Ongezeko la Posho za Wabunge ni Wizi na Dhulma dhidi ya Wafanyakazi

Serikali ndio ya kwanza kuvunja sheria hii.....per diem tu inaweza kuwa kwenye kundi la kutokukatwa kodi, lakini allowance ya kukaa inapaswa kukatwa kodi...sheria iko wazi kabisa wala haina mjadala....sheria ya kodi ya mapato inataka hata ukipewa zawadi na ofisi na ikawa na kiwango fulani cha gharama basi lazima kiwango hicho kiingizwe kwenye kipato chako na kikatwe kodi....

Wenzetu huko duniani wamepiga hatua kweli kwenye masuala ya kodi. Mfano Uholanzi hata ukienda kununua wanawake wanaojiuza pale red light street, inabidi ulilipie VAT ya 6%, na kiwango hiki cha 6% kinatozwa kwenye bidhaa na huduma za kisanii (art work and services).....sisi tumeshindwa allowance za kukalisha ****** na kujambajamba pale bungeni? Ndio maana Malawi wamefanya kujamba kuwa kosa la jinai kabisa..........ukijamba unapigwa fine au jela moja kwa moja...

Kama unachukua fedha serikalini, unatia kibindoni, haikatwi kodi, unataka serikali iendelee kuwa na fedha kutokea wapi sasa......kama ikitoka inaingia mifukoni mwa watu yote...ushenzi mtupu huu
 
suala la posho kwa wabunge alishalimaliza shibuda wa maswa cdm na joseph selasini rombo cdm.
 
Ifikie mahali tusisubiri fulani aseme, hata hao CDM wanacheza kwa principle za siasa. Inapofikia kipindi cha mambo yanayogusa maslahi ya wananchi kwa ujumla, inabidi makundi yote yajumuike. Mfano makundi ya wafanyakazi, makundi ya kiraia n.k

Kutegemea CDM tu ndio waseme, ikitokea siku uongozi wake ukaingiliwa na mamluki wa CCM sijui tutakimbilia wapi .
 
Watanzania mnalalamika sana lakini kuiondoa serikali hii dhalimu ya ccm hamtaki! Ngoja wawaoneshe kwamba wanawadharau mpaka muamke! Mtabaki kusemasema tu with no actions then kwa kuwa wanawajua ni waoga watawatenda wapendavyo na you'll never do anything! Kazi kucomplain and when it comes to action you all go to sleep
 
ndo nchi ilipofikia huko so hakuna la kushangaa

Dawa ya madudu haya kuanzia Meremeta hadi kashfa zote ni kujifinza kutoka kwa Waarabu wa Tunisia, Libya Egypt na hata juzi Yemen. Tuanzishe maandamano Occupy Magogoni na twende tukafie pale hata mimi niko tayari kufa wa kwanza Katiba mpya itakuwa ni ya kulinda CCM na vibaraka wake no way back no retreat no surrender patachimbika mpaka atoke Jakaya tumweke hata Chizi tupate pa kuanzia
 
Hapo kwenye RED nina mashaka makubwa sana juu ya uwelewa wako wa mambo,labda tu ungetueleza Chadema walikwenda ikulu kwa mazungumzo kuhusu nini, hapo ndipo utakapojiona upeo wako ni mdogo sana.

aibu!!! nadhani unagundua kuwa CDM ni wale wale tu!! wamezilamba kimya kimya....haoooooooo, unatoa mipovu humu
 
Chagua CCM - Chama Mama kinachojali maslahi ya Mtanzania hasa Maskini kwa miaka zaidi ya 50 sasa. Tumeamua kuongeza POSHO ya wabunge ili waweze kujikimu na pia kiasi kuzipekeka kwa wapiga kura majimboni kwao kwa shughuli za maendeleo na si vinginevyo: Wananchi kuweni makini na kauli za wanasiasa kuhusu posho hizi. Tuna nia njema kabisa na tunawajari wapiga kura wetu na wananchi wote kwa ujumla.

320,000/- Posho kwa siku mbunge akiwa nje ya ofice yake ni jambo ka kawaida kabisa - CCM oyee.......msikubali kabisa kauli hizi za kichochezi - Zitatugawa watanzania.
 
