Elections 2010 Oooh GOD, DONT FORGET TANZANIA

Pax

JF-Expert Member
May 3, 2009
268
87
Nimefuatilia khali ya mambo inavyokwenda wakati tunakaribia kupiga kura nimeona dalili sio nzuri kabisa maana kuna kasoro nyingi mno ambazo ni riskfactors kwa vurugu hapa nchini. Nyingi ya kasoro hizi zimeletwa na tume ya uchaguzi kwa kukosa uwazi na uwajibikaji wa kweli.

Sikuona sababu za msingi kwa nini NEC haikuweka majina kwenye vituo hata miezi miwili kabla ili watu wahakiki majina, majina bandia yaondolewe n.k ili kuweka mazingira ya uwazi na kuaminiana kabla ya upigaji kura.

Siku ya kupiga kura kwa nini haikuwa jumatatu ili watu watumie siku za weekend kusafiri kufuata vituo walivyojiandikishia?

Kila mwanajf aseme maneno haya" Mungu uliye hai, tunafahamu wapo watu hawapendezwi na amani tuliyo nayo, wapo tayari kutumia kila aina ya hila kwa matakwa yao binafsi, tunakuomba ee Mungu uwaangamize kuliko kuliingiza taifa hili katika vurugu, Amen".
 
Back
Top Bottom