Operation safisha jiji!

Jidu

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
1,232
754
Leo asubuhu nikipita katika barabara ya Bibi Titi makutano na barabra ya morogoro,kulikuwa na kamata kamata ya ombaomba,nikishuhudia askari wa jiji wakimkamata mama mmoja ombaomba,mama huyo alikuwa analia huku akiomba msaada toka kwa wapita njia kujinasua toka kwa askari hao ambao walimng'ang'ania mpka gari lao likaja likamchukua ndani ya gari hili walisha mkamata mlemave pamoja na baiskeli yake.Nikaingia ndani ya mitaa ya jiji nikakutana na ombaomba wakiendelea na shughuli zao bila wasiwasi. maswali ya kujiuliza ni kwanini wale tu walikuwa kwenye njia kuu ndio wanaondolewa je tunata kuficha nini?au ndio maandalizi ya miaka 50 ili isije onekana kuwa bado kuna ombaomba hapa mjini tokea uhuru?
 
ni muhimu sana hawa watu wakaondelewa wanajisadia hovyo hivyo wahatarisha hali za afya za watu wengine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom