Onyo - Acha mchezo huu mchafu.

Status
Not open for further replies.
kuna huyu memba ambaye anajifanya anajua kila kitu. Naomba kutuma ujumbe wa wazi kabisa. Tafadhali acha! Hili ni onyo la mwisho. Kelele zako za mambo ya siasa zimekubalika na ni kweli zimekutengenezea jina, lakini hili la sasa ni jambo ambalo ni kinyume na uungwana na lina lango moja nalo ni kuwapaka viongozi matope. Nilikuwa naunga mkono mambo ya Mbowe na Slaa kuwekwa hadharani, lakini naona mambo yote ni ya upuuzi. Nawaomba JF tuungane na kuyakataa haya kwani ingawa yana faida kidogo lakini madhara yake ni makubwa zaidi. Naomba kutoa wazo kuwa mada zote zinazohusiana na mambo ya binafsi kama ya kina Slaa, Mbowe, na Mhe. Kikwete au Waziri wetu Mpendwa Lowassa, yapelekwe kwenye udaku au kwingine. Wengine tumejaribu kuwakaribishwa wakubwa wetu ofisini, lakini leo wengi wametoka wakitikisa vichwa vyao. Nawasihi.

Asante.

Hivi MUMEO huko READING anajua kama unaingia humu kisiri siri?
 
Huyu Bi senti 50 akishatoa vitisho huyooo haonekani tena mpaka kesho yake. Inawezekana ndiyo huyo amem email mwanakijiji ku compromise baadaye mwanakijiji amesitisha zoezi kabla wengine hata hatujafaidi hata picha moja.

Sasa si mniwekee kamoja kwenye PM na mimi nijinome?
 
tatizo sio kuweka picha, its a fact kwamba those pics do not EXIST ! un existe no les fotos !
 
Umejumbe umefika crystal, loud and clear... Hili jambo limeshafikia kikomo.

Wacha FIX man, you have nothing! Acheni kutafuta cheap popularity na picha feki!

Na wewe Bi Senti acha UPUUZI wako, kwanini hukumtetea MBOWE na SLAA?, acha sisi tuliopinga mambo binafsi toka mwanzo ndio tuongee! Kazi yako kutetea tu Serikali hata ikiboronga, Come out of the box upate picha kubwa zaidi na uweze kutazama pande zote mbili kwa mapana na marefu.
 
Binti Thumuni umeongea jinsi mawazo yako yanavyokutuma sikulaumu.Ni haki yako ya kimsingi kusema hivyo.Mimi naona tuwe wawazi kama tukisema ya fulani basi tuangalia na upande mwingine wa shilingi.

Ufisadi hauangalii kama wewe ni mrefu,mfupi,mweupemweusi na kada wa chama gani.Wananchi ni lazima tuwafahamu watawala wetu i and out.Bi thumuni kama za Mbowe zipo ziwekwe na kama za muungwana zipo zianikwe vile vile ndio mapinduzi ya kifikra hayo.
 
kuna huyu memba ambaye anajifanya anajua kila kitu. Naomba kutuma ujumbe wa wazi kabisa. Tafadhali acha! Hili ni onyo la mwisho. Kelele zako za mambo ya siasa zimekubalika na ni kweli zimekutengenezea jina, lakini hili la sasa ni jambo ambalo ni kinyume na uungwana na lina lango moja nalo ni kuwapaka viongozi matope. Nilikuwa naunga mkono mambo ya Mbowe na Slaa kuwekwa hadharani, lakini naona mambo yote ni ya upuuzi. Nawaomba JF tuungane na kuyakataa haya kwani ingawa yana faida kidogo lakini madhara yake ni makubwa zaidi. Naomba kutoa wazo kuwa mada zote zinazohusiana na mambo ya binafsi kama ya kina Slaa, Mbowe, na Mhe. Kikwete au Waziri wetu Mpendwa Lowassa, yapelekwe kwenye udaku au kwingine. Wengine tumejaribu kuwakaribishwa wakubwa wetu ofisini, lakini leo wengi wametoka wakitikisa vichwa vyao. Nawasihi.

Asante.
Tutafika namna hii kweli?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom