Orodha Ya Wabunge/Mawaziri walioshindwa Kutekeleza Ahadi na Ulegevu wao Majimboni

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Ikiwa imebakia takribani miaka mitatu kujichukulia kilicho chao , wapo wabunge wengi waliojifanya kushindana na mkuu wa kaya kwa kutaja orodha ndefu na ahadi hewa/feki , mpaka leo hawajazitekeleza majimboni mwao na hawana habari nazo tena.
Ninayo kumbukumbu kidogo ya wabunge wa Dar na mikoani kidogo

1. Hassani Zungu MB Ilala, huyu kachemka kabisa, Machinga Complex imemshinda, DDC K/Koo hapo ndio kaharibu kabisa, kuna rushwa za ajabu, wenye nchi wanafukuzwa wakuja wachina na wasomali ndio wamechukua fremu za maduka kwa bei ghali.

2. Idd Azan MB: wa Kinondoni, huyu anakatisha tamaa kabisa eneo lake ndio uti wa ngongo wa madawa ya kulevya, uchangudoa. na Jimbo lake linaongoza kwa rushwa, wahamiaji haramu wa kikongo na Rwanda Brundi. Wamewafanya vijana kuiga tabia mbaya ya kuendekeza pombe na kuomba omba.

3. Mbunge wa Kisawe huyu wageni wawekezaji ndio wamejificha huko wakijitwalia maekali eti wanawekeza na ndio jimbo la kwanza kuwa na umaskini.

4. Mbunge Kagasheki wa BK Mjini, huyu kalewa sifa kasahau kwao, Manispaa inanuka kwa uchafu , pake standi utadhani sio mji wa bukoba ulisifika kwa usafi enzi za Ruangisa.

5. Mbunge wa Mleba Kasikazini Prof. Tiba, huyu ndio kajisahau kabisa, kaenda kupambana na matajiri wa jiji kurudisha viwanja wazi kumbe kapambana naserikali yenyewe sasa kanyamazishwa, nae kafanya shule ya watoto yatima kuwa ya matajiri naye kuna kiporo.

6. Mbunge Edward Lowasa, huyu atasemi mengi sana maana mengi yashasemwa, kawafanya wamasai watoke shambani wakimbilie mjini kutafuta ajira wakati hawana shule, yeye angali kutoa mamillion kwenye makanisa huku kwao mifugo ikifa kwa kukosa maji, mpaka mkuu kariona kaenda kupoza, eti anataka urais!!

7. Mbunge wa Dodoma Rusinde, umeshindwa kufanya ushawishi kuufanya dodoma liwe jiji ili uwarudishe omba omba wote wanaoteseka pale faya na bibi titi ukafuata nyayo za Malecela!!

8. Halima Mdee, wewe bado una kiporo cha kunyamazia watu wanaonyanyasika na ardhi yao.

9. Andrew Chenge, wewe wananchi wanakaribia kukusahau kabisa utelekeza miradi mingi sana , shule za bariadi zianfelisha sana

Wengine waongezee tupate orodha ndefu
 
umemsahau mbunge wa TEMEKE, kashindwa kupigania haki bungeni kuhusu wageni wahamiaji waliojaa kwenye magodauni keko,sokota,tazara hawa wanatengeneza vitu ni bala,bado bunduki wataaza kutengeneza
 
na huyu pia msimsahau Dr. Mahenge wa makete. Yeye ameshndwa kusaidia wananchi wa kijiji cha uwanji kupata makazi mapya baada ya wakazi hao kuwapisha tanapa ktk hifadhi ya kitulo.

Km 62 kufika mjn lakn mpaka leo usafiri ni wa rand lover..
Idadi ya magonjwa na umaskini vinapanda kwa kasi....

Maji yanayotumika ktk shughuli zote ni ya mferejini (sehem kubwa ya makete)......
Ongezeko kubwa la watoto yatima wanaokosa msaada kabisa kutoka kwake akiwa kama muwakilishi.....
Ukosefu wa madawati na ubora wa madarasa ktk shule....

