Onyo:urembo unaposababisha upofu

Bishanga

JF-Expert Member
Jun 29, 2008
15,323
10,050
yametokea kinondoni,mwanamke kenda kubandika nyusi,msusi kwa ubahili wake badala ya kutumia gundi yake maalum kambandikia superglue,mama kilio,kwenda ccbrt kafanyiwa operesheni ya kutoa gundi,kumbe gundi ilishaharibu macho,kawa kipofu.
Angalizo: kinamama chungeni sana mnapoamua kuongeza makalio,kutia mkorogo,kuongeza nyusi,kurefusha kucha.....na mengine sisemi ni ya siri......
 
halafu kuna wanawake wana ujasiri wa kipuuzi, kubandika nyusi na kuvaa contact lens kwa ajili ya urembo
 
Mtu unajiuliza kinachowafanya dada zetu wajihangaishe kiasi hicho... Unakuta mtu ni mzuri tu lkn kajichakachua weee hadi kawa kama katuni.
 
halafu kuna wanawake wana ujasiri wa kipuuzi, kubandika nyusi na kuvaa contact lens kwa ajili ya urembo

kuvaa contact lens na kuvaa tampons ni vitu ambavyo naona ni majasiri ndio wanaweza kufanya hivyo,mie nawaheshimu sana mie siwezi walahi.....
 
Duh! Lazma watu wajikubali vile walivyo jameni! Mwee! Afu hata huyo alikuwa anamwekea hzo nyusi akamwone mzuri hatakaa amuone tena! Jamani wadada tujikubali vile tulivyo tusalimike!
 
akapandike macho ya mchina! nasikia yapo!

yametokea kinondoni,mwanamke kenda kubandika nyusi,msusi kwa ubahili wake badala ya kutumia gundi yake maalum kambandikia superglue,mama kilio,kwenda ccbrt kafanyiwa operesheni ya kutoa gundi,kumbe gundi ilishaharibu macho,kawa kipofu.
Angalizo: kinamama chungeni sana mnapoamua kuongeza makalio,kutia mkorogo,kuongeza nyusi,kurefusha kucha.....na mengine sisemi ni ya siri......
 
jamani wanawake wenzangu mbona tu wazuri kwa jinsi tulivoumbwa madude yote hayo ya nini!
 
Itakuwa alikuwa anabandika kope,ni urembo mzuri tu wanawake dunia nzima wanabandika tatizo ni sisi wabongo ni wataalam wa kuchakachua kila kitu,amekosa gundi yake special kaamua kutumia super glue kwenye jicho la mwanadamu,Mungu amsaidie tu aweze kupona.
 
Kitu ambacho akina dada kinatusumbua ni kushindwa jisoma... ni kweli kua wanawake wengine ni wazuri saana kuliko wengine, BUT ladies believe me you kila mwanamke ana uzuri wake... Kikubwa hata kama kweli siio mzuri cheza na Mvuto... Mwanamke makini na ukiamua huwezi kosa mvuto; na mvuto ule wakupendeza ni minimal artificiality.... Hebu fikiri mdada una nywele za bandia (which in most cases tunashindwa wengi kukwepa) haya basi kucha - bandia, Kope - bandia, macho - contacts, jamani..... Dah.

Kutafuta mvuto mtu atafute her best feature mwilini, dress the right clothes... Use the right make up, tafuta a perfect hair sytle inaendana na sura yako na inayokuongezea mvuto... Try as much as possible to be asilimia kubwa saana "YOU"
 
Kwa nini mshindwe nywele za bandia?

Anaeweka nywele za bandia hana authority ya kumwambia mtu asiweke kucha au kope za bandia. Vyote ni artificial
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom