada ambao kisheria haupo, naomba kurudia tena kwenye hili kuwa wabongo wengi tuna tabia za kwenda ubalozini kuomba misaaada ambayo kisheria balozi zetu haziwezi kushiriki, ni mara nyingi nimewasaidia wabongo wengi sana mahala pa kulala kwa sababu ubalozi hauwezi kukupa mahali pa kulala,

Pia tena ni kweli kuwa wabongo tuna tabia ya kwenda ubalozini kuomba hela kwa sababu mbali mbali, ukweli ni kwamba ubalozini hakuna fungu la hela ambalo limetolewa na serikali kwa ajili ya wananchi watakao tokea wakizihitaji, nimemuona mpaka Mtikila mwenyewe one time amekwama hana nauli ya kurudi bongo anataka ubalozi umkopehse na ndipo alipoanza kuwa agent wa ccm maana walimlipia hiyo nauli, na kuna mama mmoja aliyempa hela za matumizi akaahidi kurudisha mpaka leo hajarudisha sasa unategemea next time huyu mama akumuona mbongo ana shida ya hela afanye nini? sasa swali ni je alikwendaje huko in the first place? Ni tabia yetu saa wabongo kwenda ubalozini kuomba hela, I have seeen it na mpaka leo bado hii tabia inaendelea, ni suala la kuwa wakweli tu au kuema ukweli iwapo hatujui, lakini binafsi nimewasaidia wananchi wengi sana wenye hizi shida na wasiokuwa na shukrani!

Balozi zetu siku za nyuma zilikuwa zinaajiri foreigners tu, na sio wabongo, hasa wafilipino, nilifikiri tutawapa heshima kina Balozi Daraja, Mahiga, Kibelloh na wengineo kwa kujaribu kuiondoa tabia hii, sasa badala yake eti wameajiri ndugu zao? Adam kwenye hii article anakosa ushahidi wa kuthibitisha haya, mabalzoi wengi wa siku hizi wanajaribu kuiondoa hii tabia na kuna mabalozi yetu mengi ya kuonyesha mfano, DC wakati fulani ilikuwa wafilipino watupu, Belgium ilikuwa wahindi na warundi, we can go on and on, ninawapongeza mabalozi ambao wameamua kuwaondoa wa-Filipino kwenye balozi zetu na kuajiri wabongo,


Foreign ni wizara ninayoiheshimu sana kwa kuwa na wasomi wakubwa sana katika taifa letu, wengi wao wanaheshimika sana kwenye mataifa kwa kuwa na vichwa, kama kawaida kweny kila sekta kuna wazim na wasiojiweza, lakini sijawahi kuona wananchi wenye vichwa vikali kma wananchi wengi wa foreign, wengi wao wanatoka kenye very humble families na wanashukur sana Mungu kuweza kupata nafsi ya kufanya kazi foreign, somebody has to be a diplomat wananchi wote hatuwezi kuwa, somebody has to be a president, priviledges zinafutana na kuwa na hizo nafasi zisitufanye tukwachukia waliobahatika kuwa nazo, which seeems to the case na hii article ya Adam, ambaye siku zote nina heshima naye sana isipokuwa sielewi kilichomtokea kwenye hili, ila nitamtafuta nimuulize kulikoni kuwatukana wananchi wengi wasiouwa na makosa kabisa huko foreign na balozi zetu?

4.
I think that the government is ruled by a king anyway. Too much power on the presidency and we will have to deliberate about it.

Now this ni another ishu kabisaa, ambayo haihusiani kabisa na foreign, hii ni ishu by itself inayohitaji kufunguliwa topic yake.

Ahsante Wakuu!
 
Pia tena ni kweli kuwa wabongo tuna tabia ya kwenda ubalozini kuomba hela kwa sababu mbali mbali, ukweli ni kwamba ubalozini hakuna fungu la hela ambalo limetolewa na serikali kwa ajili ya wananchi watakao tokea wakizihitaji, nimemuona mpaka Mtikila mwenyewe one time amekwama hana nauli ya kurudi bongo anataka ubalozi umkopehse na ndipo alipoanza kuwa agent wa ccm maana walimlipia hiyo nauli, na kuna mama mmoja aliyempa hela za matumizi akaahidi kurudisha mpaka leo hajarudisha sasa unategemea next time huyu mama akumuona mbongo ana shida ya hela afanye nini? sasa swali ni je alikwendaje huko in the first place? Ni tabia yetu saa wabongo kwenda ubalozini kuomba hela, I have seeen it na mpaka leo bado hii tabia inaendelea, ni suala la kuwa wakweli tu au kuema ukweli iwapo hatujui, lakini binafsi nimewasaidia wananchi wengi sana wenye hizi shida na wasiokuwa na shukrani!

Swala la nauli ya kurudi bongo ni swala la serikali kwa wale ambao hawana nauli ya kuwarudisha ndio sababu unapoomba passport kuna mahali unajaza wadhamini ili ukikwama nje waweze kulipa gharama ambayo serikali itakulipia. Kuna mifano mingi sana kwa hili, hata wale wanafunzi ambao serikali ilishindwa kuwalipia karo kule Ukraine walilipiwa one way ticket kurudi nyumbani. Wanaporudi hati zao zinazuiwa hadi walipe deni, bali sema system yetu kwa sababu ni mbovu na ufuatiliaji ni mbaya lakini hilo ni jukumu la serikali kwa raia wake.

Swala la wafanyakazi kutoa pesa mifukoni mwao hilo ni tatizo lao wenyewe kwa nini hawafuati sheria? Wana CCM kwa nini wanapokwenda nje husaidiwa na balozi zetu au kwa sababu wao wako madarakani? Mifano ipo mingi hebu niambie kwa nini balozi zetu zinatumiwa kama extension ya CCM? Lazima balozi zetu ziwahudumie WTZ wote bila kujali ni wa chama gani? Tunashuhudia jinsi London ilivyo centre hivi sasa kwa Viongozi wa CCM kuitumia vibaya kwa maslahi ya chama badala ya Utanzania. Hata wanapokuja kwa shughuli za kichama au binafsi wanatumia maafisa wa ubalozini kwa maslahi binafsi WHY? Iwe ku-book hoteli au kupiga simu hizi ni gharama ambazo walipa kodi wanalipa, Je, ni kwa wana CCM tu?
 
Huko Foreign kumejaa uvundo kama unakumbuka

1. Diria kusachiwa na wajerumani.

2. Pesa kupotea Malawi na baadaye kuhamishwa afisa kwenda Zambia.

3. Mtanzania aliyeiba Chuo kikuu Zimbabwe na serikali kutumia wadhifa wake na watu wake wa karibu ili kuona Mtanzania huyo anaachiwa wakati alifanya kosa la Wizi. Tanzania alitumia balozi wake aliyekuwa Zambia wakati huo kusafiri mara kadhaa kwa ajili hiyo. (Sir G. Kahama analifahamu hili.)

4. Mahalu na wizi wa Nyumba Italy ambapo kesi inaendelea......................

5. Ubalozi UK kununua nyumba kwa Mizengwe

6. ................................................

7. ...................................................

Sasa kuna mengi hayasemwi ni wakati wa kusafisha huko foreign. Watanzania wengi wako jela za nje lakini kwa sababu hawamfahamu nobody kwenye system hawapewi msaada wowote, Je, tutafanya mambo yetu kishkaji hadi lini?
 
Field Marshal ES said:
So far kuna balozi mmoja tu anayeitwa Mtango, ambaye amekuwa huko kwa muda mrefu, anyeweza kujibu hilo swali ni rais peke yake, maana ni presidential political appointment, foreign hahihusiki kabisaa,

..Balozi Elly Mtango alikuwa balozi Geneva, halafu akarudishwa nyumbani na Mzee Mwinyi kuwa PS wizara ya habari. Mzee Mkapa akamteua kuwa PS Mambo ya Nje. Baada ya hapo akateuliwa tena kuwa Balozi Japan.

..Balozi Hassani Kibelloh ndiye aliyempokea Elly Mtango U-PS pale Mambo ya Nje. Wakati Mtango anakwenda Japan, Raisi Mkapa alimteua Dr.Ben Moses na Charles Sanga kuwa Ubalozi.Siyo kweli kwamba Balozi Mtango amekaa Japani miaka 16!

..Mabalozi waliokaa nje muda mrefu ni wa aina ya Gen.Sarakikya, Lt.Gen.Mwakalindile na Lt.Gen.Silas Mayunga "mti mkavu." Hawa ukiwarudisha nyumbani bila kuwastaafisha Jeshi watawasumbua watu kama Waitara,Mwamunyange,na Shimbo.

