Onyo kwa wanaume

Bazazi

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
2,806
3,476
Yoshua bin Sira 9:1-9 (Jerusalem Bible).

1. Usimwonee wivu mkeo akaaye kifuani pako,
Ukamfundisha fundisho baya juu yako mwenyewe.
2. Usimpe mwanamke yeyote uhai wako,
Hata azikanyake nguvu zako.
3. Usimlaki mwanamke mgeni,
Usije ukanaswa naye kwa nasibu.
4. Usiambatane na mwanamke aliye malenga,
Ama yamkini utategwa kwa hila zake.
5. Usimkodolee macho msichana,
Ama utatatanishwa katika madai yake.
6. Usiwape Malaya uhai wako,
Usije ukapotewa na urithi wako.
7. Usitazame huko na huko katika njia za mjini,
Wala usitembee ndani yake panapo ukiwa.
8. Jicho lako uligeuze mbali na mwanamke marini,
Wala usikazie macho uzuri wa mwingine.
Wengi wamepotoshwa kwa uzuri wa wanawake,
Na kwa huo ashiki huwashwa kama moto.
9. Usijilisi sebuleni pamoja na yeye aliyeolewa,
Wala usiende mandari naye kwenye mvinyo;
Moyo wako usije ukamgeukia,
Na roho yako ikatelemkia upotevu.


NB:
Mandari = Tafrija.
Malenga = Yeye atafutaye uchumi kwa kuimbia watu.
Marini = -zuri, -a kupendeza.

Jilisi = -keti.
Ashiki = tamaa ya ngono, mapenzi.

 
pana chezeya jicho la mtoto wa kike akiamua kutega!ndo msikie sasa mnayoambiwa na yoshua bin sira,bible bwana ina kila jambo tunalofikiri halikuwapo duniani kabla yetu sisi,nikisoma WIMBO ULIO BORA huwa natafakari sana!
 
Back
Top Bottom