ORGANISED AUTOSTOP-(HITCHHIKING) in Tanzania

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,062
Wakuu,

Nimeona hii niifungulie thread yake peke yake ili tuijadili maana siku moja inaweza kuwa msaada kwenye jamii yetu. Tafadhali, TUSIMLENGE MWAKYEMBE hapa maana ametumia tu kama mfano ila tujadili in GENERAL kwa watu wote wa Tanzania wenye magari na kuamua kusafiri peke yao. Maoni yenu mnasemaje?

...Wakati tukiendelea kubishana juu ya kama ni ajali ya kupangwa ama la naomba kusema neno moja ambalo halimlengi Mwakyembe as such bali bali namtumia kama alama tu ya ubinafsi wa wabunge wetu. Hivi mtu unatokaje Mbeya ama Makambako mko wa wawili tu kwenye gari la VX lenye uwezo wa kuchukua watu wengine watatu waliokaa comfortably? Hivi kweli hakukuna na wananchi wa kwenda Dar kutoka Mbeya ambao Mbunge ama dereva angejisumbua kidogo tu angeweza kuwapata na hivyo kuwapunguzi gharama za usafiri????? Narudia tena, Simlengi Mwakyembe bali namtumia tu kama ushahidi wa Ubinafsi wa Wabunge wetu. Msitupe Ngumi.

Baba Desi,,

Hilo unalosema hata kama ni la wabunge wote bado si HAKI kwa sababu hakuna mtanzania mwenye gari yake binafsi anayewachukua watu ovyo ovyo kisa kuwapunguzia gharama za usafiri

Anzia na DSM watu wangapi wanaenda makazini, anampita jirani yake ambaye anajua anaenda huko huko? Kwa nini hili liwe ajabu kwa Wabunge?

Hivi Rais na msafara wake wanachukua watu? Mimi nadhani asingeweza kufanya hivyo kwa sababu za kiusalama zaidi hata kama utashi ungekuwepo, hasa ukizingatia hali ya kisiasa inayomwandama yeye binafsi na wabunge wengine wenye misimamo kama yake ya kupinga ufisadi; pili, kwa sababu za kibima, kama abiria wakipata ajali kwenye gari lake nani angewalipa?

Lakini la muhimu, ebu mniambia kwa mlioa ulaya na marekani huwa watu wanapeana lifti?

Mzee,
Hapa kula 5 kabisa kutoka kwangu. Hivi umesomea mambo ya Economic in Transport au mambo ya Ecology? Unafahamu kuwa kuna baadhi ya nchi wanatenga barabara kwa ajili ya mabasi na taxi na pia wanaongeza gari lolote lenye abiria zaidi ya 4? Unakuta hiyo lane nyeupe wakati nyingine zimebanana magari hadi unapata hamu ya kutafuta abiria kwa nguvu ili ufike haraka uendako. Hivyo, watu hutafuta kwa nguvu sehemu wanazoishi abiria (hasa wanafunzi) ambao kila siku asubuhi wanawabeba na kuwashusha mjini. Hiyo huwasaidia wao na kusaida wengie na wakati huohuo, wanapunguza msongamano wa magari na kupunguza kuchoma mafuta na makelele.

Miaka ya 90 nilikuja kujua kuwa German walikuwa na utaratibu wa kwenda kujiandikisha kama unataka kwenda nchi fulani. Badala ya kusimama na kibao barabarani na kuonyesha kidole na mwiso unabebwa/unabeba jamaa hulifahamu na kuishia kudhurika, wao wana-organise hizo safari. Wanakutafutia abiria na siku unaondoa mnakutana na kuanza safari pamoja. Hii inafanya usisafiri peke yako na ni safe kwani wote mnaacha data zenu na pia kupunguza gharama kwa kuchangia mafuta.

Sijui kwa Tanzania huu utaratibu unawezekanaje. Ila kama ofisi ya mbunge wilayani ikiwa ina organise, nafikiri inawezekana kwani itakuwa inajulikana mapema, abiria zake wako wapi.

Babadesi/Mods, naomba ikibidi hii muifungulie thread yake peke yake ili ikiwezekana, huu utaratibu uanze walau kwa mkoa wa Dar, watu wawe wanabeba vitoto vya shule. Unakuta mtu anaenda Posta, ndani ya shangingi, PEKEEE YAKE!!! Too Sad.

Kidogo ukisoma maelezo yangu hapo juu, ninapisha na wewe. Hiki kitu kinawezekana kabisa na usalama ukawepo. Kwani wakati anaenda kuwaomba kura, hao RAIA WAOVU wanaoweza kumdhuru kipindi hicho huwa wameenda likizo? Akishinda ubunge tu, basi jamaa wanaanza kazi ya kumsaka wamdhuru.
Pia Babadesi anazungumzia IN-GENERAL. Nchi nyingine wanafanya hili kwa mafanikio makubwa. Amini usiamini, kama wangelijenga barabara pale Dar na kutenga lane moja kwa ajili ya mabasi, taxi na magari yenye abiria zaidi ya 4, shangingi zote zingelijaa hadi ukashangaa. Ningelikuwa na uwezo, ningelifanya hili kwa kutumia mifano live.

Mkuu kwa hili? sidhani..wenyewe wana matangazo yao, kuna bwana mmoja anaitwa FATAKI, na wamemhusisha na wakina baba wanaobeba vibinti vya shule na kisha kuwafanyia mchezo mbaya...maana yake ni kwamba itaendelea kuwa vigumu kwa wenye magari binafsi kubeba wanafunzi kwa kuhofia kuitwa mafataki!

Kaizer,

Kuna nchi HITCHHIKING au Autostop ni MARUFUKU. Wanatengeneza utaratibu ili iweze kujulikana nani anambeba nani. Hii huondoa utata hapo mbeleni kwamba baba fulani anatumia watoto wa shule kwani kwa utaratibu huo, anapangiwa watoto na watu wazima. Na zinaweza kuwepo kadi special na scanner na serikali inagharamia ili kila anayebeba au kuingia kwenye gari, anakuwa scanned na anapotoka ku scan tena. Kwa mpango huo, itajulikana fulani siku fulani alikuwa kwenye gari fulani kuanzia saa fulani hadi fulani.

Mbona Maumba aliwatumia watoto wadogo kwa ingawa alikuwa fundi cherehani, je mafundi cherehani wote wamekuwa waovu? Mwanaume mmoja akibaka, basi wanaume wote tukatwe KIFAA CHA KUBAKIA? Au Wanaume wote tuondolewe karibu na watoto wa Kike? Watu kama hawa siku zote walikuwepo, wapo na wataedela kuwepo. Ni sehemu ya jamii na lazima kusolve tatizo na watu watakaotaka kusaidia kubeba watoto/watu wazima kwenda mjini basi wafanye hivyo.
Nina wasiwasi inaweza kuwa ni mbinu za wenye daladala kwani wengi wakibeba watu basi soko lao linaweza kuanza kuwa katika hali ngumu. Haya mambo inabidi kuyafanyia uchambuzi mzuri na migambo imara kabla ya kuanza. Ndiyo hiki tunasema Kikwete anaogopa kufanya mambo siyo popular. Ni kujaribu tu ingawa hakuna uhakika kama utafanikiwa. Usipojaribu, amini usiamini utakuwa siku zote palepale.

Mkuu,, in a normative perspective, hilo linawezekana, na limewezekana kwa wenzetu. Sisi hatuna hata vitambulisho vya utaifa,, hatujulikani tunakaa wapi kwa maana ya physical address..unaweza kupima mwenyewe tunahitaji muda kiasi gani kufika huko....
 
Kaizer,
Kwa Dar es Salaam hili swala husemi ukweli. Mbona wanafunzi wote wana vitambulisho? Sasa kujua fulani anabeba wanafunzi fulani kila siku itakuwa shida? Au wafanyakazi wa serikali kujua data zao ni shida? Ina mana Tanzania hakuna vitabulisho? Kama kuna vitambulisho, vinatumika na kuheshimika au tunaviona kama ni vitu vya kutengeneza?

Bado naona kuwa, mtu binafsi kwa kupewa baraka na serikali, anaweza kutengeneza kadi/kitambulisho kwa madreva wote wanaobeba watu wa namna hiyo na pia abiria wote wakapewa vitambulisho hivyo. Na serikali inaweza kwa asilimia fulani kusaidia kuchangia gharama za zoezi hilo zima. Mwisho wa siku, wananchi watakuwa happy na serikali kuwajibika kwa RAIA WAKE.
 
Back
Top Bottom