..Mabalozi wanabadilika siku hizi. Mkapa alipoingia madarakani aliteua Mabalozi kama watano kama wakuu wa idara wizarani. Kituo kama Harare wali-serve Muganda na baadaye Mbita. UN alimbadilisha Mwakawago na Mahiga. India alikwenda Capt.Kiwanuka, halafu baadaye Mama Nzaro. London alipelekwa Prof.Abdul-Kadiri badala ya Col.Mchumo. Hata itifaki alianza na Mwawado, akaja Opanga, akamaliza na Cisco Mtiro.

..Hiyo ni mifano michache tu...Lusekelo amekosea kuzungumzia kiujumla-jumla, bila data, suala kama hili.
 
1. Swala la nauli ya kurudi bongo ni swala la serikali kwa wale ambao hawana nauli ya kuwarudisha ndio sababu unapoomba passport kuna mahali unajaza wadhamini ili ukikwama nje waweze kulipa gharama ambayo serikali itakulipia.

Serikali haiwezi kuwa na hela za kuwalipia wananchi wasiokuwa na nauli huko Ulaya, bila ya sababu za msingi, kuna wanao-qualify lakini binafsi sijawahi kuwaona, nilikuwa ninaona wananchi wenye sababu za kushangaza kweli kuhusiana na kutokuwa na nauli, na kama ni ishu basi ipelekwe bungeni kuwe na fungu maalum kwenye bajeti ya foreign, lakini makosa yasisukumiziwe wananchi wa ubalozi maana hawahusiki ni lazima wawe na sheria ya kuweza kumlipia mwanachi nauli pale tu sheria inaokuwa satisfied!

2.
Swala la wafanyakazi kutoa pesa mifukoni mwao hilo ni tatizo lao wenyewe kwa nini hawafuati sheria?

Kwa sababu kisheria hawa wananchi hawawezi kulipiwa na serikali, basi wanachi kama mimi tulikuwa tunawasaidia, na siku zote huwa ni kuleta kujiletea kilio, lakini watu huwasaidia anyways!

3.
Wana CCM kwa nini wanapokwenda nje husaidiwa na balozi zetu au kwa sababu wao wako madarakani? Mifano ipo mingi hebu niambie kwa nini balozi zetu zinatumiwa kama extension ya CCM? Lazima balozi zetu ziwahudumie WTZ wote bila kujali ni wa chama gani? Tunashuhudia jinsi London ilivyo centre hivi sasa kwa Viongozi wa CCM kuitumia vibaya kwa maslahi ya chama badala ya Utanzania. Hata wanapokuja kwa shughuli za kichama au binafsi wanatumia maafisa wa ubalozini kwa maslahi binafsi WHY? Iwe ku-book hoteli au kupiga simu hizi ni gharama ambazo walipa kodi wanalipa, Je, ni kwa wana CCM tu?

Wanachama na viongozi wa pande zote mbili bongo husaidiwa sawa sawa na balozi zetu, CCM ni chama tawala na siku zote huwa wako very fast ku-respond iwapo kuna mtu wao amekwama, na most of the time huwa wanamdhamini na kuzirudisha mara moja kwa ubalozi mtu wao akisaidiwa, ingawa pia kunaweza kuwa na some abusiveness cases, hiyo ni kawaida kila sekta ya serikali hata private,

matatizo ya foreign yapo kila sekta ya serikali, in fact mafisadi wote hakuna wa kutoka foreign!
 
I used to be a regular on Adam's column "With a light touch" in late 70s up to late 80s; other popular columnists of the time included Freddy Macha with his "Cultural Images" and Agoro Anduru with his "A Short Story with Agoro Anduru." I understood Adam as a person who identifies problems in the system and generically writes about them to raise public awareness. In his writing he uses a vulgar language without providing specifics of his subject. Despite this lack of specifics, readres would easily get the message. I took this as a writing syle and I had no problem with it. I guess this sytle may have its roots in Professor Penina Mrama's Drama Group to which Lusekelo was a member.

The article copied above still reflects his "trade mark" writing style, and I clearly get his message: there is no time limit for our diplomats. Their tenure in a foreign country depends on the boss at the Ministry and at State House.
All I see as Lusekelo's mistake is in his choice of the journal. Such article should have appeared in a regular newspaper instead of this investigative newspaper.
 
Back
Top Bottom