Hute
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,537
- 6,458
kuna jamaa nimekutana naye njiani leo hii, ameota minyama kisogoni, kama lile eneo lenye mafuta kisogoni minyama inaota na kulepelepa kisogoni kama inaadondoka vile...nimeshindwa hata kumpa ushauri (kwanza kwasababu alikuwa ombaomba), kama akafanyiwe operation, kwa hela ipi sikuwa nayo ya kumpa yaani nilimwangalia tu na kuogopa...swali langu ni, jambo hili linasababishwa na nini, na je? akifanyiwa operation yakatwe, mle kwenye kovu yanaweza kuota mengine? ...chukua mfano nimeona na kwa watu wengine, mtu ananyoa ndevu halafu mle kwenye kidevu alimonyoa mikovu mikubwa kama minyama mikubwa inaota....tufanye nini ili kuzuia? intatisha...asanteni.