Operation Vua Gamba, Vua Gwanda Vaa Uzalendo ni ya Nape au CCM?

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,612
864
Wanajamvi,

Kwa muda kidogo nimekuwa nikifuatilia jukwaani na kuona au kusikia kuwa katibu mwenezi wa CCM Nape Nauye amezindua operation ijulikanayo kama Vua Gamba, Vaa Uzalendo akiwa mkoa Kagera kwa shughuli za chama.

Kiukweli nilibaki na maswali mengi ambayo naomba wanajamvi akiwepo Nape mnisaidie.

1.0 Ile operation ni ya kichama au ni ya mtu binafsi yaani Nape? Kwa nini? Nifahamuvyo mimi operation kubwa kama hizo ni lazima zifanyike kitaifa au ziwe na sura ya umoja wa kichama na si mtu mmoja mmoja.

Mf. CDM walipozindua operation yao M4C Arusha ilikuwa na sura ya kichama kwa maana maandalizi na hata uzinduzi wake ulilenga kuwajulisha umma nini maana ya M4C n.k

Lakini hilo sijaliona katika operation inayodaiwa kuanzishwa na Nape. Je hili linahalarisha ile kauli ya kuwa Nape anakifanya chama kama mali yake? Anaweza akaamka na kuja na operation yoyote bila ya Mkama au mwenyekiti wake kujua?

2.0 Ikiwa Vua Gamba, Vaa Uzalendo ni operation ya kichama basi itakuwa imekidhalilisha sana Chama Cha Mapinduzi? Kwa nini? Chama cha Mapinduzi ni chama kikongwe hivyo hakiwezi kufanya mambo yake kienyeji namna ile!!!! Kimantiki kama Nape hakutumwa na Chama inapaswa achukuliwe hatua kali ikiwemo karipio la maandishi kwa kufanya mambo kienyeji yaani bila mawasiliano (Networking)

3.0 Hata kama ni programme ya kichama bado CCM itakuwa imekosa ubunifu kwa kuiga kutoka CDM. Kama wao walipaswa kuja na programme tofauti ambayo itakuwa na manufaa kwa chama hasa katika kipindi hiki cha kupigana kubaki madarakani au kuondoka!!!! Mwanzo mbaya unaashiria mwishilizo mbaya.

Naomba nihitimishe kwa kuomba nifahamishwe juu ya sintofahamu ya Vua Gamba, Vua Gwanda Vaa Uzalendo.
 
Natamani Nape aje apite hapa na kutoa majibu juu ya hili.
 
Friends,
Nape is our fellow youth jamani kwa nini tunamsababishia BP na msongo wa mawazo?

Naombeni tumpumzishe midomoni na kumchapa na key boards zetu walau kwa siku 2, 3
 
Friends,
Nape is our fellow youth jamani kwa nini tunamsababishia BP na msongo wa mawazo?

Naombeni tumpumzishe midomoni na kumchapa na key boards zetu walau kwa siku 2, 3

English Learner siyo kwamba anachapwa mdomo, ila nafasi yake ni muhimu sana na hawezi kuepuka hili. Yeye ndiye msemaji wa chama na propaganda aote sasa kuna kipindi tunapenda kufahamu mengi na kuondoa sintofahamu nyingi ikiwemo hii ya Vua Gamba, Vua Gwanda, Vaa uzalendo.
 
According to statement yake, ''Sasa nimekuja kuwashika,hivi karibuni Nitazindua kampeni ya Vua Gamba, Vua Gwanda, Vaa Uzalendo''. So, kampeni ni yake, km ingekuwa ya chama tungejulishwa sinc last week walipokuwa kwn CC.
 
kampeni ya vua gamba, vua gwanda ni ya CCJ na siyo CCM na nape aliizinduaka kama mwanzilishi wa CCJ a.k.a CCK....
 
According to statement yake, ''Sasa nimekuja kuwashika,hivi karibuni Nitazindua kampeni ya Vua Gamba, Vua Gwanda, Vaa Uzalendo''. So, kampeni ni yake, km ingekuwa ya chama tungejulishwa sinc last week walipokuwa kwn CC.

Basi CCM ipo so disorganized maana kampeni kubwa kama ile haiwezi kuwa lunched na mtu individual. Kweli naanza kuamini Nape Nnauye hakitakii chama mema.
 
JK aliwaambia wajibu hoja za upinzani papo kwa papo bila kungoja vikao. ndo anachofanya nape!

According to statement
yake, ''Sasa nimekuja kuwashika,hivi karibuni Nitazindua kampeni ya Vua
Gamba, Vua Gwanda, Vaa Uzalendo''. So, kampeni ni yake, km ingekuwa ya
chama tungejulishwa sinc last week walipokuwa kwn CC.
 
Mi kwanza naendelea kutafakari hili jambo kwa kina. Maana kama ni vua gamba, vua gwanda, vaa uzalendo!! Nape atakuwa ametuthibitishia pasi na shaka kuwa CCM sio wazalendo hata kidog6.

Na itabidi tutafakari tena na tena, kuwa rasilimali zetu (nchi) zinatumiwa vibaya na viongozi wa serikali ya ccm kwa kuwa hawependi taifa lifaidike nazo.

Baba wa taifa alikuwa na uchungu na nchi na rasilimali zake tofauti na hawa.
 
Back
Top Bottom