Opinio Poll: Je, unaunga mkono mgomo wa madaktari?

Je, unaunga mkono mgomo wa madaktari?


  • Total voters
    174
Naunga mkono kwa sababu tangu mwanzo wa mgogoro Serikali haijaonyesha utashi wa kutaka kuumaliza! Wanafanya siasa tu huku wakiamini kuwa huo ni upepo tu utapita!! Yaani usanii na upotashaji umekuwa mwingi mpaka unakera!!!
 
Nchi ya mafara ni mafarA KWELI KWELI , kwani hizo milion 3 ni kitu cha hajabu ? mtu kupata milioni 3 ukikata kodi 30% baki ni mil 2 haya huyu doc akipanga nyumba ni laki 5 baki 1.5 sasa watz hiyo ni pesa ya kuwaonea gere hawa watu mpaka muwangoe meno, mimi nina kiosk changu kariakoo naigiza zaidi ya hizo mara mbili , silipi kodi na maisha naona ni ya kwaida sana. Mheshimiwa anatuambia amewapa laki 8 kata kodi ni laki 6 huyu mtu apange sinza ni laki 3 na daladala na kula anabaki na nini. Alafu umtegemee aje ashike mavi yako siku nzima . Jamani tuwe wakweli
 
oooooh shit! 3.5M? na wanaopokea laki tatu watafanyaje kama hao wanaopokea laki tisa wanagoma? acha uvivu wa kufikiri.!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Madaktari wamegoma for a 'cause". Je unawaunga mkono? Toa maoni yako tafadhali
That is subjective.
Ungeuliza , Je unaunga mkono mgonjwa kukosa huduma kwa vile madaktari wako kwenye mgomo?
Na utapata jibu tofauti kabisa.
 
Naunga mkono mgomo wa MaDR kwa kuwa wanachokipigania si poasho kama wengine wanavyochkulia hii issue,Madaktari wanapigania wananchi kwa ujumla kwani wamechoka kuona watu wanafariki kabla ya siku zao wakati kuna uwezo wa kuokoa maisha yao na hii yote ndio maana wanapigania ili serikali iwajibike kwa kuweka mazingira ya utabibu kuwa bora zaidi kwa kununua madawa yalioquality,mashine kama X Ray,CT Scan kwani ni aibu kwa hospitali za serikali hata baada ya miaka 50 ya uhuru haina vifaa hivyo au kipo kimoja au kibovu na hata kutengeneza serikali inatumia siasa unafika kwa hospital ati unaambiwa huduma ya X ray hakuna kwani ni miezi 6 sasa X Ray ni mbovu sasa hapo mie kama mwananchi wa kipata cha chini nitakwenda wapi hapo nauli ya kufika Hospitalini niliipata kiaina.Jamani kuna umuhimu sana wa huu mgomo ni hii yote ni kuwaamsha serikali watimize ahadi zao na za muhimmu kwa binadamu kwani hii serikali inacheza na maisha ya Watanzania na hawa viongozi hawajaki kwani wao hata Maralia unaambiwa ooh Waziri kaenda India kupima marelia au macho au utasikia kachomwa na mwiba so kaenda kuangalia vipimo zaidi Nje ya nchi so wewe na mie tutaweza?Mfano wa wazi kuwa serikali ya CCm imechoka kuwatumikia wananchi wake ni kwamba hata Dr Steven Ulimboka mwenyewe kasafirishwa nchi za nje kwa kipimo ambacho kingewezekana kabisa so huu ndio ushahidi kwa wale wanaoitetea serikali hii.
Kuhusu ati mahakama ilizuia mgomo hii haina mashiko kwani kwa tanzania hakuna mahakama ni uzushi mtupu kama mahakama iliweza kuzuia Mgomo wa madr inashindwaje kuwahukumu waliouwa wafanyabiashara wale wa madini waliouliwa na akina Zombe hapa ni rushwa tu,pia seriakili inatumie mahakama vibaya kwa kuwashinikiza pasipo kutumia sheria kwa kuwa iliyempa cheo cha Jaji ni huyo huyo Rais kwa maana hiyo lazima alinde ungali wa watoto lkn mtu sijeniambia ati Mahakama za Tanzania zinafuata sheria,Hapa dawa ni katiba mpya kama walivyofanya Kenya Mahakama haingiliani na serikali kama hapa Tanzania.Tunataka Hospitali zote ziwe na mahitaji yote madawa,mashine zote zinazotakiwa kuwepo kwa Hospitali,maji,vyoo vya kisasa,mazingira mazuri na comfortable kwa wagonjwa,wataalamu waliobobea kwa kila fani,wauuguzi wenje kufahamu wajibu wao especially kwa upande wa wazazi i mean wakunga na mambo mengi ambayo ni muhimu.
 
  • Thanks
Reactions: mob
Naunga mkono,

Tena iingie Na Jeshini, ualimu, Mahakama n.k. Mpaka pale pale wabunge nao watakapolipwa viwango sawa Na watumishi wengine
 
moderators hii topic iwekeeni gundi yaani sticky iwepo juu, vile vile napendekeza sheria iwekwe wazi kuwa wale watakaojiandikisha leo wasiruhusiwe kupiga kura.
 
Madaktari wamegoma for a 'cause". Je unawaunga mkono? Toa maoni yako tafadhali

Naunga mkono 100%
Baadhi ya sababu:
i)madaktari (mwajiriwa) anahitaji mazingira bora ya kufanya kazi kwaajili ya usalama (safety) yake na ya anaowahudumia ili kutoa outcome inayotarajiwa.

ii)Mwajiri/Serikali ilishatamka madai yao ni ya halali na inayashughulikia. Sasa kwavile miezi saba imepita bila kushughulikiwa na mazungumzo yakufikia muafaka yamekatika, sioni njia nyingine zaidi ya kugoma.

iii)Kuhusu mshahara; kama mwajiri anaona mwajiriwa anadai nyongeza kubwa asiyostahili; then mwajiri anahaki yakuajiri madaktari wengine (kama wapo) watakaokubali kiwango hicho mwajiri anachoweza kutoa na sio kuendelea kulumbana, vitisho etc. Kwakifupi kama serikali iliona kabisa haiwezi kuwapa hicho kiwango cha mshahara toka miezi saba iliyopita, then ingewaeleza wazi na kuwapa option za wasiotaka wapeleke barua zakuacha kazi, au serikali yenyewe ingewapa barua yakuwaachisha kazi.

iv)Serikali kuwapa vitisho, kukimbilia mahakamani, kuwakamata, au kuwapa ahadi zisizotekelezeka ni uhuni; ni ishara ya kwamba mwajiri hana option yakupata waajiriwa wengine wakufanya kazi hiyo kwa kiwango hicho; na hivyo kutaka kuwashurutisha kufanya kazi bila makubaliano.
 
Naunga mkono, maana kama inawezekana kuwalipa wabunge 351 Million 10 kila mmoja kila mwezi, kuficha billion 300 Uswizi, kusamehe wezi wa EPA, kulipa Richmond Billion 194, inashindikana vipi kuwalipa Madaktari 3.5 million!?
 
Nawaunga mkono.

Hoja zao zina mashiko. Ile MOJA inayopigwa upatu kwa nia ya kupotosha (mishahara) pia nayo ina msingi wa haki. Ni lazima kuomba au kudai maslahi bora kila wakati. Ni bayana Serikali ilikosa nia,utashi na uwajibikaji ktk majadiliano kati yao, mpaka kufikia mgomo wa madaktari II.
 
Shida ya watu humu na hata Bungeni ni mavuvuzela tu.Watu akili za kawaida zinawashinda, Namwomba Rais anijuze ni akili gani hiyo kwa :
  1. mwekezaji kuchukua 96% na nchi ikaachiwa 4 %
  2. mbunge kulipwa mill 10 kwa kazi ipi ?
  3. mswahili tena sio mfanya bihashara kuwa na mabilion ya shilling nchi za nje na wangoa meno unao wanaua watu tu wasio na hatia
  4. Tanzania kuwa na mali asili kibao lakini watu wake mafara tu hata akili ya kufikiri hakuna
  5. hata wanaotetewa nao akili hawana imebaki ya kula ugali na bamia
  6. utawangoa madakatari meno na kucha lkn msongamano wa wagonjwa hospitalini kama watu wapo gerezani
 
Sijawahi kuona nchi ya watu wa ovyo kama watanzania. Ntatoa mfano : walimu wakigoma kuwa hawawezi kufundisha mpaka waboreshewe sehemu za kufundishia ! Rais ataita wazee wa Dar es salaam atatukana walimu kukosa uzalendo watasutwa na atatuma wauaji wake wawangoe meno na kucha mwishowe atasema wanatumwa na Chadema.
Walimu kwa kuwa ni watu wa akli sana watakubali yaishe watasema Liwalo na Liwe na watajikunja waonavyo , sasa angalia matokeo watahiniwa 100,000 watamaliza shule bila kujua kusoma na kuandika , atawaita wazee wa Dar es salaam tena kwanini wanafunzi wamefelishwa , oh walimu watajikunja tena haya kila mtu amepata 100% hapo ****** atashangilia kisomo kimekwenda mbele kwa kasi mpya.
Jamani tusishangae ****** tangu lini akawa Nshomile ? Jadi yake na Fahri yake ni KIUNO
 
Siasa hatari sana. Madai ya Madaktari ni mengi mno na yanamhusu mgonjwa lakini wanasiasa wamekazania tu kwenye mshahara, wananchi yatupasa wakati mwingine tutafakari.
 
naunga mkono kwa sababu madai yao ni ya msingi.tusipumbazwe sana na propaganda za jk na serikali yake wangekuwa wanawajali wananchi wao tusingefika hapa maana uwezo wa kutekeleza yale yanayoombwa na madr wanao.3.5m ndio stahili yao ila kama alivosema katibu wao.madr ni wa2 wazima na ni watz na wanaelewa hali ya nchi hii na nini kinaendelea.walichohitaji ni seriousness ya serikali kwenye kutatua matatizo yaliyoko kwenye mahosp yetu na kuwaboreshea maslahi yao kulingana na kazi wanazofanya nk.
 
Back
Top Bottom