Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015

nadhani hapa panchanganya kidogo, rais kutoa amri wakati wa kampeni na kutumia pesa ya serikali kwa kmpeni hili sioni sawa.
lakini kuhusu mipango ya serikali mimi nadhani ilani ya chama kinacho tawala ndio mipango ya nchi, pia rais kulindwa mimi sioni tatizo.
pengine tatizo ni katiba haijaweka sawa mambo ya rais kipindi cha kampeni
 
Yuko sahihi kwa vile ni serikali yake ndiyo iliyofanya hivyo; ndiyo maana ni sahihi pia kwa upinzani kusema madhambi ya serikali yake. Unfortunately, upande huo wa pili unaonekana kuwa siyo "lugha ya kistaarabu."
 
Ingefaa watu kujielimisha kidogo kuhusu dhamana ya serikali inachukuliwaje. Uhusiano wa chama tawala na serikali ukoje Tanzania. Ilani ya uchaguzi ya chama ni nini. Ilani ya uchaguzi ya chama kinachoshinda uchaguzi inatekelezwaje na serikali, na inawezekanaje kwa chama tawala kuchukua sifa za serikali kwa kazi serikali ilizofanya kwa kutumia ilani ya uchaguzi ya chama tawala.

Serikali inaongozwa na muongozo wa chama tawala, kwa hiyo mafanikio ya serikali - kama kuna mafanikio yoyote - ni mafanikio ya ilani ya uchaguzi na uongozi wa chama tawala.

Ukihoji uhalali wa chama tawala kutumia mipango ya serikali kama ahadi na kuchukua sifa zinazotakana na mafanikio ya serikali (serikali ambayo ni ya chama tawala, hatuna hata serikali ya mseto so far) unaonekana hujui jinsi serikali zinavyoundwa. Hususan katika nchi ambayo haijawa na serikali ya mseto wala makabidhiano ya madaraka ya serikali kati ya chama kimoja na kingine.

Ukihoji uhalali wa chama tawala kutumia mipango ya serikali kama ahadi na kuchukua sifa zinazotokana na mafanikio ya serikali, utakubali pia kuhoji uhalali wa chama tawala kupewa lawama za mapungufu ya serikali ? Huwezi kuhoji uhalali wa chama tawala kutumia mipango ya serikali kama ahadi na kupewa sifa halafu ukakubali kutoa lawama.

Mipango ya serikali inakuwa mipango ya serikali kutoka katika ilani ya uchaguzi ya chama kinachoshinda uchaguzi, kwa hiyo chama kilichoingiza mipango hiyo kuwa ajenda ya serikali kina kila haki ya kuitumia katika kampeni. Haya mambo yanafanywa sio Tanzania tu, bali dunia nzima na kuna mifano lukuki.

Kama kuna mambo ya kukibana chama tawala yapo mengi tu, lakini hili si mojawapo. Kwa kupigia kelele non-issue wafuasi wa upinzani wanajionyesha kama vile hawana issues kwa sababu hakuna issues, kitu ambacho si cha kweli.
 
YES. this is well said. Nimeshangaa sana mavuvuzela hayakuonekana kwenye hii thread. Watu wamejadili thread bila majungu na kuweka ukweli hadharani isipokuwa wachache ambao uelewa wao ni mdogo na ambao walitakiwa kuuliza kwa wanaojua na si kuchangia kwani wamechangia pumba tuu.
 
Hili linanitatiza sana, binafsi nafikiri sio sahihi kabisa kwa mgombea urais kutumia mipango ya serilkali kama ahadi za chama chake.

Kwa mfano, kusema, ....tumeshaanza kufanya uchambuzi yakinifu wa barabara X na tutaanza kkuijenga mwakani.........this is wrong in my opinion.

Mnasemaje wakuu??

Hiyo ni mipango ya serikali ya CCM na yeye kama Rais aliyetoka CCM ana haki kabisa kusema mazuri yaliyofanya au yatakayofanya na serikali yake. Na vyama vya upinzani nao watasema CCM imeshindwa nini na wao watafanya nini.
 
Hili linanitatiza sana, binafsi nafikiri sio sahihi kabisa kwa mgombea urais kutumia mipango ya serilkali kama ahadi za chama chake.

Kwa mfano, kusema, ....tumeshaanza kufanya uchambuzi yakinifu wa barabara X na tutaanza kkuijenga mwakani.........this is wrong in my opinion.

Mnasemaje wakuu??

Bigirita tatizo linaloikabili nchi hii ni kutokuelewa majukumu ya serikali kwa wananchi. Elimu ndio inatuangusha maana watu wanishindwa kutofautisha wajibu wa serekali kwao. Kujenga shule,zahanati,barabara ni wajibu wa serikali na sio chama kwa hiyo hayo majisifu ya mkuu ni kuwa anajua hapaswi kusema hivyo lakini je ni nani atamwuliza kuwa huo ni wajibu wa serekali wakati anajigamba. Nafikiri kipindi hiki cha kampeni ni vyema vyama vya upinzani vikawafungua macho wananchi kuwa kujenga barabara na mashule sio ilani ya chama ni jukumu la serikali kwani tangu ukoloni vitu hivyo vilikuwapo na vizuri kuliko hizi shule zetu za kata. Kaka Mnyika na wenzako tusaidieni kwenye hili.
 
Mie naona kwa mawazo yangu JK kama mgombea wa kiti cha urais alitakiwa asilindwe kama rais bali alindwe kama mgombea urais tu.

Nijuavyo mimi kipindi cha kampeni kinavyo anza tu ndio inakuwa kikomo cha Urais wake Nchi inakuwa chini ya Jaji Mkuu lakini tangu kampeni zianze tarehe 21 naona bado mawaziri wapo kitu ambacho kinatakiwa kisiwepo wizara zinatakiwa ziwe chini ya Makatibu Wakuu ndio wawe viongozi wa kuwa wakilisha Mawaziri kwenye mikutano. Sasa sijajua tatizo ni nini hasa hadi MAWAZIRI na RAIS wawepo madarakani hadi leo na JAJI MKUU anafanyanini. KATIBA YETU INASEMAJE KUHUSIANA NA HILI!!
 
Mkuu ni makosa makubwa kujinadi kwa kutumia mkakati wa maendeleo wa taifa. Hapa kinachotakiwa ni kujinadi kama chama pekee. Maendeleo yana target every individual and that vision has to remain neutral when it comes to political campaigh. Acheni majigambo, semeni thithiem itafanyia nini watanzania kwa kutumia rasilimali zilizopo, siyo kuleta bla bla.
 
Bigirita tatizo linaloikabili nchi hii ni kutokuelewa majukumu ya serikali kwa wananchi. Elimu ndio inatuangusha maana watu wanishindwa kutofautisha wajibu wa serekali kwao. Kujenga shule,zahanati,barabara ni wajibu wa serikali na sio chama kwa hiyo hayo majisifu ya mkuu ni kuwa anajua hapaswi kusema hivyo lakini je ni nani atamwuliza kuwa huo ni wajibu wa serekali wakati anajigamba. Nafikiri kipindi hiki cha kampeni ni vyema vyama vya upinzani vikawafungua macho wananchi kuwa kujenga barabara na mashule sio ilani ya chama ni jukumu la serikali kwani tangu ukoloni vitu hivyo vilikuwapo na vizuri kuliko hizi shule zetu za kata. Kaka Mnyika na wenzako tusaidieni kwenye hili.

Inabidi uelewe kwamba, serikali inaendeshwa kwa muongozo wa chama. Serikali inaendeshwa kwa sera za chama, ilani ya uchaguzi ya chama na falsafa za chama.

Tungeweza kabisa kuwa na chama chenye kuweka mbele kutafuta mabomu ya nyuklia na kutotoa huduma za jamii hata zile ndogo tu, na serikali ingetekeleza sera hizi. Anachosema Kikwete na wenzake ni kwamba chama cha CCM kimeweka mbele mambo ambayo yana manufaa kwa wananchi, na kwa kuwa chama ndicho kinatoa muongozo wa serikali ifanye nini, basi serikali ikifanya mazuri chama kinaweza kuchukua sifa kwamba mipango yake mizuri inaleta mambo ya manufaa kwa taifa.

Unaweza kujadili kama CCM imeleta mazuri ya kutosha kujisifu ama laa Tanzania, lakini ukishakubali kwamba kuna mazuri yamefanya na serikali, serikali ya CCM, huna budi kukubali pia kwamba CCM inastahili pongezi.

Lawama tunazosikia kila siku CCM inatupiwa asilimia nyingi ni kwa sababu ya udhaifu katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya serikali. Sasa kama upinzani unaweza kutoa lawama kwa CCM kwa sababu ya udhaifu katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya CCM ndani ya serikali, kwa nini kutoa sifa kwa CCM pale mipango hiyo hiyo inapofanikiwa inakuwa nongwa ?

Baniani mbaya, kiatu chake dawa ? Mkuki mtamu kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu ?

Ukikubali kuishutumu CCM kwa makosa ya serikali, ukubali pia kuipa sifa kwa mambo serikali inayopatia.

Ukitaka kusema CCM haistahili sifa kwa mambo ambayo serikali imefanya sawa, itabidi kwa msingi huo huo wa kutenganisha CCM na serikali ukubali kwamba kwa yale mambo ambayo serikali imekosea CCM haiwezi kulaumiwa.

Huwezi kuwa na double standards kwamba nitampa mtu kazi ya uongozi, siwezi kumsifu akipatia, ila akikosea tu naweza kumsema. Huu utakuwa upumbavu.
 
Mie naona kwa mawazo yangu JK kama mgombea wa kiti cha urais alitakiwa asilindwe kama rais bali alindwe kama mgombea urais tu.

Nijuavyo mimi kipindi cha kampeni kinavyo anza tu ndio inakuwa kikomo cha Urais wake Nchi inakuwa chini ya Jaji Mkuu lakini tangu kampeni zianze tarehe 21 naona bado mawaziri wapo kitu ambacho kinatakiwa kisiwepo wizara zinatakiwa ziwe chini ya Makatibu Wakuu ndio wawe viongozi wa kuwa wakilisha Mawaziri kwenye mikutano. Sasa sijajua tatizo ni nini hasa hadi MAWAZIRI na RAIS wawepo madarakani hadi leo na JAJI MKUU anafanyanini. KATIBA YETU INASEMAJE KUHUSIANA NA HILI!!

Ujuavyo wewe ni makosa.

Nchi haiachi kuwa na rais kwa sababu ya kampeni.

Soma kifungu cha 42 cha katiba ya jamhuri ya muungano kinavyoelezea hili kwa bayana.

Ukurasa wa 34- 35 wa pdf hii http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf

Wakati na muda wa kushika madaraka ya Rais Sheria ya 1984 Na.15 ib.9

42.

-(1) Rais mteule atashika madaraka ya Rais mapema iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote itabidi ashike madaraka kabla ya kupita siku saba.
(2) Isipokuwa kama atajiuzulu au atafariki mapema zaidi mtu aliyechaguliwa kuwa Rais, bila ya kuathiri masharti yaliyo katika ibara ndogo ya (3), atashika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitano tangu siku alipochaguliwa kuwa Rais.

(3) Mtu aliyechaguliwa kuwa Rais atashika kiti cha Rais hadi-
(a) siku ambapo mtu atakayemfuatia katika kushika kiti hicho atakula kiapo cha Rais; au
(b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka;au
(c) siku atakapojiuzulu; au
(d) atakapoacha kushika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

(4) Iwapo Jamhuri ya Muungano inapigana vita dhidi ya adui na Rais anaona kuwa haiwezekani kufanya uchaguzi, Bunge laweza mara kwa mara kupitisha azimio la kuongeza muda wa miaka mitano uliotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara hii isipokuwa kwamba muda wowote utakaoongezwa kila mara hautazidi miezi sita.

(5) Kila Rais mteule na kila mtu atakayeshikilia kiti cha Rais, kabla ya kushika madaraka ya Rais, ataapa mbele ya Jaji Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake
kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
 
Wadau hii ikoje, mbona huyu jamaa anatufanya watoto wadogo. Hizi ahadi anazotoa atazitekeleza au kwasabau anatuona sisi mazoba hatutauliza? Ona hizi:

Mwanza: Serikali italipa madeni ya Nyanza yote, haya madeni yana maswali kibao, aliyeua Nyanza mpaka leo hajachukuliwa hatua, iweje leo serikali ibebeshwe mzigo wa madeni yenye utata??

