Online Meeting with CHADEMA - Kuimarisha Upinzani na Kuleta Maendeleo - No 1

Good post. Kumbe ni kweli Jf ni ya Chadema. Utaona kila post CDM good. Tuwe kitaifa zaidi. Hii ni kawaida kwa Post za kibongo kushabikia hata jambo lisilo na tija kwa Taifa.
Jf take care. Kuna blog nyingi zimefungwa kwa ajili ya uchochezi. I am sure if you do not change your trend soon or later it will be blocked. I am sure 100%. Bye

Ama kweli wewe hamnazo JF Haitafugwa kamwe na itadumu mpaka mabadiliko ya kweli yapatikane hizi siyo zama za kutishana bana wewe vipi!
 
Mkuu, naukubaliana na wewe 100%

Lakini nasisitiza bado kuwa kiongozi bila uadilifu haina maana yoyote kwa kuwa mabadiliko hayatakuja hata kama watachaguliwa kwa kura nyingi. Itakuwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

Tujifunze kutoka CCM . . . Si wanaendesha serikali sasa? Si walichaguliwa? Ubunge, udiwani, nk. Lakini je kuchaguliwa kwao kumeleta tija yoyote?

UADILIFU UADILIFU UADILIFU na MIKAKATI ndiyo mbinu pekee ya kuleta msukumo. Na hayo CHADEMA inabidi myafanyie kazi.

Of course common sense ni muhimu katika maamuzi, unafikiri Watanzania waliowapigia kura Mafisadi walifahamu kuwa ni mafisadi? Ni nini kifanyike kuwatambua mapema?

Kama nikiamua kujiunga CHADEMA binafsi sitotaka Cheo chochote, nitapenda kuwa mbunifu wa mikakati na kama hilo halikubaliki eti mpaka nigombee katika mitaa, au nafasi nyingine yoyote, then I am sorry to say, wengi mtatukosa bado.

Haya mambo si ya kuongea kwa jazba, tunapenda kuona reasoning, ukisoma post zangu zinajieleza kikamilifu unless kama tunataka kuleta ule ubishi wa kisiasa usio na Tija.

Mwenye macho haambiwi Tazama wala mwenye masikio haambiwi Sikia.

Mkuu nakubaliana nawe katika mambo mengi. Nami nakuomba tuungane sote katika ki-mkakati na ushauri ili CDM ilete ukombozi wa kweli kwa maisha ya mtanzania. Sisi wengine tumekuwa na CDM kimkakati, hata kama si viongozi na wala watu hawajatufahamu vema. Lakini nia ni kuona CDM sasa inwakomboa watanzania. Kama chama,CDM bado inampungufu yake, lakini ni imani yangu kuwa with time, kitakuwa sawa kwa kuwa watakaokiweka sawa ni sisi wenyewe tutakao weka mikakati mizuri. Mimi nashauri tuuungane na CDM na kuomba umma wa watanzania kwa hali ilivyo sasa tuwaunge mkono CDM, tulete mabadiliko huku tukiendelea kusisitiza UADILIFU na NIASAFI ya KUMUKOMBO mtanzania.
 
Toa evidence ya hizo kauli zako kwanza au utakua umetumwa wewe. kwanza hao watu wanaotaka kuingia chama kimasharti hawafai na ikiwa masharti yenyewe sio ya kikatiba, kwanza omba katiba ya chadema then ikikuridhisha ujiunge na sio hizo porojo zako. kujiunga kwa vyama kwanza inaanza na kutunga katiba ambayo itaongoza au kuridhiana na vyama vyote so, ni makubaliano na ili ni ngumu kokote duniani ukizingatia hata hicho chama tawala hakiwezi kwa sababu ya ruzuku zaidi ni kwa serikali kuchuja na kubakiza vichache vyenye nguvu na majimbo mengi au katiba hii tunayoitarajia tolimit vyama aidha mwisho viwe vitatu au viwili kwa idadi ya majimbo iliyotwaa ili kodi zetu zisichezewe


(2. Kuna mambo kadhaa wa kadhaa ya kimsingi yanayohitaji mabadiliko kuhusu CHADEMA kama suala la Ubinafsi, Ukabila, Upendeleo, Ubadhirifu wa pesa nk.)

Tunaitaji ushaidi wa kitaaluma please can you count with evidence? jf sio janvi la bla,bla or ndio propaganda mnazokujanazo hapa jf?
3. Naongeza hapo mlikuja na chadema inavunja amani, chadema inafadhiliwa pesa na mataifa ya nje ili iondewe serikali madarkani, chadema na maandamano so, tueleze na kama wapo hao UWT waeneza uongo watueleze kwa evidence

Magamba wanavyofanya maandamano ya kujisifia kuwa tumejivua magamba! na kutumia msululu wa magari ya kifahari bila kutueleza wananchi kwanini tuu maskini ivi na huu mfumuko wa bei juu kila kukicha, ubadhirifu wa kodi zetu,mikataba ya kuneemesha wachache, vijana kufanya vibaya mashuleni, migomo kila kona dowan+richmond nk embu tujuze na wewe ni vipi chadema walichokosea wao wanaenda kwa raia kuwaelimisha na sasa wamewafungua macho wananchi kuhusu katiba je hao Magamba wanawaelimisha nini wazalendo uko kwenye mikutano yao?

Na sasa Mmefanikiwa kuvibana vyombo vya habari jamani nchi aiendishwi kijinga namna hii
Spika wa bunge na ujinga wake
Magamba kudakia sera za chadema mfano katiba wanasema wao ndio wameanzisha huu mswada wakati wamelazimishwa na ukikumbuka kwenye campaign hii ilikua ni ilani ya chadema wakati Magamba uko ilani yao aikuwepo. mengi na mengi......

Mtoa mada tuache upotoshaji wa mambo na naomba ujibu hoja zangu.

Mkuu;

Hivi umesoma thread kuu na ni ya mwaka gani?

Umesfuatilia posts na mijadala humo ndani?

Unayajua matatizo ya msingi ya CHADEMA pamoja na mazuri yao au unaleta ushabiki tu wa kujitetea kama CCM?

Unajua Marehemu Chacha Wangwe alipigania nini?

Acha ushabiki wa kujifanya hujui matatizo ya kimsingi na kuogopa kujadili masuala magumu. huko si kukua.

Ukiwa na donda ndugu litibu na si kufunga bandage.
 
Mkuu,kama wewe umeona kuna udhaifu fulan katika uongozi wa cdm,ni vizuri ukauweka wazi na ukatoa maoni yako jinsi ya kuutatua na si kuanza kuzunguka.B streight to the point.
 
Wana-CHADEMA mliomo humu, Karibuni katika Thread hii maalumu kwa ajili ya mambo muhimu ambayo tunataka myajibu.

Tunaanza na CHADEMA na tutawapima kutokana na maelezo yenu. Then tutaviita pia vyama vingine katika thread tofauti. So this is KITI MOTO!

Tunajua Mh. Mbowe, Dr. Slaa, Zitto, Mwanyika, nk wote mko humu, so tunataka majibu ya uhakika.

Watanzania tumechoka sana mwekeo wa nchi yetu.

Hakuna wa kututetea kikamilifu ndani ya Chama Tawala . . . .

Upinzani nao bado unasua sua na hauna mwelekeo wa kushika hatamu . . . .

Sasa baadhi ya wana JF na watanzania wengine makini ambo wako nje ya JF kwa hiari yetu tumeamua tunapenda kuona Nchi yetu ikiwa na mabadiliko na maendeleo ya kweli.

Tunapenda kuona mambo ya kimsingi ya kuleta mabadiliko ya kweli yafanyike na ikiwezekana CHADEMA ishike madaraka mwaka 2010 au 2015. Na wengi tuko tayari kuwaunga mkono na kujiandaa kufanya kweli endapo tu mtakidhi matakwa ya watanzania

Kujiridhisha mwanaweza kupitia thread hii kwanza: https://www.jamiiforums.com/complai...jamii-forums-kuwa-chama-tishio-cha-siasa.html

Kwa kuanzia tunaomba mtoe comment katika hili:



Kazi kwenu Wana-CHADEMA
Unaweza kutufafanulia una maan gani ktk hiyo red hapo juu ili tuweze kuchangia ipasavyo?
 
Mkuu;

Hivi umesoma thread kuu na ni ya mwaka gani?

Umesfuatilia posts na mijadala humo ndani?

Unayajua matatizo ya msingi ya CHADEMA pamoja na mazuri yao au unaleta ushabiki tu wa kujitetea kama CCM?

Unajua Marehemu Chacha Wangwe alipigania nini?

Acha ushabiki wa kujifanya hujui matatizo ya kimsingi na kuogopa kujadili masuala magumu. huko si kukua.

Ukiwa na donda ndugu litibu na si kufunga bandage.

Ujanijibu hoja yangu na sijakuelewa unamaanisha nini kwenye thread yako nachoktaka jibu maswali yangu na ushaidi wake sio porojo unazoziweka hapa jf

Mtoa mada sina ushabiki wa chama chochote ila nafuatilia mstakabadhi mzima wa wapiganaji wanaotutetea maslai yetu katika kuiendeleza nchi yetu
 
Mkuu Nono;

Nadhani kiini cha hoja ya msingi bado hujakielewa . . .

Shida si kwa Watu Makini na uwezo mkubwa kujiunga CHADEMA na kupewa Uongozi. Shida ni viongozi wa namna gani wanatakiwa na je ni Waadilifu kiasi cha kuvuta Umma wa Tanzania kuwatambua kuwa wako serious?

Concept ya Watu Makini kuachiwa uongozi si suala jipya na limefanya kazi sana katika Historia ya Mabadiliko ingawa si wote wamefanikiwa kuleta mabadiliko ya kweli. Nyerere alifanya hivyo, CCM wao wana utaratibu wa Kung'atuka na hata kuchukua watu wanaohama Upinzani na kuwapa madaraka, Oliver Tambo alimwachia Nelson Mandela, Mabere Marando alimwachia Mzee wa Kilalacha n.k.

This issue if you look into the positive side, you will understand what I mean. Baadhi ya viongozi wa CHADEMA ambao ndiyo wenye nafasi kubwa ya kuleta Tranformation wamekuwa questioned sana juu ya uadilifu wao, matumizi mabaya ya pesa, upendeleo, na hata kwa baadhi ya maamuzi . . .

For sure these are not about constitution or about election procedures, it is about leadership. Wakati CCM wanaendelea kukumbatia Rushwa na hata Ufisadi, Makundi nk katika Chaguzi zao i.e UVCCM, UWT nk. CHADEMA inatakiwa ijisafishe . . .

Yote hayo kwa Ujumla wake ndiyo yanatakiwa yafanyiwe kazi. Na tunataka commitment yao . . . .

Kwenye huu mchezo wa siasa mtu msafi ni yule ambaye bado hajapata furs ya kuongoza. Once ukipata nafasi hiyo na kufanya maamuzi fulani kila mtu atanza kutafsiri maamuzi hayo kwa mtazamo wake na kushawishi kikundi kikubwa cha watu in the line ya mtazamo wake hata kama mtazamo huo sio sahihi
 
Nilichogundua humu jamvini ni kwamba mtandao mzima umeshatekwa na cdm tofauti na awali.pindi hichi imejaa mashabiki tuu sio kwamba mpo hapa kwa hoja mbadala za maslahi ya taifa ila mko kichama.
 
Mkuu;

Kuna mambo kadhaa wa kadhaa ya kimsingi yanayohitaji mabadiliko kuhusu CHADEMA kama suala la Ubinafsi, Ukabila, Upendeleo, Ubadhirifu wa pesa nk. Tunataka CHADEMA waje hapa kama baadhi ya viongozi watakubali kuyaacha.

Pia kuwe na mfumo ambao hayo mambo hayata ruhusiwa kutokea . . . . Kuna maswali mengi ya kuwauliza. waje tu wasiogope. Waanze na post kuu hapo juu.

Nimekufatilia sana kwenye majibu yako kuhusiana na reply za watu nilichijifunza ni kuwa, kwanza umehama kwenye maada yako ya awali aitha kwa kuvutwa na repliers au kwa kutokujua, maada yako ya awali imeongelea ubinafsi ulioko CDM? Ukabila ulioko CDM? Upendeleo ulioko CDM? au ubadhirifu? Huna lolote wewe GAMBA tu, unaweza kuyadhibitisha haya? kuna sehem umesema mtaanzisha chama chenu, nadhani hilo ndo jema kwako na hao wanaokutuma toka MAGAMBANI.. jiondoeni huko muanzishe chenu
 
Wana-CHADEMA mliomo humu, Karibuni katika Thread hii maalumu kwa ajili ya mambo muhimu ambayo tunataka myajibu.

Tunaanza na CHADEMA na tutawapima kutokana na maelezo yenu. Then tutaviita pia vyama vingine katika thread tofauti. So this is KITI MOTO!

Tunajua Mh. Mbowe, Dr. Slaa, Zitto, Mwanyika, nk wote mko humu, so tunataka majibu ya uhakika.

Watanzania tumechoka sana mwekeo wa nchi yetu.

Hakuna wa kututetea kikamilifu ndani ya Chama Tawala . . . .

Upinzani nao bado unasua sua na hauna mwelekeo wa kushika hatamu . . . .

Sasa baadhi ya wana JF na watanzania wengine makini ambo wako nje ya JF kwa hiari yetu tumeamua tunapenda kuona Nchi yetu ikiwa na mabadiliko na maendeleo ya kweli.

Tunapenda kuona mambo ya kimsingi ya kuleta mabadiliko ya kweli yafanyike na ikiwezekana CHADEMA ishike madaraka mwaka 2010 au 2015. Na wengi tuko tayari kuwaunga mkono na kujiandaa kufanya kweli endapo tu mtakidhi matakwa ya watanzania

Kujiridhisha mwanaweza kupitia thread hii kwanza: https://www.jamiiforums.com/complai...jamii-forums-kuwa-chama-tishio-cha-siasa.html

Kwa kuanzia tunaomba mtoe comment katika hili:



Kazi kwenu Wana-CHADEMA

hamjui hata mda wa kuwataka watu wajibu hoja,people are busy now ,wanatafuta ukombozi mda wakuja JF ni finyu watafuteni baadae,au umetumwa kuvuruga agenda za Arusha.wapelekee pale NMC utapata majbu yenu.
 
hamjui hata mda wa kuwataka watu wajibu hoja,people are busy now ,wanatafuta ukombozi mda wakuja JF ni finyu watafuteni baadae,au umetumwa kuvuruga agenda za Arusha.wapelekee pale NMC utapata majbu yenu.

dunia ni kijiji huitaji kuwa kila sehemu bali unaweza kujiwakilisha kwa kutumia technolojia
 
hamjui hata mda wa kuwataka watu wajibu hoja,people are busy now ,wanatafuta ukombozi mda wakuja JF ni finyu watafuteni baadae,au umetumwa kuvuruga agenda za Arusha.wapelekee pale NMC utapata majbu yenu.
mama hii post ni ya mwaka 2009.
 
Hapa patazuka kama ile maoni iko kusema Kikwete anapendwa , sijaona msukumo wowote ambao unaonyeshwa Chadema ina nguvu ,jamani tusemeni ukweli ,nguvu gani ambazo Chadema inazo,mimi sijaziona kabisa zaidi ya makelele ya kumfukuza mwizi halafu mwizi wenyewe msimpate ,hivi mtakuwa na nguvu hapo ? Na ikitokea habari mwizi amekamatwa nyie hamhusishwi kabisa ,wengine ndio wanajisifu na kujisifia kuwa ndio waliomkamata mwizi.Chadema mnaachwa mnahema na mawe mikononi ,mkiulizwa mnajibu tumemuona...!Mbona hamjamkamata..mnabaki sie ndo wa mwanzo kumwona.

Kwa wakati huu tulionao tusidanganyane ,mimi nasema Chama chochote ambacho kitafanikiwa kuibua hisia za wananchi na kuungana katika kudai Katiba mpya ya Nchi hii ,Chama hicho ndicho kitakachofanikiwa kuwa na nguvu ,Ingawa Chadema wanasema kuwa CHama chao ndio Chenye nguvu lakini ukweli uliopo ni kuwa bado CUF ni Chama nambari mbili Tanzania hilo halina ubishi ,na hili inatokana na kuwa wanachama wa CUF hawafi moyo ,hilo tu,na hiyo ni akiba ya Chama ,wanachama wa CUF wamekaa kama mazezeta ambao msimamo wao haubadiliki,imani waliyo nayo ni kuwa Chaguzi zilizopita wameibiwa kura ,matokeo yamebadilishwa ,hivyo hazina ile ipo pale pale naweza kusema wanachama wa CUF inakuwa kama wanakisasi wanaposhindwa na kila uchaguzi ukija kura yao haibadiliki inakuwepo pale pale ,hiyo ni silaha ambayo Chama cha CUF kinabaki na mhimili ,ona Tambwe ametoka chama lakini hakuna mwanachama ambae umemsikia akimsifu Tambwe kila unaemuuliza anamlaani Tambwe ,ikimaanisha wanachama wa CUF ni wanachama wenye msimamo mkubwa sana usio tetereka.

Mimi huwaga sipendi kubishana sana kuhusu vyama vya upinzani .kwa sababu najua hakuna mpinzani wa kweli wa serikali hii zaidi ya CUF na hakuna Chama kilichotulia kama CUF ,kusema kweli kimevuka mambo mengi ukilinganisha na vyama vingine ,kwa mfano katika uongozi wa Chadema naamini kabisa watu au wananchi wengi hawawatambui wengi zaidi ya Slaa na Mbowe na kidogo Zitto katika uongozi wa Chadema,tuzungumzeni ukweli na tuondoe jazba ,nazungumzia wananchi na sio waishio humu JF na hata humu ndio hivyo hivyo ,mnazungumzia mtandao hivi ni asilimia ngapi ya wapiga kura waTanzania wanauwezo wa kuwepo na kutumia mtandao ,zaidi mtajikuta mnazungushana nyie kwa nyie mtu mmoja ana majina zaidi ya matatu ,mtu huyo huyo mmoja anajivalisha vyama vyote.

Chadema ili kuuteka umma wa Tanzania ni lazima ienee mikoa yote kama ilivyo enea CUF ,maana CUF sio mchezo hakuna kona ya Tz utakayotembelea usiione bendera yake ikipepea ,ni true story wandugu ,ndani vijijini huko makolokoloni utaikuta bendera ya CUF,japo juu ya mti.

Chadema lazima wajitambulishe zaidi ya Slaa na Mbowe ,hivi chama hiki kina viongozi wawili tu ? Viongozi wengine watumike wasikike waonekane wakiandikwa kwenye magazeti ,wapewe hoja nzito kuhutubia wananchi ,hapo itaweza kupiga hatua lakini kujikusanya wapiga debe hapa JF na kurapu ,itakuwa kama mpo stendi ya basi mkisubiri abiria wakati wengine wanakusanya abiria kwa njia za mkato wala hawaikaribii stendi.





Mkuu sikubaliani na ww kitu kimoja, cuf zanzibar inabebwa na maalim na upemba wake na si chama leo hii maalim akihamia chadema cuf haitopata jimbo hata moja pemba kwa taarifa yako!! hapa ni vyama vyote kuungana ndio mwisho wa ccm na wao wanalijua hilo ndio maana wanasaidia vyama kujisajiri ili kuwe na vyama utitili mfano chama cha mziray au dovutwa vya nini?
 
It is a false start on the premise that you want parallel line to meet. Who ever you are; start with CCM waungane na vyama vingine kupursue democracy ambayo ndio msingi mama wa kuleta Maendeleo.

Mimi binafsi nakutilia shaka kwa mtazamo wako wa kuunganisha upinzani na kuleta maendeleo.

Pitia hizi zifutazo:

1. Agenda ya Katiba ni Ilani ya CDM, ili kuiprempt rais kajiingiza humo one wanavyojikanganya maana yake Maendeleo Mark Time.

2. Baada ya uchaguzi Dola kwa maagizo ya CCM inakandamiza kila kitu cha wapinzani for its survival. Bado naamini "Action and reaction are equal and opposite" Kwa hiyo matumizi ya ovyo ya dola lazima yapingwe na organised party. Umesikia chama gani kinaunga mkono mambo mazuri ya chama kingine?

3. So wrongs have been committed by the Dola na CCM kunyima nchi hii maendeleo. Hawa wawili wameteam for their survival pamoja nakutumia mamluki kwenye baadhi ya vyama. Why shift the responsibility when you can take it? Ndiyo wanachofanya CDM ndiyo maana wanaungwa mkono nna baadhi ya wananchi wanaowaelewa. Ni katika hoja hii nakutilia shaka na wewe.

4. Angalia Sera (Siyo ahadi za vyama (CCM)) wapi zinakutana, kwa uongozi upi unao ona fursa ya kushiriana zaidi ya kuhujumiana?

Jifunze yafuatayo

CCM imefanikiwa kuibadili dola kuwa tawi lake. Kwa maana nyingine serikali haipo, kilichopo ni tawi la chama cha mapinduzi inayoitwa serikali. Kwa hiyo mipango, kazi za serkali zinafanywa kisiasa kunyume na sheria, taratibu, kanuni na rasilimali zilizopo nchini. Ushahidi ni hizo kashfa. Ushahidi mwingine ni wa leo hao wana wa wafalme wamekuja kuuza (kufanya biashara na Rais). Movernpic changes ownership from Prince Charles to Agha Khan, prince wa kiarabu naye utasikia.

Wananchi wamepigika, wana uzoefu na hizo ngonjera za kuunganisha vyama au wauzofu wakunadanganywa hivyo. Wanaishi kwa matumaini siyo ya muungano wa vyama bali uongozi wa vitendo wa chama makini.

Wewe na mimi kwenye hii forum tunamuwakilisha nani? Nadhani hatujafanya uchaguzi sahihi wa kukataa kinachoendelezwa na CCM na Dola. Tunajificha kwenye blanket la muungano wa vyama ambao hauna nafasi kwa sasa na wala kikatiba.

Nina mengi ya kukueleza naomba nikomee hapa kwa sababu thread yako ni brain teaser
 
Back
Top Bottom