Onyo la Hatari ya Njaa Tanzania

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Wadau, nimeona taarifa hii inayohusu onyo la hatari ya njaa inayonyemelea maeneo kadhaa ya Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa hii, ni kuwa serikali tayari imeshapewa taarifa (kwa mara nyengine tena, taarifa imetolewa na vyombo vya nje kwa sababu serikali "ilikuwa haina habari), kwa hivyo isisubiri hadi hali imekuwa mbaya. Tumechoka na kauli za "mipango imo njiani, tumeunda kamati kufanya uchunguzi n.k.
Shirika lisilo la Kiserikali la ACT Alliance limeonya kuwa maeneo kadhaa ya kati na kaskazini mwa Tanzania yako katika hatari ya njaa na kutokuwepo kwa usalama wa chakula.

Kiwango kidogo cha mvua za masika kuliko wastani kumepelekea mavuno hafifu, na kusababisha kupanda kwa be za chakula na upatikanaji mdogo wa vyakula, kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa wiki iliyopita.

"Mikoa tisa ya Tanzania, ambayo ni Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Shinyanga, Dodoma, Iringa, Mwanza, Mara na Tabora, imekubwa na ukosefu na usalama wa chakula kutokana na mavuno haba au kukosekana mavuno kabisa," ripoti hiyo inaeleza. "Bei za chakula zimepanda kwa kiwango kikubwa sana, na kuwaacha watu wasio na uwezo, wakulima, wachungaji na wachuuzi wadogo wadogo kutokuwa na uwezo wa kununua chakula katika kipindi hiki kigumu, cha mwezi wa Juni hadi Disemba 2012."

ACT Forum Tanzania inakadiria kuwa watu milioni 3 wataathirika na mita za ujazo 300,000 za msaada wa chakula lazima zipatikane kwa nusu ya pili ya mwaka 2012.

Kufuatia mawasiliano yake na serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa, ACT imepanga kufanya kampeni ya miezi 12 ya msaada ili kuzuia tatizo hilo, ambayo katika awamu hii ya mwanzo ya miezi sita ni kusambaza chakula kinachohitajika na awamu inayofuatia ya miezi sita ya baada ya tatizo ni kutoa mafunzo yanayohusiana na usalama wa chakula.

Nawasilisha
 
Nadhani hizi ndo habari tunazohitaji,zinasaidia ku broadern mind na kujua utajiwekaje kiusalama zaidi na chakula though my experiance inaonesha wanaohadhirika sana normally na hili swala ni watu wa vijijini ambao wanauza vyakula vyao mapema na wakati mwingine vikiwa bado mashambani,so lesson learn
 
Hili la njaa hakika liko wazi hasa kanda tajwa hapo juu!

Na kwa kuwa tuna serikali DHAIFU yenye kauli hii LIWALO na LIWE ngoja tutaona kauli yao itaishia wapi!

Kama gunia moja ya nafaka jamii ya mahindi haijauzwa Tsh. 150,000/= tukae na tutaona.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom