Operation Chaos: Lowassa, Chenge, Rostam et al; Don't Quit CCM!

Tuliyaona haya na kujua yanakuja.

Uzuri au ubaya wa Kikwete, unaweza kumsoma kama kitabu kutokana na asili yake.

********************************************************************

https://www.jamiiforums.com/tanzania-2010-2015/78626-ushindi-wa-kikwete-2010-shubiri-kwa-ccm.html

UCHAGUZI 2010: USHINDI WA JAKAYA KIKWETE, SHUBIRI KWA CCM

Mwaka 2005 wakati Jakaya Mrisho Kikwete akiwania kuwa Rais wa Nne wa Tanzania, aliendesha kampeni za ndani ya CCM kwa hila, mbinu na njia ambazo zilimpa ushindi ndani ya CCM na baadaye kuwa Rais wa awamu ya nne.

Hila, mbinu na njia alizotumia, japo ziliwapa baadhi ya watu na wafuatialiaji wa siasa matumaini makubwa, pia ziliwaumiza na kuwaangamiza wengi ndani na nje ya CCM katika mpito wake kufikia nafasi hiyo. Kuna wachache kama akina S. A. Salim, F.T. Sumaye, J.S. Malecela, P.J. Mangula, na hata B. W. Mkapa ambao bado wanauguza majeraha ya huo msuguano wa kugombea kuteuliwa ndani ya CCM.

Ikumbukwe kuwa B.W. Mkapa hakuwa mgombea mwaka 2005, bali alikuwa ni Mwenyekiti Taifa wa CCM na Rais anayemaliza muda wake, baada ya kupitishwa dhidi ya Kikwete mwaka 1995 kwa nguvu za Mwalimu Nyerere. Hilo halikuwa rahisi kwa Kikwete kulimeza na kamwe hakutaka kumpa Mkapa nafasi nyingine ya kummaliza 2005, hivyo ilikuwa wazi kuwa Kikwete asingependa au kuacha Mkapa awe na the last laugh. Kama wanavyosema waswahili ‘piga, ua' Kikwete na mtandao wake walidhamiria na kuutaka u-Rais kwa udi na uvumba (literally!!), na hatimaye waliupata.

Kwa mantiki hiyo basi utaona kuwa mvutano na mvurugano uliokuwepo 2005, na kuzidi kupaliliwa na kukuzwa katika kipindi cha miaka 5 kuelekea uchaguzi wa 2010, kunaiweka CCM katika daraja bovu juu ya mto wenye mamba. Wakati wa u-Rais wa Kikwete 2005 – 2010 alitumia na anaendelea kutumia muda mwingi kuhakikisha kuwa maadui wake wa ndani ya CCM wanamalizwa kimya kimya na kufutiliwa mbali kwenye siasa za kitaifa. Viongozi kama Mangula, Salim, Sumaye, Malecela, J.J. Mungai, P. Kimiti, C.M. Mzindakaya, C.D. Msuya, J.S. Warioba, J. Butiku, marehemu Lawrence W. Gama, Mzee P.M. Ndejembi, C.N. Keenja na wengineo waliokuwa na msimamo kama wao walianza kukandamizwa kidogo kidogo na hatimaye kumalizwa kabisa ndani ya CCM ili Kikwete na kundi lake wazidi kujiimarisha.

Kuna wengine kama akina M.J. Mwandosya, S.J. Sitta, A.M. Diallo, W.V. Lukuvi na wengine ambao walipona msukosuko huo na kuzidi kujiimarisha kwa nguvu zao, bali hata hivyo hali zao ni tete na wanategemea kudra za Kikwete na mtandao wake.

Ukisogeza miaka na kuja mbele hadi 2010, utaona kuwa mtandao wa 2005 upo kwa vipande pande na nguvu za Kikwete kama Rais na kama Mwenyekiti Taifa wa CCM, zinasuasua kiasi kwamba sasa yeye Kikwete ndiyo anategemea ukombozi wa maadui zake na kudra za mtandao-mafisadi kama akina R.A. Aziz, A. J. Chenge, A.R. Kinana, N.M. Karamagi, E.N. Lowassa, B.P. Mramba, L.K. Masha, na viongozi wapofu wa maadili kama akina Y.M. Makamba (aka Baba January), K.N. Mwiru, R.M. Chegeni, E.J. Nchimbi, J.A. Msekela, P.J. Serukamba, S.M. Simba, na hasa hasa ‘nguvu' za mke wake Salma, wanae Ridhiwani na Miraji, na ‘nguvu za ziada' kutoka kwa wanajimu na wana-sayansi anga.

Vile vile kuna wale wengine ambao hawajui kama walie ama wacheke kama akina C.O. Ole-Sendeka, A.M. Kilango-Malecela, H.G. Mwakyembe, J.D. Lembeli na wengineo ambao aidha kwa nyakati tofauti walijitokeza ‘kumsugua' vibaya Kikwete na sasa wanahitaji kudra zake ili nao ubwabwa wao usitiwe mchanga.

Kwa maana hiyo basi CCM imekuwa si Kikwete tu, ila vile vile CCM haina njia isipokuwa Kikwete. Hapa kuna maana gani?

Kwa mantiki ya kawaida, CCM kama chama kingembeba mgombea wake kwa hali na mali ili kumuuza kwa wapiga kura, kwa maana kuwa CCM si Kikwete tu bali iwe ye yote yule, CCM ingemnadi kwa nguvu zote.

Hata hivyo, kwa kuwa Kikwete kawamaliza maliza wale wote waliosuguana naye mabega kuanzia 1995 hadi sasa, na wachache waliopo wanaogopwa kumalizwa pia, basi CCM inajikuta haina mtu tena wa kumnadi isipokuwa Kikwete tu. Hata kama CCM watakaa pembeni na kuwaacha Baba, Mama na watoto wakichanja mbuga peke yao, mwisho wa yote CCM itabidi ikubali tu kuwa Kikwete na mizigo yake ndiyo CCM hiyo. Hawawezi kumpinga na hawawezi kumbeba.

Je, ni nini hatima ya haya yote?

Kuna uwezekano mkubwa kuwa uchaguzi wa 2010 Jakaya Mrisho Kikwete atashinda tena na kuwa Rais kwa miaka mingine 5, na muhimu zaidi ni kuwa atakuwa tena Mwenyekiti Taifa CCM kwa miaka mingine 5, kutokana na utaratibu wa CCM wa kuachiana hadi amalize muda wake. Kwa wataotaka kinga zake watasali na kupiga dua kuwa aendelee na katiba ibadilishwe aweze kupata muhula mwingine. Hizo sala na dua hazitafanikiwa. Kwa wale adui zake ndani ya CCM watasali na kupiga dua kuwa asimalize hata hii awamu ya 2010 – 2015, kwani wanajua kuwa watamalizwa ki-kweli kweli ndani ya CCM. Kama ikitokea kuwa hatamaliza 2010 – 2015, hayo yatakuwa mapenzi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa.

Ila kilicho wazi ni kuwa Kikwete aliyejeruhiwa 1995 si sawa na Kikwete aliyejeruhiwa 2005. Kikwete wa 1995 hakua anajua utamu wa Ikulu na vipambio viambatanavyo na u-Rais. 1995 aliambiwa wewe bado ‘mtoto' kaa pembeni wakubwa wafanye kazi. Akakaa pembeni kwa hasira. Kikwete wa 2005 amekwisha onja utamu wa Ikulu kwa miaka 5, na sasa anaona kuna watu wanataka ayakose hayo yote, kuwa wanamwambia hawezi kazi. Hasira za 1995 changanya na 2005.

Ikiwa Kikwete wa 1995 aliweza kuwashughulikia na kuwamaliza hadi kuwa vipande vipande wale wote waliompinga, kumkejeli na kumdharau wakati ‘hajaukwaa', nachelea kufikiri kile ambacho Kikwete wa 2005 atakachofanya mara tu akichoropoka katika hali hii na kurudi Ikulu na Uenyekiti Taifa CCM. Ya Babu Seya yatakuwa nafuu.

Tukumbuke kuwa kufura kwake kwa sasa kunakolezwa pia na Mama na wana haswa Ridhiwani ambaye ni rubani msaidizi, ambao mwanzoni hawakuwa na hili wala lile katika ‘kazi za baba', ila sasa wanaona kuwa mustakabali wao wa maisha unatishiwa.

Kwa mtazamo huo, ni wazi basi ushindi wa Jakaya Mrisho Kikwete 2010 ni shubiri kwa CCM. 2010 CCM wanacheza lizombe juu ya daraja bovu na chini kuna mto wenye mamba.

Wenye macho na tuangalie.
*************************************************************************************
 
well put MMM...Go go go mapacha watatu

Samora10 sidhani kuwa hawa wa3 tu ndo wameifikisha TZ hapa tulipo. Rejea updated list of shame na pitia involvement ya kila mmoja.
Playmaker Ronaldinho Gaucho aliondoka Barcelona lkn Barcelona ikazidi kutisha zaidi.
 
So far there is no evidence whatsoever put forth by the ruling party that you are the most corrupt members of the part. No one has accused you publicly or has even claimed that there is enough evidence to warrant your removal from the party. At least the Mwakyembe's report had some resemblance of credible allegations especially againt EL and RA but not this so called "skin shedding".

For this reason, I believe you will do your part and your supporters a huge favor and justice by not resigning from any party position and as a matter of fact any measure that will be taken against you should be met with a forceful and precise response.

They have failed to even name you in their public report of the party, they failed to level any credible allegation beside saying "these people have been named by a number of citizen and media that they are involved in corruption".

If you agree to resign you will infact prove without any doubt that you are the most corrupt CCM members ever! By resigning or quitting the party the allegations that have been on your tails for sometimes now will need no further proof. You will go down in history as the most corrupt public officials ever to have hold power.

Are you? Well CCM believes that you are to warrant the resignation of both the Central Committee and the Secretariat. If you resign or quit within the 90 days the answer will be in the affirmative.

I know for sure one thing after 90 days CCM will not do anything against you and still remain credible. They can't fire you, they can't just take your party membership without due quasi judicial course within the part as outlined in the CCM's own constitution or the Principles of Ethics guideline.

So.. stay put, enjoy your position, work like ever before and don't mind the new CCM leadership. They can't do a damn thing.
Mwanakijiji,

Nguvu zoooooooote na matambo yoooote waliyonayo hawa mapacha watatu yanatokana na backup kutoka top! Leo hii hiyo backup ikiondolewa hawa mapacha watakufa (kisiasa)! Ona orodha yao:

Chenge: Huyu sihitaji kueleza chochote kwani kitanzi kimeshafungwa shingoni.. ni kiasi cha kukivuta tu. Swala lake la corruption kwenye rada lipo wazi mno, kuanzia takukuru hadi UWT... ni backup kutoka top tu imekuwa inamsaidia.

Aziz: Huyu ndio kabisaa ma-file ya madhambi yake yanajaza lori la tani saba huko UWT

Lowassa:

Labda hapa uta-argue kama wana JF wengi kuwa hawa mapacha wana siri nyingi moyoni na wakiamua kuzifunua JK amekwisha..? Sidhani..

kuna issues zinazoendelea background zinanifanya niamini hatima ya hawa jamaa ipo mikononi mwa JK... Tena nakuhakikishia inabidi wakae kimya maana wakijaribu kuleta fyoko moto utakaowaunguza ni kama ule wa welding...
 
Msijidanganye..

Hawawezi wakashindana na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa CCM ndani ya vikao vya chama ambacho wajumbe wake future yao ya kisiasa inaweza ikavurugwa kabisa kama watampinga Mwenyekiti, na ukizingatia pia hawatapata baraka za kamati ya wazee ambayo wajumbe wake wengi hawapo pamoja nao.

Huu mpira upo kwa JK, akiamua anaweza akafanya chochote anachotaka kwa hawa mapacha bila kizingiti chochote ndani ya chama na kisha kuwa shujaa kwa wananchi.
 
Mkuu;

Uchonganishi huo . . . LOL

What is going behind the Curtains now is believed kuwa Mkuu wa Kaya anawabembeleza jamaa waishe.

Inasemekana jamaa "Pembe tatu pacha" aka RACHEL wana kete muhimu sana za kummaliza Mkulu.

Kama ni kweli, it remains to be seen. Time will tell. Time. timex.

Respect.

I liked the post but expected more from the Superman.You could have done a great service to our nation by not speaking in parables.Najua mkuu una certain facts.Unless ni data zinazohitaji kuhifadhiwa kwa sasa,basi tumwagie hadharani.

Njia pekee ya kumsulubu kibaka ni kuendelea kumpa kipigo anapoanguka
 
Mkuu, soma habari vizuri. Sidhani kama kuna mtu kaoshwa hapo. Watu wameambiwa wafanye maamuzi, ambayo matokeo yake, kwa uamuzi wowote ule, yatakuwa na athari kwa ccm.

DINGSWAYO; Nakubaliana na nawe kabisa! Mana nikweli hao mafisadi yakiendelea kubaki kwenye chama hapo ndo bazuri wanyukane VIZURI na chama kimeguke na ndoto zitimie .RIP JK Nyerere
 
Njia pekee Kikwete kama RAis anayo ya kuwashughulikia ni kuwafikisha mahakamani. Hilo hawezi na sidhani kama ana uthubutu huo akamaanisha hivyo. Kama Mwenyekiti wa CCM hana nguvu yoyote zaidi ya kushawishi wajumbe tu kwa kutumia kofia ya Urais. Ndio maana wazo la kutenganisha ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Chama ni wazo zuri.

Jamani, watu hamjiuulizi taarifa iliyotolewa na NEC haikutaja hata tuhuma au kusema kuna mtu kapewa karipio. Na hilo tamko halikusema hata hizo siku 90! Haya ya siku tisini tumeyasikia kwenye majukwaa tu hakuna mahali popote yameandikwa au kuelezewa.

Wakiondoka CCM itakuwa ni sababu ya woga. Sidhani kama hawa jamaa wana hizo genes.
 
So far there is no evidence whatsoever put forth by the ruling party that you are the most corrupt members of the part. No one has accused you publicly or has even claimed that there is enough evidence to warrant your removal from the party. At least the Mwakyembe's report had some resemblance of credible allegations especially againt EL and RA but not this so called "skin shedding".

For this reason, I believe you will do your part and your supporters a huge favor and justice by not resigning from any party position and as a matter of fact any measure that will be taken against you should be met with a forceful and precise response.

They have failed to even name you in their public report of the party, they failed to level any credible allegation beside saying "these people have been named by a number of citizen and media that they are involved in corruption".

If you agree to resign you will infact prove without any doubt that you are the most corrupt CCM members ever! By resigning or quitting the party the allegations that have been on your tails for sometimes now will need no further proof. You will go down in history as the most corrupt public officials ever to have hold power.

Are you? Well CCM believes that you are to warrant the resignation of both the Central Committee and the Secretariat. If you resign or quit within the 90 days the answer will be in the affirmative.

I know for sure one thing after 90 days CCM will not do anything against you and still remain credible. They can't fire you, they can't just take your party membership without due quasi judicial course within the part as outlined in the CCM's own constitution or the Principles of Ethics guideline.

So.. stay put, enjoy your position, work like ever before and don't mind the new CCM leadership. They can't do a damn thing.

So.. stay put, enjoy your position, work like ever before and expediate UFISADI and don't mind the new CCM leadership. They can't do a damn thing BECAUSE THEY ALL AND THE CCM PARTY BENEFIT FROM YOUR UFISADI PRACTICE
 
Acheni spinning, hao jamaa hata uwaoshe na sabuni gani hawasafishiki!

hujamwelewa mwanakijiji,.anasema ni vizuri wabaki kwenye chama,..wewe huoni kuwa wanachafua chama na wakiondoka ccm watasema ni wasafi sasa,.naikubali hija ya mwanakjj,..hawa watu ni turufu muhimu ya CDM kuisakama ccm ingawaje na kikwete naye ni tururfu muhimu tu,..ccm wagejua wangemvua jk gamba kwani naye yupo kwny list of shame part one and part two ya tabora
 
I liked the post but expected more from the Superman.You could have done a great service to our nation by not speaking in parables.Najua mkuu una certain facts.Unless ni data zinazohitaji kuhifadhiwa kwa sasa,basi tumwagie hadharani.

Njia pekee ya kumsulubu kibaka ni kuendelea kumpa kipigo anapoanguka

Kamanda Mlalahoi;

No facts; no rights to speak, ndo maana niko kimya!

Inasemekana kuna bomu litalipuka siku si nyingi toka kwa hawa kina RACHEL. Sasa Mzee wa Kaya anajaribu kwa kila hali kuwa karibu na EL ili kumaliza tofauti. This remains to be seen. Maana habari nyingine zinasema Wakulu wastaafu wamemwambia Mkuu wa kaya awatose.

Mistake aliyoifanya JK ni mwaka jana wakati wa kampeni . . . . ilikuwa awatose huko lakini sasa ni ngumu. Sasa leo anawatumia akina Nape; Chiligati na Mukama waseme ili kusudi yeye asionekane mbaya kwa hawa kina RACHEL. Pia kuna nyeti zinasema Mkuu wa Kaya yuko radhi kumtosa AC wakati wowote lakini kwa kuwa amejipachika kwa hawa jamaa wawili inakuwa ngumu.

Mzee Mzima aliambiwa wakati wa Richmond kuwa hii kampuni sio Genuine na akapewa data zote lakini EL akaenda kwa haraka sana kumsakizia Msabaha kwa sababu kuwa anacheewasha mchakato na akaingia Mkenge. JK bila hiana akamuondoa Msabaha kwenye Wizara

Kwenye EPA mpaka sasa Mkkulu amekalia Mafile mezani kwake hajayafanyia kazi na data za wezi wote anazo.

Kesi ya ex-Balozi wa Italy Prof. Mahalu inasemekana ni visa binafsi na uwezekano ni mkubwa kwa prof kushinda ile kesi.

Katika mazingira hayo, definetely hii ni Ngoma ya Kikubwa ambayo mkuu wa Kaya inabidi aicheze vizuri.

All in all kama ana nia ya kweli bado uwezo wa kushinda anao in any way.

Peace and Love.

Respect.
 
Wakitoka wanathibitisha kweli wao ni vinara wa mafisadi - yaani kwenye kundi la mafisadi wao ndio wafalme wao!
Wakibakia CCM wanaendeleza kile ambacho tayari watu wanakijua - CCM inakumbatia mafisadi.

Upande mwingine:

CCM ikiwaondoa bila kufuata taratibu za Chama kama zilivyokwenye Katiba yao na kwenye Maadili ya Uongozi Toleo la 2010 wataonekana wamewaonea na kuwa chama kimeamua gia ya kutokea tu bila sababu yoyote ya msingi. Huwezi kwenda na kusema "wanaandikwa sana kwenye magazeti kuwa ni mafisadi" ndio ikawa sababu ya kuwaondoa watu waliokitumia chama kwa muda mrefu na kwa nafasi nzito kama hawa.

CCM ikiwaacha itaoonekana kuwa CCM imeshindwa "kuwang'oa mafisadi"...
 
walipokuwa NEC na CC ya CCM tulisema CCM chafu
sasa wameondoshwa NEC na CC tunawaonea huruma

kesho watahamia CDM wataonekana wapiganaji
 
So far there is no evidence whatsoever put forth by the ruling party that you are the most corrupt members of the part. No one has accused you publicly or has even claimed that there is enough evidence to warrant your removal from the party. At least the Mwakyembe's report had some resemblance of credible allegations especially againt EL and RA but not this so called "skin shedding".

For this reason, I believe you will do your part and your supporters a huge favor and justice by not resigning from any party position and as a matter of fact any measure that will be taken against you should be met with a forceful and precise response.

They have failed to even name you in their public report of the party, they failed to level any credible allegation beside saying "these people have been named by a number of citizen and media that they are involved in corruption".

If you agree to resign you will infact prove without any doubt that you are the most corrupt CCM members ever! By resigning or quitting the party the allegations that have been on your tails for sometimes now will need no further proof. You will go down in history as the most corrupt public officials ever to have hold power.

Are you? Well CCM believes that you are to warrant the resignation of both the Central Committee and the Secretariat. If you resign or quit within the 90 days the answer will be in the affirmative.

I know for sure one thing after 90 days CCM will not do anything against you and still remain credible. They can't fire you, they can't just take your party membership without due quasi judicial course within the part as outlined in the CCM's own constitution or the Principles of Ethics guideline.

So.. stay put, enjoy your position, work like ever before and don't mind the new CCM leadership. They can't do a damn thing.

Afterall it was comrade RA who enabled CCM to score a landslide victory in the 2005 general elections. I hope Nape Nnauye with his wide mouth hasn't forgotten this. Let those who are shouting threats and insults to these noble men stop forthwith for the sake of peace and stability in our goal of establishing and consolidating our new and well thought 'cassino capitalism'.
 
Back
Top Bottom