Orodha na Hatima ya Viwanda na Mashirika Yaliyobinafsishwa

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,063
2,471
Katika thread hii ningependa kupata majina ya viwanda na mashirika yaliyokuwa mali ya taifa na baadaye kubinafshwa. Kama kuna uwezekano naomba taarifa mwaka wa kuanzishwa kiwanda, capacity ya kiwanda, na sababu za kiwanda kubinafsishwa.

Inasemekana Nyerere aliacha viwanda au mashirika ya kiserikali zaidi ya 400. Kuelewa namba peke yake hakutoshi. Inabidi tupate majina na shughuli za taasisi hizo za kibiashara.

Vilevile ningependa sifa na lawama kuhusu uongozi wa Nyerere au Ujamaa zikae pembeni. Kwanini siasa za kujenga viwanda zilifanyika katika nchi za zote za kiAfrika bila kujali itikadi ya nchi hizo.

Karibuni

Wenu katika kusukuma gurudumu la ujenzi wa fikra pevu,

Za10.

1. National Housing Corporation (NHC), Bado linafanya kazi, lilianza mwaka 1962, lilifanyiwa mabadiliko 1990 (source post #2)

2. Tanzania housing Bank (THB), established by an Act of Parliament No.34 of 1972, become operational 1973. Capital 400 Tsh. Shareholder Tanzania government (46.5%), National Insurance Corporation (30.2%), National Provident Fund (23.3%)
THB collapsed in 1993. The demise of the Tanzania Housing Bank was prompted by the liberalization of the Banking Sector. The bank had issued many housing loans which were irrecoverable due to high default rate.

3. Tanganyika packers LTD was established in 1950, Ownership: Territorial government (51%), Liebig's meat Extract (49%), Nationalized in 1974, defunct

4. Tanzania Shoes Company - Viatu vya BORA

5. Tanzania Elimu Supplies - vifaa vya Elimu

6. Kampuni ya mabasi ya taifa -KAMATA

7. Shirika la Usafiri Dar-es-Salaam - UDA

8. Ubungo Garments
9. Ubungo Spinning Mills

10. Polysacks

11. Tanzania Sewing Thread

12. Coastal Dairies
 
Baadhi ya mashirika yalianza kufa hayati Nyerere akishuhudia yeye mwenyewe.

Moja ya mashirika hayo ni shirika la nyumba tanzania au THB (Tanzania Housing Bank) ambalo lilianzishwa kwenye miaka ya katikati ya sabini.

Shirika hili ambalo lilikuwa ndilo alama ya mikopo kwa kila mtanzania lilikuwa na jengo lake ambalo lipo katikati kabisa ya jiji la dar likitazama mnara wa askari.

Bosi wa mwisho wa shirika hili ni kama nakumbuka vizuri ni Basil Mramba ambae ndie alieliua kabisa kwa kushindwa kufuatilia madeni ambayo watu walichukua kama mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na wakapotea.

Hayati mwalimu aliona pia majumba yakianza kujengwa kumzunguka eneo la karibu na makazi yake Msasani.
 
Baadhi ya mashirika yalianza kufa hayati Nyerere akishuhudia yeye mwenyewe.

Moja ya mashirika hayo ni shirika la nyumba tanzania au THB (Tanzania Housing Corporation) ambalo lilianzishwa kwenye miaka ya katikati ya sabini.

Shirika hili ambalo lilikuwa ndilo alama ya nyumba kwa kila mtanzania lilikuwa na jengo lake ambalo lipo katikati kabisa ya jiji la dar likitazama mnara wa askari.

Bosi wa mwisho wa shirika hili ni kama nakumbuka vizuri ni Basil Mramba ambae ndie alieliua kabisa kwa kushindwa kufuatilia madeni ambayo watu walichukua kama mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na wakapotea.

Hayati mwalimu aliona pia majumba yakianza kujengwa kumzunguka eneo la karibu na makazi yake Msasani.

Nime-google na inaonyesha shirika hili bado linadunda. Na wana website NHC Profile.

Nitaliweka kwenye orodha ya mashirika ya umma.
 
