OPERESHENI Okoa Kusini ya CHADEMA yashika kasi

Wakati wa ukombozi wa Tanzania ni sasa, kila mmoja awe sehemu ya ukombozi huu kwa kupinga Ufisadi na kuhimiza uwajibikaji katika ngazi zote za mahamuzi.
 
Hivi hawa CHADEMA wataka kuchukua hii nchi 2015? Mbona manakwenda mbali namna hiyo? nilikuwa najua nyie ni ka chama ka kaskazini na ni ka chama ka msimu, sasa sijui huu ni msimu gani?
Wahenga walisemaje? Mdharau mwimba mguu hufanyaje?? Ndiyo yanayowakuta CCM sasa hivi.
 
Mlitika umeeleweka...USA Democratic wanajulikana wao wanatetea tabaka la chini Republican wao wanatetea uchumi mkubwa. CCM utambulisho wake ni wakulima na wafanyakazi; natamani nifahamu CDM utambulisho wenu ni nini?
Utambulisho wa CHADEMA ni DEMOKRASIA NA MAENDELEO. Lipi kati ya maneno hayo mawili ni la kigeni?
 
Ndachuwa; CHADEMA = Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Demokrasia = Utawala wa watu (Umma) na kwa ajili ya watu.
Maendeleo = Kujikwamua kutoka hali duni katika nyanja zote kimaisha kuelekea katika hali bora. Pakiwepo demokrasia ya kweli hakuna anayebaguliwa wala anayefaidi wengine waachwa.

Hii ndiyo tofauti ya CHADEMA na CCM. CCM haipiganii tena maendeleo ya hao wakulima na wafanyakazi Hiki ni chama cha kuwafaidisha na kuwalinda wachache (mafisadi) na adui wao mkubwa ni DEMOKRASIA (tuseme ukweli jamani). Hakuna demokrasia ndani ya CCM namna ya kugombea uongozi (hata wa ndani ya chama); hakuna demokrasia ndani ya CCM katika Tume ya Uchaguzi, jeshi la polisi na sasa hata mahakama.

CHADEMA ina dhamira ya dhati ya kuondoa uozo huu ndani ya nchi hii badala yake kujenga jamii ya kidemokrasia inayotafuta maendeleo ya kweli.
Halafu mdai kabisa na tuition fee!
 
Chadema good job........... Kwa jinsi hiyo chama kitaenea kila kona ya nchi, ndiyo kuleta upinzani wa dhati, kabla ya hapo chama hiki kilikuwa bado hakijaingia kwenye vichwa vya baadhi ya watz, ukisikia kwa kipindi kile cha uchaguzi ndiyo mwisho kabisa mpaka uchaguzi mwingine. Hamkuwa na ofisi yoyote kwa baadhi ya vitongoji, vijiji , kata, tarafa,wilaya hata mkoa. Chama kinasomeka tu mijini,bado vijijini................... Kazi...plant matawi, sera,elimu,hapo hata sisi magamba tutawaelewa.............maana viogozi wetu walishasema vyama vya msimu, ruzuku ikiisha kimya.....
 
Wanatwangwa kote kote.
Kuwachanganya CCM ni kuwashambulia kama nyuki, mpaka wajipange game imeisha.
 
Nabwada siyo kufanya malumbano; Kesho asubuhi tuwe pamoja kwa Shilingi tupate supu. CCM Mtwara haina mpinzani zaidi ya CUF ambao kwa kiasi fulani wanajikongoja kwa kutumia misikiti.

Ukweli hapa Mtwara vyama vinashika nafasi kama ifuatavyo:-
1. CCM 80% wapiga kura
2. CUF 12% wapiga kura
3. NCCR Mageuzi 5%
4. CHADEMA, UDP, TLP, TADEA, NLD, UPDDP, Demokrasia Makini 3%

Bado haujajibu maswali yangu,Jibu hapa hawa uliowadanganya wanaosoma comment zako waujue UWONGO na UKWELI,MAFILÍLI kumbe ukishaandika humu unaenda hapo kwa Shilingi kulipwa Supu.JAMANI HUYO SHÌLINGI ni Mayor wa Manispaa,Unatumika kwa Supu ?,duu pole kaka .
 
Timu ya Nape itakuwa Nungwi na timu ya lukuvi itakuwa mwnakwerekwe! Pia timu ya Wasira itakuwa arumeru, bila ya kusahau timu ya lusinde itakuwa Uamshoni!

Operation vaa Uzalendo choma makanisa!
Hahahahaahahaahahahahaa aisee umenivunja mbavu sana sikutegemea kukutana na kioja kama hiki bila shaka utakuwa mtu wa utani sana duh!
 
makamanda wapo kusini wakijenga msingi. Ni wajibu wetu sasa kuwawezesha ili kuondoa vikwazo vidogo vidogo kama transport, bendera, machapisho ya katiba za nchi na chama, na mengine mengi. Shime mtanzania
 
CCM ilizaliwa,ikakua,ikazeeka na sasa inakufa....2015 ndiyo inazikwa rasmi kwenye nyumba yake ya milele.
 
Good job CDM, but how Zito as one of the greatest kamanda hatumuoni katika hizi harakati?

Angekuwepo Zitto, wananchi angewatoa hofu ishu ya UDINI na UKABILA..... timu iliyoenda iko ukaskazini zaidi!!! Oeresheni angeifanya Zitto na Mnyika pekee, labda ingezaa matunda!!!
 
Good job CDM, but how Zito as one of the greatest kamanda hatumuoni katika hizi harakati?

Wewe umemuona zito tu? mbona wengi tu hawapo? SUGU hayupo, Msingwa, Nyerere, na Natse, na wengineo, huwezi peleka Chama kizima kule na kumbuka hawa jamaa walikuwa Marekani so wanahitaji kupumzika kwa ajiri ya majukumu mengine
 
Wakuu cdm,bado inatakiwa kuwekeza mtaji wa wapiga kura,dom,singida,shy na moro.
 
Back
Top Bottom