Operesheni wachawi kanda ya ziwa!!!!!!

Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,073
341
Wakati umefika wa kuandaa maandamano makubwa ya kulaani mauaji ya vikongwe na albino ktk ukanda wa magaribi!
Mimi nilifikiri imani hizi zimekwisha lakini kwa mujibu wa BBC kiswahili mauaji ya vikongwe yameanza upya tena na kuwatia wasiwasi wenyeji na wakazi wa maeneo hayo!

Serikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini, vyama vya kiraia na wananchi kwa ujumla tunaomba tushirikiane ili kumaliza tatizo hili!
 
Hii yote ni kwa vile serikali imelala. Mpaka CDM iwashinikize ndio wazinduke na kufanya kazi husika. Tumeona baada ya maandamano ya kanda ya ziwa Rais na serikali yake wanaanza kutekeleza baadhi ya mambo yaliyotajwa kwamba yafanyike. CCM badala ya kuiongoza na kuikumbusha serikali pale inapojisahau wao wamebaki na malumbano na fikra za Urais 2015 basi.
 
Kama ni elimu wamepewa lakin hawaelimiki,kushauriwa wameshauriwa lkn hawazingatii,minaona kwasasa ni bora mkamkodi manyaunyau ili hao wabishi waone timbwili lake.
 
Haya ni matokea ya imani potofu za uchawi ambazo hata viongozi wa ngazi za juu wanaziamini. Kama kiongozi anaamini katika uchawi, vipi kuhusu mimi niliyehuku Kitinku?
 
uchawi upo wala sio imani tu kwa hiyo kinachohitajika tukubaliane kwanza kuwa uchawi upo. kama haupo inatokeaje mtu aliyekufa tuakazika akaonekana baada ya muda fulani akiwa hai . hapo ndio kwenye utata zaidi na kumfanya mtu aliyeona kama mimi hivi itakuwa ngumu maana jamii nyingi zinashuhudia kwa kuuana hakuwezi kuisha kanda ya ziwa maana mimi natoka huko labda hiki kizazi kipotee kije kingine kitendo ambacho ni kingumu sana
 
Back
Top Bottom