Tanganyika Meat Packers -usindikaji nyama

Tanzania Shoes Company - Viatu vya BORA

Tanzania Elimu Supplies - vifaa vya Elimu

Kampuni ya mabasi ya taifa -KAMATA

Shirika la Usafiri Dar-es-Salaam - UDA
 
serikali haiwezi ku run business tembea uone,ni private companies ndo zinazoendelea zaidi,ni jukumu lako kutafuta shirika lililokufa na ulifufue
 
Tanganyika Meat Packers -usindikaji nyama

Tanzania Shoes Company - Viatu vya BORA

Tanzania Elimu Supplies - vifaa vya Elimu

Kampuni ya mabasi ya taifa -KAMATA

Shirika la Usafiri Dar-es-Salaam - UDA

mkuu kama unaweza kuweka maelezo kidogo ya hayo mashirika kama kuanzishwa, kubinafsishwa na hali yake kwa sasa.
Shukran.
 
serikali haiwezi ku run business tembea uone,ni private companies ndo zinazoendelea zaidi,ni jukumu lako kutafuta shirika lililokufa na ulifufue
Na ukipewa mfano wa mashirika yanayoendeshwa na serikali (nchi nyingine) tena kwa ufanisi utasemaje?
 
serikali haiwezi ku run business tembea uone,ni private companies ndo zinazoendelea zaidi,ni jukumu lako kutafuta shirika lililokufa na ulifufue

tatizo watumishi wa umma wamekosa uzalendo, mbona nhc inajiendesha kibiashara na inafanya vizuri sana?

Kwa nini serekali isichangie mitaji kwa wawekezaji wazalendo ili kuwavutia na kuweza kuvifufua?
mfn serekali itoe asilimia 49 ya gharama za kufua kiwanda na muwekezaji atoe 51 nae aendeshe kiwanda.

Kiwanda kikisha jiimarisha labda kwa miaka 2 serekali iuze hisa zake kwa wananchi ili hizo fedha iwekeze kwenye sekta nyingine?
 
Tanganyika Meat Packers -usindikaji nyama

Tanzania Shoes Company - Viatu vya BORA

Tanzania Elimu Supplies - vifaa vya Elimu

Kampuni ya mabasi ya taifa -KAMATA

Shirika la Usafiri Dar-es-Salaam - UDA

I have added the list into my introduction.
 
tatizo watumishi wa umma wamekosa uzalendo, mbona nhc inajiendesha kibiashara na inafanya vizuri sana?

Kwa nini serekali isichangie mitaji kwa wawekezaji wazalendo ili kuwavutia na kuweza kuvifufua?
mfn serekali itoe asilimia 49 ya gharama za kufua kiwanda na muwekezaji atoe 51 nae aendeshe kiwanda.

Kiwanda kikisha jiimarisha labda kwa miaka 2 serekali iuze hisa zake kwa wananchi ili hizo fedha iwekeze kwenye sekta nyingine?

Do you expect a person who isn't well paid or supervised to be a patriot?
 
Sababu kubwa ya haya mashirika ku binafsishwa ni nn? Msaada tafadhali kwa mwenye uelewa..
 
Sababu kubwa ya haya mashirika ku binafsishwa ni nn? Msaada tafadhali kwa mwenye uelewa..

HOPE man Hiyo ilitokana na uzembe wa serikali kutokujua namna ya kuendesha na kusimamia investments zake za kiuchumi. Ikadhani kuwa ikiwapa watu binafsi basi holaa mambo yatajipa: kumbe mkenge tu.

Nikirudi kwa Z10 (Zakumi ) kwa post yake ya miaka saba iliyopita: Zamani sana kulikuwa na mashirika yanayohusu nafaka za chakula kama National Milling, Gapex, na mashirika ya maendeleo wilayani kama vile TARDECO, MORODECO, MWADECO, SHIDECO, MUDECO, KADECO na kadhalika ambayo yalikuwa yametapakaa katika kila wilaya. Je bado yote hayo yapo? Vile vile kulikuwa na mashirika ya ya biashara kama STC (Saidia Tujenge Chetu), na mangene sikumbuki majina yake yaliyokuwana jukumu la kuuza na kununua biadhaa kutoka nje kwa ajili ya taifa; je una taarifa zake?.

Katika kuzurura kwangu mtandaoni nikakutana na hii beji ya STC ya kusherehekea miaka kumi ya uhuru mwaka 1971

1123418
 
Asante bwana Kichuguu,, lakin ningeomba kuuliza hilo shirika la nyumba NHC linamilikiwa na private sector?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom