Ongezeko la Watoto wa Mitaani ni Tishio kwa Taifa..

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
925
Taifa linaangamia kwa kukosa wenye maarifa. Ongezeko la matatizo katika taifa hili ni kisahilio cha maafa katika siku za usoni.

Wimbi la kuongezeka kwa watoto wa Mitaani limekuwa likichukuliwa kirahisi mno na jamii yetu. Hivi leo kila kona ya mji unaopita huwezi kukosa kukuta watoto wa mtaani ambao wengi wao wanaonyesha kuwa sugu na maisha magumu. Katika kundi hili la watoto hao, wapo pia ambao wanajihusisha na ukahaba, ukora nk. Hivi leo, karibia kila mji hapa nchi (hata kule kwa wenzetu Zenji) lazima utakutana na maeneo ambayo ni kituo cha makahaba (wauza miili), kuna maeneo ambayo huwezi kuuliza kutokana na umaarufu wa kuzalisha "makahaba". Ukiachilia wale ambao waingia katika biadhara hii kwa hiyari, wapo wale ambao maisha yamewalazimisha kuuza miili yao. Wengi wao ni wale ambao walikumbwa na shida za kifamilia nk.

Pengine najiuliza, kama Serikali inaweza kujenga magereza ya kuhifadhia wafungwa na inatumia fedha nyingi sana kuwahudumia waharifu wakiwa huko magerezani, ni kwa nini isiwe na mpango wa kuwa na vituo maalumu vya kuwatunza watoto ambao tuna wahita watoto walio katika mazingira magumu (lakini hatuwasaidii??). Ikiwa jamii inaweza kuchangishana kwa ajili ya mambo ya kifahari kama harusi nk, ikia runaweza kuwachangia waliopatwa maafa nk, kwa nini watanzania tusione ipo haja sasa ya kuweka mkakati wa kumaliza tatizo la watoto hawa wa mitaani kupitia nguvu sa pamoja na sio kama ilivyo sasa kupitia NGOs amabazo nyingi huwa sinafanya kazi kwa malengo ambayo pengine ni ya Kitapeli au ya kibinafsi?..

Sielewi nini maana ya kuwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii ikiwa mengi ya yale inayopaswa kuyasimamia yanashindikana...
 
Hapo kwenye red, nakumbuka katika halmashauri fulani hawa wenye NGOs waliambiwa pamoja na shughuli zao kufanyika kwa ufasaha basi angalau watume na taarifa zao za fedha ili ijulikane ni kiasi gani khutumika kwa ajili ya evaluation/value for money, hawakuzitoa ng'o, na NGOs nyingine zinaishia kugawa mipira hasa katika maswala ya UKIMWI na watoto yatima/wa mitaani. Wabongo NGOs ni ulaji na wizi mtupu.

Mwisho wataalam wa saikologia wanadai ukiwaweka hawa watoto peke yao watajiona wanatengwa na jamii na watakuwa na hulka tofauti hivyo wakiwa watu wazima hawataweza kushirikiana na watu wengine na watakuwa wanyonge, inashauriwa pamoja na kuwekwa pamoja basi wachanganyike na watoto wengine kuanzia shule za awali na kuendelea, ingawa mpango huu pia una matatizo maana watoto wengi hutoroka na kurudi mitaani walikozoea...
 
Lipo tatizo kubwa sana Mkuu. Hizi NGO hakika ni vyanzo vya Ulaji wa watu. Hata pia ikiwa strong kama Dogodogo Centre, Kuleana, nk hakuna uhakika sana kuhusu survival yake kwa siku za baadae hasa yule aliyeianzisha akifa au kuamua kujihusisha na masuala mengine..

Hawa watoto wa Mitaani wakishazoea sana kukaa huko wapokaa, si rahisi kuhifadhika kutokana na mazingira wanamokulia..Serikali ikipiga marufuku kupitia mikakati ya kuwaondoa na kuwatunza katika vituo halali, inawezekana kabisa hata misaada inayotolewa na jamii hata wafadhili ikaweza kuonekana ikileta matunda (huko wataweza kuratibiwa na kupatiwa huduma muhimu ikiwemo elimu nk). Pengine, kiini cha hawa watoto ni wazazi walioshindwa jukumu, wapo baadhi ya watoto hawa wanaishi mitaani na wazazi wao..wakiombaomba kwa staili ya kulahisisha maisha..hawa nao ni rahisi sana kwa serkali kuwathibiti.
 
Issue ya watoto wa mitaani ni ngumu mno,
Kwasababu hakuna hata mtu mmoja anajali katika serikali au wizara husika ambaye anaweza kuwafikilia, binafsi naona watanzania wengi tunamapungufu akilini mwetu, ki haki kabisa hili la watoto wa mitaani ni tatizo ila wachache ndo tunaliona nitatizo hata humu JF ni wachache ambao wataguswa na isue hii. . . Ila under the sun Wewe usipo hurumia watoto wa wenzako wako watakuga kukutana na magumu kama hayo. Nh kazi kukua bila wazazi
 
This may sound very harsh and cold, but hili suala la watoto wa mitaani root cause yake ni wazazi wa hawa watoto.
Unakuta familia ya baba na mama wote chini ya miaka arobaini but wanawatoto zaidi ya sita na bado wanazidi. Hawana kipato cha kuweza kumudu size ya familia yao. Hii ilikuwa sana sana vijijini lakini na mijini nimeishuhudia.
Kwa upande wa vijijini, enzi zile ilikuwa faida kuzaa watoto wengi wakasaidie kulima mashamba. Tena baada ya mavuno, baba ndio anauza na kutumia hela hizo kuoa mke mwingine wakuja kusaidia kuzaa na kuongeza free labour.
Unfortunately, those days are over.
Watoto wa siku hizi hawalimi.
Baada ya muda wazazi wanashindwa kumudu hizo familia zao. Ndio unakuta wanatumwa mijini kuja kuishi na ndugu wawasomeshe, ila na mjini napo maisha magumu kwa hiyo watoto wa watu wanateseka.
Wengine hutumwa kuwa housemaids, ndio hao wengine hupelekwa kwenye ukahaba.
Na watoto wengine wanashindwa maisha magumu nyumbani kwa hiyo wanatoroka kujaribu kutafuta maisha yao wenyewe kwa njia yoyote.

Watoto ni responsibility ya baba na mama.

Hili tatizo kubwa ambalo haliongelewi waziwazi, yaani chanzo cha maisha magumu kwa hawa watoto.

Je, tufanyeje ili familia, mijini na vijijini waweze kujali maslahi ya viumbe wanavyovileta duniani?

PS: Kunabaadhi ya nchi hutoa huduma za elimu na afya bure kwa mtoto mmoja tu, ukizaa zaidi, serikali inakutoza ushuru kwa hao watoto. Yaani wazazi na serikali vinashirikiana kugharamia elimu na mahitaji ya mtoto....
 
Kwa ujumla wakuu nakubaliana nanyi asilimia mia moja. Tukiangalia chanzo cha ongezeko hili la watoto tena wengine wanapo karibu kabisa na Ikulu ya Serikali yetu. Inasikitisha sana pengine kuona viongozi wajuu wakitoa vijizawadi vya mbuzi na mpunga eti wakale watoto siku za sikukuu pasipo kuangalia hasa mahitaji yao makuu kwa maisha ya badae.. Historia inafundisha kuwa watu hatari sana duniani utokana kundi la wale walioishi ktk maisha magumu utotoni hata dikteta Adolf Hitre yasemekana ni magumu aliyopitia ndio yalimfanya achukie baadhi ya wanadamu. Hatujifunzi kwa baadhi ya wenzetu ambapo ni kosa kubwa sana kwa mzazi kumtelekeza mtoto au kuzaa pasipo kujali matunzo ya watoto. Kama tungekuwa na sera madhubuti ya kupunguza vyanzo vya hili tatizo hakika watoto wangepungua. Sijui hata ile Sheria ya Mtoto (the Children Act)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom