Original comedy kwisha kazi sasa!

Ptz

JF-Expert Member
Aug 23, 2011
541
384
Nimekuwa nikifuatilia hawa akina Masanja, Joti, Mpoki na wenzie mbona marudio marudio ya nyuma, hawana jipya? Kama leo wametoa ya Gongo La mboto waloitoa mwaka jana na mengine mengi yalopita! Hawa jamaa wameishiwa kabisa! Kama kuna mtu anajua kinachoendele kwa hawa jamaa atujuze!
 
we uko wapi. Inaelekea ni mgen humu mjengoni..hii kitu ilasha wekwa sana hapa yakwamba tbc wamekataa kuingia nao mkataba mpya...hivyo wanabaki kurusha recorded za nyuma, wamefulia haswaaaaa!! Ila sio ki pesa!
 
we uko wapi. Inaelekea ni mgen humu mjengoni..hii kitu ilasha wekwa sana hapa yakwamba tbc wamekataa kuingia nao mkataba mpya...hivyo wanabaki kurusha recorded za nyuma, wamefulia haswaaaaa!! Ila sio ki pesa!

Mimi nina wasiwasi kama bado wako hewani maana hata website yao hawajaupdate tangu mwaka jana. Au nayo wamenyimwa mkataba?!
 
mi hawa jamaa nawakubali sana, 4sure wataibuka soon, hebu tulieni wananchi
 
Tuachilie mbali, hawa jamaa ni innovative na kwa hiyo wana soko zuri mda wowote wataibuka kama alivyosema BLB
 
wasubiri uchaguzi ujao au waende arumeru wakawapigie magamba kampaini.......washafulia hao....
 
hawa jamaa kwisha habari yake wengine wamekuwa walokole wengine wagonjwa ili tuliwapenda itv iliwapenda zaidi, kifo chema jamani ehe, ndio mtajua mengi ni nani
 
Mwez mmoja au miwil nyuma,masanja alikua anafanya kipind on Tymz fm,kuanzia sa kumi to kumi na 2,alikua na steve Nyerere,tena during mg0m0 wa kwanza wa madaktar,cjui kama anaendelea
 
Warudi kwa Mengi sasa wakalambe matapishi yao
Kama alivyofanya Mancini kwa Tevez,lakini nakumbuka Dr Remmy aliimba tusirudi nyuma .nachowaambia Ze Komedy Mengi sio Mungu na maisha sio lazima yatoke kwa Mengi,mna kipaji kitumieni msikubali kuwapigia magoti hao wamiliki wa vyombo vya habari ,nao wananufaika kupitia migomgo yenu,tafuteni stesheni za TV hata Kenya nyie ni brand tosha ,huko Kenya wanapenda kiswahili cha bongo na wako huru mnaweza hata kumukomedy hata Amolo au Mzee wa Gofu na msifanywe chochote,kwa vituko vya wanasiasa wa Kenya mnaweza kuwa moto wa kuotea mbali
 
Pamoja na yote, wanahitaji kurudi kambini kujifua upya, wamechosha na kwa kuwa TBC hawakua na muanglizi wakatumia umaarufu na kwa kweli wamekwisha. Sasa kama wanataka kurudi wajifue upya wasilete huu mchezo wa kipumbavu, kuhusu comedy kwa ujumla nakubali kwamba wale wa ITV waliojidai kutaka kutoka zaidi ya hawa hawakuweza kutoka kabisa, ni uchafu kama ule wa zembwela actually huwezi hata kuangalia, hivyo kwa hilo wameshinda maana kweli imeonyesha pesa si talanta. lakini lazima wasome sana na wajifunze kila siku maana pia program ya weeklky ni mzigo kama huna kifua
 
Back
Top Bottom