Oral interview nssf

Status
Not open for further replies.
tanzania sasa hivi kuna udini sana zamani ilikuwa ukabila mara wachaga,wahaya,wanyakwisa. Leo uislam na ukristo. Waislam wanadini yao na wakristo wanadini yao hivi tatizo nini....

Watu wana uelewa finyu Brother!! Tumshukuru M/Mungu tuu watanzania tunakaa pamoja mkristo na muislam wanapiga story, wanakaa nyumba moja bila kuhitilafiana tofauti na Nchi nyingine Kaka!!
Hata mimi Brother huwa nashindwa kuelewa, kama mtu ni Muislam anafanya kazi zake vizuri, anashirikiana vizuri na mwenzake pia uislam wake hauna madhara kwa mkristo tatizo ni nini????
Hata kama mtu ni Mkristo anafanya kazi vizuri naye anshirikiana vizuri na wenzake na ukristo wake hauna madhara kwa Muislam shida iko wapi??
KILA MTU ANA UMUHIMU WAKE AWE MKRISTO, MUISLAM au MPAGANI!!
 
Akina Juma, Mwinyi, Issa, Abdallah, Amina, Ramadhan, Abdulrahman, Zainabu, and the like walishaitwa lakini sio sisi akina John, Mathew, Esther, Hellen and the like.

Acha kuwa na mawazo Mgando wewe!!
Usiwe na akili za kushikiwa!!
kwani pale wameambiwa waaply akina Juma, Mwinyi, Issa, Abdallah, Amina, Ramadhan, Abdulrahman na Zainabu??
Kwa hiyo pale akina John, Mathew, Esther, Hellen hawapo??????
Unavyoongea jaribu kuwa na full data sio unaropoka ropoka tuu kama uko kijiweni!!
 
mh, endelea kusubiri, ila endelea kuapply kwingine. ukiona kimya kimezidi ujue wamekuweka kando.
 
Nani asiyejua ya kwamba NSSF kuna udini humu? Pole kwa kukumbuka shuka asubuhi...Dau kaiharibu NSSF tena sana hilo halipingiki wandugu.
 
Acheni kupandikiza mbegu ya udini na fanyeni research kwa myasemayo nyinyi kama wasomi msipayuke kwa kusikiliza maneno ya vijiwe kama nini wewe panda benjamin mkapa ukaangaalie idadi ya hao unaosema ni wengi then ndo ukoment ,kama huna sema tukupe data za tanzania nzima then ulinganishe kama hutofunga koromeo lako ukafyata mkia .tukianza kubaguana kwa dini mzizi wake hautoishia hapa mpaka jinsia tutabaguana ndugu wa tumbo moja .
 
Nani asiyejua ya kwamba NSSF kuna udini humu? Pole kwa kukumbuka shuka asubuhi...Dau kaiharibu NSSF tena sana hilo halipingiki wandugu.

Kwani hii ndio mara yako ya kwanza kuomba kazi? Huko ulipoomba kabla ya nssf ulikosa kwa sababu ya dini yako?
 
Jamani acheni Unafiki na chuki binafsi! Wote mnaolalamika mlishaomba sehem nyingi na hamkupata ajira ama hamkuitwa kabisa kwenye interview, je, ilikuwa ni kwa sababu ya dini zenu? Kwanini iwe nongwa kwa NSSF? Mnataka muonewe huruma kwa kulalamika? Acheni uvivu wa kufikiri! Cha ajabu nchi ya Tanzania, wasomi ndio wanaolalamika kwa kutopata ajira huku wakiwa na elimu. Wasio wasomi wanajishughulisha na ndio walipa kodi wakubwa! Kaeni chini,. Tumieni elimu mliopata ku innovate ideas ili muweze kujiajiri na kuajiri wengine ili tuweze kusonga mbele!
 
ndugu MNYIHANZU ukikaa na udini wako karne hii hutoki coz utashindwa kuomba makampuni kibao eti kisa kuna waislamu.badilika twende kaka.
 
Akina Juma, Mwinyi, Issa, Abdallah, Amina, Ramadhan, Abdulrahman, Zainabu, and the like walishaitwa lakini sio sisi akina John, Mathew, Esther, Hellen and the like.

Unaonekana huna hata qualities za kufanya kazi kwenye public offices! Nenda kijijini ukalime, then uuze mazao, uone kama watakaonunua kama watakuuliza wewe muuzaji ni wa dini gani! Utapata pesa za wakristo, islam, pagans, hindus etc,...
 
Nafikiri ktk vigezo vilivyotajwa dini haikuwemo hivyo suala la kuitwa Ally na Haruna sio shida sana kwangu la msingi wawe na vigezo jaribu kuangalia na sekta nyingine km TRA na kwingineko sio udini kuuona nssf tu!ujui ulisemalo mkuu

nssf udini opo sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom