Ortello Business ya Loliondo yaanzisha kampuni ya simu bila leseni!

Mbembeaji

New Member
Dec 3, 2009
3
1
Jamaa huyu wa Falme za Kiarabu ameigeuza Loliondo kuwa sehemu ya nchi yake. Naamini kuwa hii ni kukiuka Ibara ya 28 ya Katiba ya nchi yetu kuhusu ukamilifu na umiliki wa nchi yetu. Je si kosa la uhaini kuitoa nchi yetu kwa watu wengine?


TCRA kumbana mwekezaji Loliondo

Imeandikwa na Maulid Ahmed; Tarehe: 2nd December 2009 @ 22:00 Imesomwa na watu: 280; Jumla ya maoni: 0
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imebaini kuwa kampuni ya simu za mkononi yenye makao yake katika Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE), inaendesha shughuli zake za kutoa huduma ya mawasiliano ya simu bila leseni.

Kwa mujibu wa TCRA, kampuni hiyo inatoa huduma hiyo katika eneo la uwindaji liliopo Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Profesa John Nkoma, amekataa kutaja jina la kampuni hiyo ya simu.

Kwa mujibu wa Profesa Nkoma, wataalamu wa TCRA wamebaini hilo baada ya kwenda kwenye eneo hilo kuchunguza.

Eneo hilo lipo chini ya kampuni ya uwindaji ya Otterlo Business Corporation Limited (OBC) inayodaiwa kumilikiwa na mwanajeshi wa cheo cha juu kutoka familia ya kifalme,UAE.

OBC ilipewa eneo hilo mwaka 1992 na tangu wakati huo imekuwa ikiongezewa muda kila baada ya miaka mitano.

Bunge limeiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kutoa upya vitalu vya uwindaji ifikapo mwaka 2011 kwa kufuata taratibu mpya.

Wananchi wa eneo hilo wamewahi kulalamika kuwa wanapoingia kwenye eneo hilo simu zao zinabadilika na kuonyesha wanaingia eneo la Uarabuni.

Kwa mujibu wa madai hayo, simu zinakuwa chini ya kampuni ya Etisalat na wanatozwa fedha nyingi wanapopiga simu.

Mkurugenzi Mtendaji wa OBS, Isaack Mollel, aliwahi kukaririwa akisema kuwa, eneo hilo lipo chini ya Etisalat kwa sababu familia ya kifalme ya UAE inahitaji mawasiliano ya uhakika inapotembelea eneo hilo.

Mollel alisema, kwa kuwa Etisalat ni mwanahisa mkuu katika kampuni ya Zantel, hakuna haja ya kuomba leseni TCRA.
Chanzo: HabariLeo
 
Huu ni upumbavu hapa JF watu wameeleza haya miezi sas leo TCRA ndo wanajifanya wamegutuka? Huu ni ujinga kama mnakula rushwa si mseme? Prof. Nkoma wewe una deals zako na hao waarabu lakini ujue kuwa siku zako zinahesabika.
 
usalama wa Taifa wako wapi? mpaka mtu anajiwekea mawasiliano yake tena ya satellite yaani yanayoruhusu international calls mbaya zaidi bila regulation ya authority zetu. Suala hili limesemwa hapa karibu mwaka sasa. Hii nchi tumshukuru Mungu tu, tungekuwa tushavamiwa siku nyingi. Ila mali asili wanajichukulia kama zao.
 
usalama wa Taifa wako wapi? mpaka mtu anajiwekea mawasiliano yake tena ya satellite yaani yanayoruhusu international calls mbaya zaidi bila regulation ya authority zetu. Suala hili limesemwa hapa karibu mwaka sasa. Hii nchi tumshukuru Mungu tu, tungekuwa tushavamiwa siku nyingi. Ila mali asili wanajichukulia kama zao.
kwani nchi hii ina usalama wa taifa tena?!
 
Back
Top Bottom