Optoelectronics knowledge…

Kilongwe

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
423
115
Umuhimu wa optical fiber technology
Leo nivizuri tukakumbushana kidogo juu ya fiber optics pamoja na umuhimu wake
Fiber optics - Ni glass iliyonyumbuliwa yenye wembamba kama unywele wa binaadamu
Ina uweza wa kubeba “300 bilion bits of information per second”
Kazi ya fiber optics kwenye mawasiliano ni kusafirisha optical signal kwa kutumia physic’s law inayosema “total internal reflection” Kwa wale waliopitia physic wataikumbuka hii law.
Hivyo badala ya kutumia “copper wire” sasa tunatumia” fiber optics” kusafirishia habari zetu kwenye mfumo wa “light beam” wakati zamani tulikuwa tunasafirisha habari zetu kwenye “copper wire” ktk mfumo wa electrical signal
Kwa nini tunatumia optical fiber
Kutokana na life style ya leo kumetokea mapinduzi ya habari kwa kiwango kikubwa sana kupita maelezo !! hivyo basi mwanaadamu anahitaji kupata habari kwa haraka sana na kwa kiwango kikubwa kwa mfano anahitaji music, picha, video, hivyo ili uweze kubeba information kwa wingi lazima utumie carrier yenye frequency kubwa sana ,
Tukumbuke kuwa hizi carrier zinapatikana kwenye “ electromagnetic spectrum” zipo kwenye kiwango tofauti za frequency kuanzia Radio frequency(RF) , microwave, infrared, visible light, ultraviolet etc
Hivyo basi infrared na visible light zinauwezo mkubwa wa kubeba hizi habarii zetu na kusafirisha kwa kutumia fiber optics
Hapo ndio tulipofikia sasa kusafirisha habari zetu kwa kutumia infrared and visible light kama carrier za kusafirishia habari zetu kwa kupitia njia ya fiber optics, kwahiyo fiber optics ni kama barabara ya kupita au bomba la kupitisha maji
Kwa upande wa medical diognasis
Fiber optics hutumika kwa kufanyia examination ya inner part s of organ kwa kuchukua picha kutoka sehemu za ndani ya mwanadamu kwa mfano kupata picha ya utumbo kwa vile fiber optics ni nyembamba sana , huwekwa kwenye vifaa vinavyoitwa endoscopes
Kuna endoscopes za aina nyingi hivi sasa zinatumia hii fiber optics pia sasa tunaweza kujua digestive system ya mwanadamu kwa kutumia technologia ya optics fiber. Tunaweza kupata picha ya system yako yote na kugundua kama kunamatatizo

Fiber Optics sensor
Unaweza kutumia fiber optics kama ni sensor kwa kutumia moja ya tabia zake kwa mfano
Intensity modulation, Phase, Transmission time, Wavelength pamoja na polarization
Matumizi ya optical fiber kwenye miundombinu - intelligent infrastructure
Fiber optics sensor hutumika kwenye madaraja makubwa kujuwa kama kuna ufa au yanahatarisha usalama kwa kujuwa uwezo wa kuhimili vishindo
Fiber optics sensor pia hutumika kwenye mfumo wa usalama wa ndege kwa mfano sehemu zile zenye joto kubwa sana la mvuke wa engine nakadharika
Hitimisho!
Umuhimu wa elimu ya optics katika taifa letu unahitajika kwa gharama yoyote hatuwezi kuwa kwenye karne ya 21 bila ya maarifa ya optics


Hii mada imetolewa na mmoja wa watanzania ambaye anachukua Shahada ya tatu(PhD) in Optic fiber yeye amejitolea kutuletea mada mbalimbali kuhusu hii technology kwa niaba ya Afroit forums
Kwa original post tembelea Hapa
 
Back
Top Bottom