Original komedy kwishiney

Status
Not open for further replies.
Kwa dhambi ya kufungamana na hawa ccm na kukebehi wapigania haki na raslimali za nchi yao, hiyo dhambi iwatafune siku zote kuanzia hivi sasa,
daima malipo ya usaliti ni hapahapa duniani,
ila njaa mbaya.
 
Mimi
nasema watu wote walioipigia kampeni au wanaendelea kuipigia chapuo CCM
lazima laana iwaangukie.The original komedi wanavuna walichopanda,na
kwa kweli hawa jamaa watafulia mpaka aibu..sijui watakimbilia
wapi.Walidanganywa na Manji na vihela vya msimu.Laana ya kuwapigia
kampeni CCM inawala na itawala sana.
Waende Clouds TV.
 
watajuta kunyea kambi ya mzee mengi,wamrudie tu mzee wao yule ndio aliyewatoa atawasamehe,otherwise waende kwa manji awape kazi ya kuchekesha wateja pale nje kwenye mall yake pale nyerere road quality
Hawakujua kwamba ulikuwa mpango wa manji wa kumuudhi Mengi kupitia kwao na Yanga Afrika, Mwenzao katimiza lengo lake sasa wote kawatema kama big G.
 
kiukweli jamaa walikuwa vizuri ,walileta mapinduzi katika tasnia ya vichekesho,walikuwa wabunifu sana.Si vizuri tukawashambulia sana kwa kunyea kambi pale EATV kwani hatujui mkataba wao ulikuwaje,sanaa ya bongo si endelevu hili ni tatizo linalowakumba wengi,kwani leo nani anataka kumsikiliza KINGWENDU? HAYO NDIO MAISHA YA SANAA YA BONGO UKIWA JUU KULA UWEZAVYO MAANA UKISHUKA HAURUDI TENA JUU.
 
CCM hapa inaingia vipi? Hawa wanatumiwa tu kama waburudishaji, na hamna sehemu yoyote ambao wameshawahi kusema wao ni CCM. CDM pia ikiwahitaji kwenye kampen zao hawa zecomedy hawawezi kukataa cuz hawana mkataba na CCM!

Chamuhimu hapa jadilini hatma ya hawa vijana na siyo kuingiza mambo ya CCM hapa

No Pain, No Gain! Always ukweli unauma..
 
Mzee Mengi ndio mlezi wao kisanii toka waanze sanaa za kwenye runinga, swala la wao kumtukana na kumdhalilisha baada ya kumpata Manji ni dhambi mbele ya Mungu na malipo yake ni hapahapa duniani.

Ile nafasi waliyokuwa wameipata kwa mzee mengi wataijutia sana. Walijiona wajanja kumtusi mzee wa watu kwa vihera vya manji. Kwa kifupi hawa raia hawana jipya labda warudie kuusoma vema ushauri aliowapatia Shigongo
 
Mzee Ngongo taratibu...! sio kila mwanamke wa bar ni wa hovyo. Ile ni kazi kama kazi nyingine. Bila wao sijui bar zingekuwaje.


Mkuu Ngorunde,

Ni kweli mkuu wangu unajua wakati mwingine vidole vinakwenda kasi kuliko ubongo unafikiri.

Mkuu natumaini hapa uliteleza kidogo

Mkuu Paulss,

Nadhani niliteleza sana.Nachukua fursa hii kuwaomba radhi wanawake wote wauza bar popote walipo hasa maeneo ya Arusha hasa ukizingatia bila huduma zao maisha yangekuwa shabala bagala.
 
Tena namsikia Mpoki ndani ya Mawingu ktk kile kipindi cha leo tena,akichambuwa mambo na watangazaji wengine,labda ndio kalamba ajira huko nini?
 
Tu show zinarudiwa rudiwa nikajua kabsaa hali si shwari lzm kutakuwa na sintofahamu hapo. Jamaa wakipigwa chini hapo baaasi labda waende c2c television yaani full uswazi
 



Mkuu Paulss,

Nadhani niliteleza sana.Nachukua fursa hii kuwaomba radhi wanawake wote wauza bar popote walipo hasa maeneo ya Arusha hasa ukizingatia bila huduma zao maisha yangekuwa shabala bagala.
huu msisitizo nimeupenda
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom