Online membership registration CHADEMA

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
31,553
37,711
Salaam,

Napenda kutoa ushauri kwa uongozi wa juu wa Chadema kuanzisha Online membership registration, nina uhakika CHADEMA itapata wanachama wengi zaidi kuliko kufuata huu mfumo wa kiasili tuliozoea (Traditional system) ambayo lazima uende physically kwenye ofisi ya tawi then uandikishe kwenye daftari kabla ya kupata hard-copy membership card.

Mi naongelea softcopy membership registration card ambayo naweza kulipia online pia kwa kutumia system zilizowekwa sasa hivi kama M-Pesa or Tigo Pesa. kwa hiyo wale watakao design sytem hii basi wa link na Voda / Tigo Pesa.

Pesa hizi zinaweza kusaidia chama hasa kipindi hiki ambacho chama kinaenda kuwafikia wenzetu wa vijijini. Mwisho naupongeza uongozi mzima wa CHADEMA kukifikisha chama hapa kilipo kwani tayari kinaaminiwa sana na wananchi, Hongera Mwenyekiti, hongera za pekee ziende kwa DR. Slaa mpiganaji numberi one. tupo pamoja kamanda wetu na crew nzima ya wapiganaji - Lissu, Myika, Zitto, Lema, Mdee na wengineo.

Hoja ya msingi ni kwamba watanzania wengi hasa wa mijini ni wavivu sana kwenda kutafuta ni wapi wanapata kadi ukizingatia muda, foleni za barabarani na najukumu waliyonayo. kwa mfano nikiwa hapa kwenye laptop yangu basi naweza kufanya registration na kulipia kadi yangu kwa urahisi sana - pia baada ya hapo naweza kuwa napata updates za chama online kama mwanachama hai wa chama changu.

Mawazo yako ni mazuri mkuu tatizo linaweza kuja kwa wale wenzetu walioko mbali na hii mitandao ambako ndiko kuna wapiga kura wengi namzungumzia watu wa vijijini,lakn kama ukibuniwa utaratibu mzuri zaidi basi naamini huu utakua mpango mzura sana wa kuendeleza chama hiki ambacho kimekua ni mkombozi wa Tz wengi currently maana mchango wako unaonekana ipasavyo
 
mkuu kama umenisoma vizuri mfumo huu utalenga zaidi watu walioko mijini, wale wa vijijini wataendelea na utaratibu ule ule wa zamani, hapa tuna uhakika kupata wanachama wapya wengi sana - kwa mfano Dar es salaam peke yake tunaweza kupata wanachama wapya zaidi ya 10,000 approx. hiyo ni hatua nzuri then mikoa mingine inafuatia.
 
Wazo zuri sana. Pia wanaweza kuoganaizi na mitandao ya simu za mikonon, ambapo registratio inaweza ikafanyika kwa kuandika jina na kutuma kwenye namba fulani
 
Wazo zuri sana. Pia wanaweza kuoganaizi na mitandao ya simu za mikonon, ambapo registratio inaweza ikafanyika kwa kuandika jina na kutuma kwenye namba fulani

wazo zuri, mitandao ya simu haiwezi kukubali kushiriki ktk zoezi lolote la vyama pinzani hasa hasa CDM,watatoa sababu kwa hawashirki mambo ya siasa etc.
ila kampeni ya sisiem walitumia network za simu .
 
Wakati nafungua thread hii nilidhani naweza labda kutakuwa na link ya kujisajili nilitaka nijisajili.Gud idia ai aprishieti
 
Ungekuwa umewahi kujaribu ku register katika mfumo huu huu wa kwenda kiguu na njia ofisi za CHADEMA ukaona ilivyo hustle kuregister uanachama ndio ungejua kwamba kwa teknologia ndio hawawezi kabisaaaaaa...
 
Hii kitu muhimu,nadhani chama kiwe na idara ya ICT ili kuplan strategy mbalimbali online ikiwemo hiyo registration,matangazo,fund raisings na campaign
 
Wazo zuri sana. Pia wanaweza kuoganaizi na mitandao ya simu za mikonon, ambapo registratio inaweza ikafanyika kwa kuandika jina na kutuma kwenye namba fulani
jiwe jeusi unataka kumshirikisha Rostam(vodacom). Think twice
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom