ORIGINAL imechakachuliwa.

cheusi, akijidanganya mwenyewe kuna shida gani? Au inakuuma wewe ambaye umetumia zaidi ya $1,200 kununua hizo nywele za mbrazil na wote mkaonekana mbele ya kina Kongosho (ambao ni wengi) mko sawa?

my love mtu ambaye kwa mfano ameshawahi kuwa na hermes bag ya kweli akiiona feki yake hata ikiwa umbali wa hatua tatu mbele ataijua tu,ambao watadhani kuwa mim niliyena kitu changu cha ukweli wakadhani ni sawa na kile cha mtu aliyenunua feki watakua ni wale ambao hawajawahi kuona cha ukweli kilivyo.Haya mabegi au viatu vya madesinger wakubwa vinatofauti nyingi na copy zake,mfano zile nyuzi tu wanazotumia kushonea viatu au mapochi unakuta jinsi zinavyoingia na kutoka zinakua zina idadi ambayo kila pochi ya aina hiyo ina idadi sawa nayo na alama nyingine nyingi.
Hivyo sijaandika sbb roho inaniuma kuwa nitaonekana sawa na wa fake,na sina shida mtu kuvaa fake,bali tu nimeona ni vizuri mtu ukivaa fake ujue ni fake,kuliko kuvaa fake halafu ukapita ukisema kwa kujiamini kuwa ni original sbb fake inajulikana tu.
Yaani kama tunavyofundishana kupaka wanja,japo kila mtu ana uhuru wa kupaka wanja wake atakavyo,sio mbaya pia kufundishana kuepeuka aibu kwa kuvaa fake bila kujua ni fake.Mtu akiuziwa kitu fake akashawishiwa kuwa ni original inakua kama vile ametapeliwa ndo mana najaribu kuwafumbua watu macho,wajue kuwa vitu vya big designers sio vya kitoto,bora mtu ununue fake yako kariakoo ukijua ni fake na unavaa ukijua ni fake kuliko kitu hicho hicho unachoweza kupata kariakoo kwa elfu kumi
 
kweli wanawake wana kazi...............

we acha tu tuna kazi sana baba angu,ubebe mimba miezi tisa,uzae kwa uchungu,ulee hadi aweze kujitegemea bado akiwa na maisha yake anaweza asikukumbuke,wengine wakutukane,akioa mke mke anaweza kukuita eti mama mkwe mchawi,bado baba zao wanatuhitaji tuwaridhishe,na hata uwaridhishe vipi bado watatatafuta nyumba ndogo,kama ni mlevi akirudi akupige sura yote iwe na ngeu kuliko sura ya tyson,ukileta housegirl lazima amfanyie launching,ukileta houseboy baba anaweza yeye ndo akafanyiwa launching maana wababa wa leo wengi ni kama wa sodoma na gomora.Sasa unadhani hiyo ni kazi ndogo mkuu.
Acheni tu tujifariji na malace front wigs tuna kazi kubwa sana wanawake,nyie hamna kazi.
 
Waambie bana, wanatuchafulia sisi maselebriti. Yuko sistaduu mmoja hapa mpaka colgate ananunua feki lakini pozi zake utazani anjelina jolie. Nyambaaf zake
 
msema kweli mpenzi wa Mungu,nataka Mungu anipende ndo mana nimesema ukweli.
Wewe hauoni wamekimbia chit chat leo. Hii Jeiefu kumbe imejaa feki. Ubarikiwe cheusi kwa kufichua huu uoza. Sumu hawawezi kukuwekea online lakini tahazari wasje wakakuwekea fitna ukalambwa ban.
Long live cheusi
 
lol, sina cha kuongeza.

Cheusimangala mie nakusalimu tu mpendwa... Nimekumbuka ile ndoto yako..

baada ya salam mim sijambo,usiongelee ile ndoto shemeji yako bado yuko kwenye coma kila akizinduka akiniona anazimia tena.
 
Wewe hauoni wamekimbia chit chat leo. Hii Jeiefu kumbe imejaa feki. Ubarikiwe cheusi kwa kufichua huu uoza. Sumu hawawezi kukuwekea online lakini tahazari wasje wakakuwekea fitna ukalambwa ban.
Long live cheusi

hata wakiniwekea vichupa elfu vya klorokwini sifi sbb Mungu kanipenda kwa ukweli niliosema.
Kuhusu ban mie mwenzio nina immune,siwezi kupata na siku nikipigwa ban ujue na server ya jf itajipiga ban.
 
Hili neno ORIGINAL naona wabongo wameamua kulichakachua.Ninamaanisha kwamba,mara nyingi utasikia mtu anakwambia nenda duka fulani wale wanauza lace wig au brazillian hair original.

Kusema ukweli mim naona kama wadada wengi wakibongo hawajui wanachokiongea hasa kwenye maswala ya vipodozi,nywele na human hair.
Vitu kama MAC make ups,brazillian hair na designer pieces kama nguo viatu na mabegi vinapendwa sana na wadada wa kibongo sababu wamesikia viko juu na watu wenye pesa zao wanavitumia hivyo na yeye anapokua navyo anajiona yuko juu.

Ila ukweli ni kwamba hivi vitu vyote mtu ukinunua bongo ni fake,copy kutoka china na thailand.Kama hizo nywele nyingi zinakua zina quality nzuri na zinaonekana kama real human hair lkn ni fake,mtu huwezi kununua brazilian hair ya kutosha kichwa kizima ya ukweli kwa laki 3,watu tunatoa hadi milion mbili kwa hizo nywele za ukweli halafu mtu anakupitia na vya kwake vimekakamaa anakwambia ni original,how come.

Unakuta mtu kavaa loubs kanunua elfu themanini za kikwete anadai ni original.

Ila sio wadada tu hata mabrazameni,wanashobokea sana vitu vyenye majina lkn ni aibu mtu kapiga mtisheti wa YSL mbwembwe nyingi halafu hata bila kuulizwa atakwambia original hii nimenunua elfu sittini,za kikwete,hii si aibu jamani,maana yaani unajua tu kaka wa watu hata hajui ukubwa wa hilo jina fake alilovaa.

Mi naona ni vizuri kuacha kusema copy za big brands kuwa ni original wakati zimefyatuliwa hapo Thailand.Vile vile kwenda na fasheni sio lazima kuvaa big names wakati uwezo wa kupata original haupo,kuliko kuvaa immitations huku wanaojua vya ukweli vikoje wakitusanifu ni bora kuvaa vitu ambavyo havina majina lkn ni vizuri.

Kama hujaipenda mada yangu gonga like.
Kama umeipenda usinipe like.

Love u all.

Unajifanya unajuwa sana,chekechea puraimari mupaka sekondari hujapata vema..mie nakwendaga kuparis kupata muvitu za kuvaa na majewely.
 
,mtu huwezi kununua brazilian hair ya kutosha kichwa kizima ya ukweli kwa laki 3,(watu tunatoa hadi milion mbili )kwa hizo nywele za ukweli halafu mtu anakupitia na vya kwake vimekakamaa anakwambia ni original,.
upo juu dada, bora umewachana live waache kujishaua na vitu vyao fake wakati watu mnaspend mamilioni ya pesa. Bg up.
 
cheusi, akijidanganya mwenyewe kuna shida gani? Au inakuuma wewe ambaye umetumia zaidi ya $1,200 kununua hizo nywele za mbrazil na wote mkaonekana mbele ya kina Kongosho (ambao ni wengi) mko sawa?

inauma kaunga, utupie wigi lako original la mil 2 halafu yule mwenye fake la elf 10 kapendeza zaidi yako...oops! Kumbe swali la cheusie.
 
unajua kitu kimoja mi sijakuelewa wewe...so unataka mtu asiseme orijino au unataka aseme kanunua milion 100.Sikia nikuambie,kama wewe unavisent vya kutosheleze mpk ukawaponda wenzio kuna mwingn zaid yako anakuona mshamba vilevile coz anatumia vya fest zeo grade SAWA....acha kila mtu ajisifu kwa nafasi yake na kwa uwezo wake...ulichokisema hapo ni DHARAu kwa wengine kama unahela KWENUUUUU si hapa.alaaaaaaa!
 
teh teh punguzeni hasira kidogo wazalendo mtaniua mwana wa mangala,sikujua nitawaumiza wengi namna hii.

Hata hivyo nilishatabiri kuwa wengi wenu mtaboreka,sikutegemea coment ya kunisupport hata moja,kwa kifupi ni kwa kwamba nilijua sitatishika na coment ya aina yeyote kutoka kwa yeyote na ndio maana sikusita kuwaletea waraka huu.

Mim siogopi kusema kitu chochote cha ukweli au ninachoamini kuwa kinastahili kuongelewa kwa hofu ya coment za kunirarua,ilimradi tu simtukani mtu wala sikiuki sheria za JF.

Mara nyingi ukweli unauma,tunao madesigner wetu kama kina Ally Remtula,kina chichia,kuna kina Asia idarious na kina masoud kipanya wanatengeneza nguo nzuri tu,badala tuvae ubunifu wao ambao sio wa ghali ukilinganisha na madesigner wa italia na kwengineko ughaibuni tunaowashobokea,tuko radhi tuvae immitations za designers ambao tukiambiwa ukweli kuwa hatuwamudu tunalipuka kwa hasira.

Mim lengo sio kumdharau mtu,bali kuwafumbua macho wale ambao hawajui hizo bidhaa original zikoje kiasi kwamba wanaibiwa hela zao kwa kudanganywa kuwa fake ndizo original.Mim mnanikasirikia bure tu,lakini hebu fikiria kuwa kitu hicho hicho unaweza kukinunua kariakoo kwa elfu 10 halafu mtu anadanganywa kuwa kitu hicho hicho ni original anatoa elfu 80.Nchi za ulaya ni marufuku kwa duka au mtu yeyote kusema hii saa ni Rolex wakati ni copy ya Rolex.
Wachina hawadhubutu kuingiza hayo matakataka kwenye nchi zilizoendelea.

Faida ambayo mtu unaweza kuipata kwenye uzi wangu ni hii,ninakufumbua macho ujue kuwa big names zote zinazouzwa bongo ni fake,hivyo hukatazwi kuvaa fake kama roho yako inapenda ila usidanganywe ukatoa elfu 80 ukaacha kununua zile za kariakoo za elfu 10 kwa kuamini kuwa zile ndio fake.Lengo langu la kuwasaidia wapenda fasheni kusave pesa hamlion mnakimbilia kunichukia.Nani asiyejua hali ya watanzania wengi ni ngumu,tena sana hivyo inapopatikana mbinu ya kusave pesa kwa muonekano ule ule inabidi iongelewe haraka.

Week end njema jamani nakwenda kupata prenatal massage kidogo.
Cheers.
 
Back
Top Bottom