Ongezeko la watoto wenye vichwa vikubwa(Hydrocephalus) na Mgongo wazi(spina bifida)

Tram Almasi

JF-Expert Member
Feb 26, 2009
749
226
Miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa vilivyojaa maji kwa jina la kitaalam ''Hydrocephalus'' na wenye mgongo wazi ''Spina Bifida''. Takwimu zilizotolewa karibuni na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Dr. Shabani Hamisi zinaonyesha kwamba katika kila watoto hai 1000 wanaozaliwa,3.02% wanazaliwa na matatizo haya. kwa maana hyo kila mwaka watoto 4485 wanaozaliwa wakiwa na matatizo haya.Kati ya hao wanaopatiwa tiba ni 200 tu waliobaki 4285 hawajulikani wako wapi au wanaishia wapi. DSC07602.JPG DSC08167.JPG
kukusanyika kwa maji katika kichwa aidha baada ya homa kali,degedege au kwa ajili ya uvimbe kichwani unasababisha hydrocephalus. Na upungufu wa folic acid wakati wa ujauzito inasababisha Spina Bifida.Wanawake wengi wanapokuwa katika umri wa kuzaa au wanapopata ujauzito hawapati folic acids ambazo ni muhimu kuondoa tatizo hili. Folic acids zinatakiwa kuliwa bila kukosa katika kipindi cha ujauzito. wengi hawapati hizi dawa, achilia mbali vijijini hata mijini wengi hawapati na wale wanaopata huzitupa wakidai zinawatapisha kutokana na harufu yake na hivyo wana-risk kuzaa watoto wenye matatizo haya. Ni muhimu kula hizi dawa ambazo zina-supplement kile ambacho kingepatikana ktk vyakula asilia ambavyo havipatikani. DSC08167.JPG sbFIDA.JPG
Je, ukiwa kama dada,mume au ndugu unajua juu ya hili?Wewe mwenyewe au mkeo mnafanya nini kuepuka tatizo hili? Kama ukimuona mtoto mwenye tatizo hili na anafichwa nyumbani mshauri mzazi ampeleke hospitali apatiwe tiba mapema. NAWASILISHA.
 
Back
Top Bottom