Original komedy kwishiney

Status
Not open for further replies.
watajuta kunyea kambi ya mzee mengi,wamrudie tu mzee wao yule ndio aliyewatoa atawasamehe,otherwise waende kwa manji awape kazi ya kuchekesha wateja pale nje kwenye mall yake pale nyerere road quality

nakumbuka ITV ndio waliowaleta na kuwatambulisha kwetu,nilishangaa sana walivyomtukana yule mzee Mengi,jamani tujifunze kufikiria tulikotoka
 
Kuna wale wa EATV jamaa wako njema sana,nadhani watachukua usukani...jamaa wanafanya kipindi alhamisi muda uleule wa original komedi wa TBC ila mimi uwa nawatch hawa jamaa wa EATV....halafu ukitaka kujua kuwa jamaa wa ORIGINAL KOMEDI wamefulia walikuwa wanachonga sana Facebook,now days wamejificha yaani kwa mfano huyu masanja nadhani kaishiwa hata hela ya vocha ya kuweka kwenye moderm....
Wale wa EATV ndio vilaza kabisa!
Halafu wewe yaelekea una chuki binafsi na akina masanja! Kwa taarifa yako hawajafulia..wana nyumba nzuri, magari mazur na biashara zao! Tofauti na wewe ambaye sidhani hata kama una uwezo wa kujinunulia kitanda!
 
ccm hapa inaingia vipi? Hawa wanatumiwa tu kama waburudishaji, na hamna sehemu yoyote ambao wameshawahi kusema wao ni ccm. Cdm pia ikiwahitaji kwenye kampen zao hawa zecomedy hawawezi kukataa cuz hawana mkataba na ccm!

Chamuhimu hapa jadilini hatma ya hawa vijana na siyo kuingiza mambo ya ccm hapa

ccm ndio chanzo cha laaana zote hapa nchini.
 
CCM hapa inaingia vipi? Hawa wanatumiwa tu kama waburudishaji, na hamna sehemu yoyote ambao wameshawahi kusema wao ni CCM. CDM pia ikiwahitaji kwenye kampen zao hawa zecomedy hawawezi kukataa cuz hawana mkataba na CCM!

Chamuhimu hapa jadilini hatma ya hawa vijana na siyo kuingiza mambo ya CCM hapa

Walijidhatiti sana na Kampeni za CCM wakati watu washachoka....then umaarufu wao baada ya kampeni ukaanza kushuka kwa kasi ya ajabu sana...isitoshe pia walishamtukana sana Shigongo na ndiyo maana habari zao haziandikwi tena kwenye magazeti pendwa!! Unganisha dots Rejao

Wamenyea kambi hawa mabwa-mdogo!! Labda waende Efatha kwa Mwingira baada ya mahubiri waonyeshwe hawa.
 
Wale wa EATV ndio vilaza kabisa!
Halafu wewe yaelekea una chuki binafsi na akina masanja! Kwa taarifa yako hawajafulia..wana nyumba nzuri, magari mazur na biashara zao! Tofauti na wewe ambaye sidhani hata kama una uwezo wa kujinunulia kitanda!

Yaonekana unawajua sana hawa vijana mkuu!!!! Lakini kuwajua kwako isiwe kero kwa wenzako kwani hakuna sababu ya kutoa matusi kWA SABABU YA KUTOWAJUA HAWA JAMAA ZAKO.
 
Yaonekana unawajua sana hawa vijana mkuu!!!! Lakini kuwajua kwako isiwe kero kwa wenzako kwani hakuna sababu ya kutoa matusi kWA SABABU YA KUTOWAJUA HAWA JAMAA ZAKO.
Sidhani kama kuna sehemu yoyote nimetukana..aliyetukana ni huyo anayewaponda bila kujua wana hali gani kiuchumi.
Kisanaa tunakubali kweli wameshuka, but kiuchumi bado wapo vizuri
 
Naona wameanza kujipenekeza ktk FM RADIOS maana nimemsikia Masanja ktk kituo cha Times fm na Mpoki ktk Clouds fm. Inabidi wawe wamejipanga ipasavyo ili nao wakose kuwa ktk kundi la Kina sisi TULIOFURIA.
 
Hawa jama wako njema sana mfukoni.wote wana nyumba zao binafsi isipokua kiongozi wao.na wana biashara ndogo ndogo zinawapa kipato .nadhani facebook ya kinondoni ni ya mmoja wao,vengu cjui ye yukoje.hata wakiacha kuigiza usitegeme watatangatanga kama tulivyo zoea .walimtumia manji vizuri na ccm .kipindi kile wako peak.kwa hyo msitegeme kuwa watakuwa maskini.Mengi aliwa opress na still ana oppress wandishi wake kimshahara.wandsh wachache wanafaidi wengi bora liende
 
Naona mnataka kuleta uchama na siasa kwenye hili jambo . Hawa jamaa ni wazuri kuliko wale vilaza wa eatv hilo kila mtu anajua . Hakuna mtu bongo asiyemjua joti au masanja . Paka watoto wakawa wanaiga staili ya kushtua ( kijoti joti ) . Kosa sio kuhamia tbc ila kosa ni kuhama eatv na kumtukana mzee mengi aliyewafikisha hapo alipo .
 
Wanakufa natural death,jana nimeangalia FUTUHI nao naona mwelekeo ni huo huo,wale wasanii waliokuwa na mvuto wote hawapo,waliopo wanaboa sana.Nadahni Comedy inahitaji new blood
 
Mdomo huponza kichwa.. baada ya kupata mafaniko kwa Tajiri aliyewapatia kazi iliyo muweka ktk Mwanga na ulimwengu kuwatambua {hasa Masanja} then wakajiona wamewin,wakamtusi pac na kufahamu bila ya yule aliyewapa kazi wasingeuona huo mwanga..Sikio halizidi Kichwa
 
Wasanii wa bongo na mjifunze kwa haya ya wenzenu as mkijenga....kwenye gazeti.....mkinunua gari....kwenye radio kutangaza.....haya ni maisha ya kawaida sana wandugu na mjue kuna kupanda na kushuka pia......na umaarufu wenu hauliwi wala hautawalipia bill za maisha.

Na mtambue watu hupunguzwa kazi na elimu na uzoefu wao itakuwa kipaji????

Heshima kitu cha bure hata ukiwa maarufu......mzee mengi mtaenda kumuangukia tuuu as huo muziki mnaodhani mtauweza thubutuuuu yenu vipaji ni vingi sana na wanafanya kazi based on profession na sio umaarufu tu......kama umaarufu basi mzee small ndo angekuwa juu sana katika muziki

Mkipata umaarufu na pesa ya kubadili mboga mkumbuke na shule pia.....elimu ndo permanent asset
 
Duh hawa jamaa nilijua lazima watapotea katika ulimwengu wa vichekesho .Origional Komedy walifanya makosa makubwa kuchanganya fani yao ya vichekesho na ushabiki wa siasa na mpira,walikubali kutumiwa na CCM na kutumiwa na mfadhili wao kushabikia Dar Young Afrika haya ni baadhi ya mambo yaliyochangia kuwaangusha.

Hakuna jambo la hovyo walilofanya kama kumtukana Mzee Mengi hili lilinifanya niwaone kama wanawake wa Bar.
 
Mabosi wa TBC wamekuwa wakipigana vikumbo kukwepa ku renew contract ya hawa vijana machachari wanaokosa umaarufu kila kukicha,taarifa zinasema wao wenyewe wameanza kushtukia hiyo baada ya kipigwa kalenda kila siku huku ma technicians wa TBC wakirudia rudia show zao zilizopita miaka mingi,,kwa nini TBC wasiwe wazi na kukataa ku sign au ku sign ili hawa wandugu wajue moja??Tbc wakikataa ku sign hawa jamaa itakuwa ndio mwisho wao au wataenda ITV?watathubu kwenda ITV na walishamtukana mzee Mengi live kila mtu aliona??waswahili wanasema usinyee kambi,,kazi ipo!

Bora wahamie Chanel Ten au Clouds TV
 
Kumbe ndio maana masanja anaparamia dili za akina kakobe,lwakatare, mzee wa upako. Sio mbaya inaweza ikamlipa
 
Duh hawa jamaa nilijua lazima watapotea katika ulimwengu wa vichekesho .Origional Komedy walifanya makosa makubwa kuchanganya fani yao ya vichekesho na ushabiki wa siasa na mpira,walikubali kutumiwa na CCM na kutumiwa na mfadhili wao kushabikia Dar Young Afrika haya ni baadhi ya mambo yaliyochangia kuwaangusha.

Hakuna jambo la hovyo walilofanya kama kumtukana Mzee Mengi hili lilinifanya niwaone kama wanawake wa Bar.

Mzee Ngongo taratibu...! sio kila mwanamke wa bar ni wa hovyo. Ile ni kazi kama kazi nyingine. Bila wao sijui bar zingekuwaje.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom