Osama bin Laden killed!

Status
Not open for further replies.
Dunia ni kijiji utafanya vyote ila iko siku utapatikana. tunakumbuka mpagowake mzima wa kupiga Ubalozi wetu Dar-es-salaam na kuua zaidi ya watu 200. licha ya machafuko yote ya ugaidi apa duniani ndiye mzamini mkuu.
kapumzike salama Osama uliyo yafanya yanatosha
 
hata mimi najiuliza, inawezekana Osama alishakufa kitambo kwa ugonjwa wake, au kafa kifo cha kawaida. lakini kwa kuwa Marekani sasa inatafuta namna ya kuondoka Afghanistan gracefully, kwa sababu ni dhahiri ile vita imegeuka kuwa liability kwao !. ukizingatia Taliban wametangaza kuspeed up mashambulizi, hawa jamaa wanaweza kustage up hii kitu ili waondoke Afghanistan peacefully!.
Kwa aina yoyote ya kifo ambacho atakuwa kafa, au kwa muda wowote (wa kuuawa)whether ni siku za nyuma au leo au jana, bado hii ni News inayokuwa broken kwa mara ya kwanza leo na US, LAKINI kubwa zaidi ni kwamba America ndio wanaumiliki mwili wake kwa muda huu!!.. Hivyo dunia ikae mkao wa alert, maana iam afraid wafuasi wake wanaweza kufanya chochote kuonyesha kuwa hata kama jamaa amefariki, kundi la Alqaeda bado lipo!...So check-out!..Wanaweza kuzaliwa Osamas 50 zaidi.
 
Saa nzima na ushee imeshakatika tangu ilipotangazwa Obama atazungumzia kuhusu National Security 10.30pm ET sijui kuna details zipi zinazomchelewesha kutokea pale East Room, labda anasubiri umati uongezeke. Maana kuna kundi kubwa la watu waliojawa na furaha tele wakiimba USA USA USA. Hii hotuba ya Obama usiku huu lazima itatumika katika kampeni za 2012.
 
Sasa hapo Obama kwa nini apewe credit? Yeye ndo alihatarisha maisha yake kumuwinda Osama huko Islamabad?

Siasa saa ingine bana.....kazi afanye mwingine ujiko achukue mwingine. So Very unfair!!!!

Unfortunately siasa iko hivyo
 
..........kwishney habari yake, kama kauliwa atakuwa kauzwa na walinzi wake.
 
Sasa hapo Obama kwa nini apewe credit? Yeye ndo alihatarisha maisha yake kumuwinda Osama huko Islamabad?

Siasa saa ingine bana.....kazi afanye mwingine ujiko achukue mwingine. So Very unfair!!!!
Mwalimu alipopewa credit ya kumwondoa nduli Idi Amin naye alienda frontlines kupigana?Mbona haya ni mambo ya kawaida sana tu.Credit anapewa kwasababu wakati wanafanya move zote huwa wana mbrief na hiyo ni daily,halafu yeye huwa ndo anatoa a go ahead in any mission FYI.Kabla ya kumwua,if kulikuwa na family members lazima aliulizwa kuhus a goa ahead,Obama anatangaza hapa sasa hivi kuwa an opearation has been successful.
 
Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa, bina laden kauawa! Rais Obama wa Marekani ametangaza rasmi kuwa jamaa kauwa. Angalia breaking news za Aljazeera, BBC, CNN, Skynews, mtaipata. Mwili wa bin laden upo mikononi mwa USA.
 
Obama anasema alikuwa briefed about the intelligence last week,leo akatoa a go ahead ya shambulizi,amesema kulikuwa na fire fight,hatahivyo wamarekani walishinda na wakamwua Bin Laden na wanao mwili wake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom