Operation M4C: Moto kuwashwa Kesho Vijibweni Kigamboni

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,973
Salam wadau,
Kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam hasa pande za Kigamboni na maeneo ya jirani, kesho kutakuwa na mkutano wa hadhara utakaofanyika Vijibweni na kuhutubiwa na makamanda kadhaa kutoka Makao Makuu pamoja na majimbo jirani na Kigamboni.

Pamoja na shughuli za kuimarisha Chama lakini pia wananchi watapata fursa ya kuzungumza na viongozi wetu juu ya masuala mbalimbali ya kijamii yanayowasibu yanayohitaji msukumo wa kipekee ili kufanikisha utekelezaji wake. Bila shaka suala la malipo kwa wananchi wanaotakiwa kuhama kupisha mji mpya wa kigamboni na wale wanaotakiwa kuhama kupisha upanuzi wa bandari, ambao kwa bahati mbaya serikali imeshindwa kuwalipa stahiki zao ili wahame yatakuwa ni mojawapo ya mambo yatakayojitokeza, kwani kwa takribani miaka minne wananchi wale wameshindwa kufanya shughuli yoyote ya kimaendeleo wakisubiri kulipwa stahili zao.

Shughuli itaanza saa nane kamili mchana.
 
Tutakuwepo, hilo pick-up tumeliona linamwaga matangazo, nawashauri viongozi yule kijana aliyeshindwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi Wa udiwani na Selemani Mathew, kamwe wasimuache njia, his very very potential for CDM!!!
 
Kamanda yuko pamoja sana na wanakigamboni na hata mkutano huu ameshiriki kwa kiwango kikubwa sana kuufanikisha.
 
Vipi polisi CCM wamewapa kibali au tujiandae na kesho kusikia mauaji mengine?
 
Kamanda Mwita kila la heri una uhakika kibali umepata? Hatutaki kusikia maafa yanayoweza kuepukika

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Safi sana kila la kheri, samahani jamani najua hapa sio sehemu yake, kama kuna mtu ame-copy list ya watu walioweka fedha nje ya nchi (uswiss) naomba ani PM, nilikuwa nimelala nikapitiwa. Please please....
 
Msingi wa maisha ni kufanya kazi, kuepuka siasa za kukata tamaa na kusonga mbele, kushindwa kwangu mimi leo ni changamoto, kwangu mimi nitajitahidi kutengeneza njia kwa ajae asipate ugumu kama nilioupata ktk uchaguzi ule, karibuni kigamboni watz wenzangu. M4C daima
 
Tutakuwepo, hilo pick-up tumeliona linamwaga matangazo, nawashauri viongozi yule kijana aliyeshindwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi Wa udiwani na Selemani Mathew, kamwe wasimuache njia, his very very potential for CDM!!!
kamanda unachekesha sana, naomba mchango wako wa one bag of cement nimalizie ofis ya kata, M4C Daima
 
Kamanda Mwita Maranya,pia msisahau kuzungumzia swala la mafisadi ku-hold maekari maelfu kwa maelfu bila kuendeleza wanaacha mapori tu mfano wa watu wanaocha mapori ni akbaru,mzee chacha(kaanza kuchoma moto wiki iliyopita),Hussein Mwinyi etc tunaomba mlipeleke hili kwa mama tibaijuka hawa watu ndio wanaorudisha nyuma maendeleo maeneo wanayaacha mapori tu bila kuyaendeleza kama hawayaitaji wakate viwanja vyo robo heka wayauze kwa wananchi.
 
tunaomba more evidance
 
Mambo yameshika kasi.
Sasa Kamanda Isaya Charles aliyegombea udiwani katika uchaguzi mdogo wa vijibweni anatoa neno la shukrani kwa wananchi, kwa kura walizompigia.
 
Isaya; Amemuonya waziri magufuli aache ubabe katika mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni. Wananchi watakaohama kupisha ujenzi wa daraja ni lazima walipwe haki zao kikamilifu bila kufanya ujanja ujanja wa kuwadhulumu au kuwapunja.
 
Mambo yameshika kasi.
Sasa Kamanda Isaya Charles aliyegombea udiwani katika uchaguzi mdogo wa vijibweni anatoa neno la shukrani kwa wananchi, kwa kura walizompigia.

Tunashukuru sana Mwita endelea kutupa updates! Ni viongozi gani wamehudhuria?
 
Kamanda Stephano mwanasheria kitaaluma ametoa salamu za peoples power kwa askari polisi wanaolala kwenye vijumba vya hovyo na visivyo na thamani lakini wanakubali kutumiwa na ccm kuwapiga raia wasio na hatia risasi za moto na kuwalipua mabomu na hatimaye kuwaua!
 
Back
Top Bottom