........MAFANIKIO....
Amejenga vilabu vya pombe za kienyeji vi4 .
Amesaidia kupunguza mauaji ya kishirikina.
Amejenga kisima ki1 kilichozinduliwa na nb w wa tamisemi..

......WASIFU WAKE......
Ni mbunge asiyependa kuwabughuzi mawaziri kwa maswali.....
Hajawai kulala bungeni ni mkarimu na si muongeaji....
Ye yupo tayali kama posho zikiendelea sawa kama zikistopishwa poa napo....

Ningeendelea wino umeniishia.....
 
We lijamaa usimchambue kwa kuchekesha hivyo mbunge wako. Kweli kijiji cha Kikondo- Uwanji hawajatendewa vema. Huyu jamaa ni neutral sana na ni shetani mwenye nafuu kuliko TUNTEMEKE na KITINE.
 
Asumpta mshana wa nkenge!huyu sijui anajua anachokifanya au hakijui!make tangu achaguliwe mimi sielewi kafanya nini?kiporo chako kipo na nina uhakika hauwezi kurudi 2015!
 
Mbunge wa Bukoba vijijini,kashindwa kusaidia wananchi wake wanaolipia umeme na kukaa Miezi 9 wakisubiri LUKU
 
We lijamaa usimchambue kwa kuchekesha hivyo mbunge wako. Kweli kijiji cha Kikondo- Uwanji hawajatendewa vema. Huyu jamaa ni neutral sana na ni shetani mwenye nafuu kuliko TUNTEMEKE na KITINE.

ujue mwana huyu jamaa anajivunia uwicha !
Pesa wanazohonga zilikuwa zinatosha kabisa kwa maendeleo !
 
tunapolalamikia hao wabunge wetu kwani wakati wanaomba kura hatukujua kuwa watatusaliti? mkuu wakaya (JMK....t.e) je ahadi zake zinatekelezeka ? tuelimishane jinsi ya kuwapata viongozi wetu sio kupewa pilau na kofia na kutupa kura zetu choooni
A%20S%20465.gif
 
Kwa nini Lowasa/Andrew Chenge/Lusinde wasiige mfano wa Rais Mtarajiwa Dr. Slaa jimboni mwake hata akaweza kusimamia Hospitali ya CCBRT ikaweza kuwasaidia wa-tz kupona midomo-sungura na kistra kwa wakina mama, Chenge kazi kupeleka nguo ulaya kwa DHL kufua wakati Bariadi visima vimeharibika vibaya
 
Ninyi wachangiaji ina maana wabunge wenu wanafanya mazuri? yatoe nayo basi wengine waige
 
Dah!Huku Tabora mjini sijui nisemaje aisee!Maana naona mbunge wetu amekuwa anaiwakilisha Simba SC bungeni!Rage hebu rudi huku jamani mpaka leo kero ya maji na kudolola elimu huoni???
 
`Jimbo la chalinze kuna mbunge anaitwa Said Bwanamdogo kweli yeye bado Bwanamdogo hajui aanzie wapi analala tu bungeni na kisha kukusanya posho yake 330,000/= kwa siku lakini hakuna afanyalo. Wakwere kwisha kazi
 
Yupo mtu anaitwa John Z.Chiligati wa Manyoni Mashariki,yaani huyu jamaa hajijui wala kujitambua
kuwa ni Mbunge,anavyojijua yeye ni kiongozi wa CCM basi.

Na hivi aliingia kwa kuchakachua Khuu!! Bora jimbo lisingekuwa na mbunge wana Manyoni mashariki wangejua moja.
 
Yupo mtu anaitwa John Z.Chiligati wa Manyoni Mashariki,yaani huyu jamaa hajijui wala kujitambua
kuwa ni Mbunge,anavyojijua yeye ni kiongozi wa CCM basi.Na hivi aliingia kwa kuchakachua Khuu!!
Bora jimbo lisingekuwa na mbunge wana Manyoni mashariki wangejua moja.

"Mfungwa hachagui gereza"
Mbona mnataja wabunge wa mijini tu? Wale wa majimbo masikini na yasiyo maarufu mbona hamsemi????
 
Back
Top Bottom