Kagera: Uwanja wa ndege wa kimataifa na meli kubwa zaidi ya MV Bukoba, kuunganishwa na gridi ya taifa

Kigoma: International airport!

Mpanda: Kaagiza mahindi yote yanunuliwe na SGR wakati hata fedha hamna.

Mbeya: Kukamilisha mara moja uwanja wa ndege, bajaji 400 kwa wajawazito!!

Hiyo ni mikoa minne tu, je akimaliza nchi nzima iatakuwaje? Hiyo fedha anatoa wapi na ameshindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali? Tangu aingie madarakani serikali hijawahi kufikia malengo ya ukusaji kodi, na mwaka 2009/10 ndiyo ilikuwa worse. Huyu bwana ni muongo kupindukia!

Watanzania tuamkeni, is time for change!!!!!!!
 
Atekeleze kwa fedha gani?? Tangu June 2009 mpaka 2010 hajwahi kutimiza malengo ya kukusanya kodi hata mwezi mmoja, data tunazo. Alikuwa wapi miaka mitano iliyopita, mbona hatukuona project yoyote ya maana aliyofanya, sana sana aliishia kuzindua miradi iliyoanzishwa awamu iliyopita.

Huyu jamaa ni msanii, keshaprove failure, nilimshabikia miaka mitano iliyopita, he has disapointed us! unahitaji mtu atakayeshughulika na matatizo ya watu, sio ya familia yake na marafiki zake.

Hawezi aondoke!!!!!!!
 
Ni sahihi kabisa kwa JK kutumia mkakati huo. Kama wapinzani wake wanaishambulia serikali yake unadhani ni nani wa kuitetea? Automatically ni yeye! kwangu mimi sioni tatizo. Mnadhani ataongea nini kama si utendaji wa serikali yake na pia matarajio yke kama atapata chance. Tuacheni ushabiki, tuwe na mawazo yanayoishi na tuachane na maawazo yaliyokufa au mawazo stagnant
 
nataka mjue kwamba zitatekelezeka tena bila wasiwasi,wapinzani kazi yenu ni kelele tu hamana hoja ya msingi,tukizungumzia maendeleo sio kitu cha kufumba na kufumbua ....naomba mlijue hilo, SLAA JAPO WEWE NI KIJAKAZI WA CHADEMA , coz najua wewe ni mtu wa YES na NO ndani ya CHADEMA, unadanganya wananchi kwa kujivalisha ngozi ya ufisadi wakati ndani ya chadema wewe ni YES na NO, ulipoambiwa uwafukeze wale vijana wawili KAFULILA NA MWENZAKE ulitekeleza bila kupinga

SLAA WAAMBIE WANANCHI NA WANACHADEMA WENZIO KILICHOKUFANYA UKAMUACHA MKEO....................sitanii najua A 2 Z yako katika chadema ,toa SERA ZA CHAMA CHAKO NA SIO UNAPIGA POROJO ZA UFISADI,AMBAZO NDANI YA CCM ZIMEANZA KUSHUGHULIKIWA NA ZITAENDELEA KUSHUGHULIKIWA mpaka kitaeleweka.

CCM inasera zinazotekelezeka sio kwa porojo za maneno BALI KWA VITENDO. hili amelithibitisha kijana wako ZITTO KWABWE NDANI YA BUNGE LILILOKWISHA ,akimsifia MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI KWAMBA NI MTU MUUNGWANA..., AU BADO SLAA UNAPINGA NA HILO? wapinzani mtaelimika lini? kuachana na SERA ZA CHUKI? NA UKABILA, nasema ukabila kwa nguvu zote kwani jinsi mbinu ya kummaliza ZITTO KABWE ilivyotengenezwa sio ya kitoto...... inatisha ! KAMA NA HILO CHADEMA MNABISHA BISHENI LAKINI UKWELI NDIO HUO.
 
Back
Top Bottom