La kujiuliza hapa ni: Tuna la kufanya kuzuia haya? Wabunge wana TUME YAO YA UTUMISHI inayoamua inavyotaka. Haina wa kuihoji katika maamuzi yake haya isipokuwa BUNGE lenyewe! Zitto tupatie mwanga kidogo jinsi tume yenu hii inavyochaguliwa na inavyofanya kazi.
 
sie wengine tunapigania income zetu zipande(salary) which means PAYE nayo inakuwa juu watu wengine wasio na huruma wanatafuta namna ya kuzitafuna hizi hela jamani kuweni na huruma hata kidogo sasa mtakata tumuamini nani hapa.. mbona mnaziweka dhamira zenu za ulafi waziwazi agrrrrrrrh ... KIMA CHA CHINI WAMESHINDWA KUKITETEA WAMEWACHIA TUCTA hivi hawa ndio wawakilishi wetu kweli ........WATATUKAMUA SANA MORE TO COME........

Hawa TUCTA si ndiyo akina Mgaya hawa?? Wahuni tu. Walipigwa mkwara mwaka jana wamenywea hatuwasikii tena. Sasa hii ndiyo nafasi yao ya kuonyesha umuhimu wao kwa siasa za nchi!! lakini utasikia wameitwa Ikulu wakitoka huko kimya. Au wanafanya madaliiana na serikali.................... sijui kwa muda gani??

Si ni hawahawa waliambiwa tena kwa kupitia wazeee wa CCM DSM kuwa hata wa miaka nane ijayao 300,000 kama kima cha chini haiwezekani?? Sasa wabunge wao wanavuta hiyo kwa siku. Mgaya anapigwa kivovozi kishawasahau wafanyakazi wenzake. Mshahara wake actually si wa serikali................. Wafanyakazi ambao alitakiwa awaongoze na kuwatetea ndiyo wanamlipa mshahara mnono na malupulupu kibao. Jaribu kufuatilia mishahara ya hawa viongozi wa vyama vya wafanyakazi utajua ni jinsi gani wanavyofaidi kulioko wanaojidai wanawawakilisha au kuwatetea. Ukipata kazi TUCTA una uhakika wa mlo kamili!!
 
Katika hili nayarudia maneno yangu yale yale..tunawahitaji Wanaharakati tena wanharakati wakakamavu na wanaoweza kujitolea muhanga na sikama hawa wakina Kibamba tulio nao na si wanasiasa..Mwanasiasa kila siku yeye anawaza kujilimbikizaia mali..kada ya Siasa kwa Tanzania ya leo, haitofautiana sana na kada ya Biashara...nkimaanisha wanasiasa wana waza sawasawa kama wafanya biashara wawazavyo......
 
siku nyingi nilishasema hapa jamvini hakuna wanasiasa tanzania ila ni maopurtunist ,
na hili la posho linaelezea hivyo, ni misaada gani wanayotoa huko majimboni? watu tunadanganywa sana watanzania. nikimuona mbunge yoyote anapita mbele yangu namdharau sana sababu ni mnyonyaji hakuna wakujitetea kwa hili na haya matabakaya kipato wanayotengeneza iko siku yatawaumiza na nchi itakuwa kwenye hali mbaya sana.
halafu vitu vya maana hawapiganii. wabunge wote ni wasaniiiiii na bunge liko kibinafsi zaidi no body goes there for the sake of his people, sio upinzani wala chama tawala. HALAFU 2015 MTU ANIAMBIE NIMPIGIE KURA AU NIBEBE BANGO LA KUMSUPPORT MGOMBEA? NITAKUWA MWEHU KWA KAZI GANI ANAYOIFANYA BUNGENI
1. KULALA BUNGENI
2. KUPIGIANA VIJEMBE
3. KUUNDA KAMATI MAALUMU AMBAZO HAZINA MAAMUZI YA MWISHO NI KUTOA MAPENDEKEZO TU
4. LA MWISHO NA MUHIMU KUDAI MISHAHARA YA WABUNGE IONGEZWEZE NA POSHO ZAO
 
Haya ni matokeo ya mfumo mbovu tulioujenga kwa muda mrefu ambapo mbunge jukumu lake kuu ni "kuwaletea wananchi maendeleo". Tunapima performance ya mbunge kama kajenga barabara, shule, hospitali jimboni kwake n.k. Hivi wakuu wa mikoa na wilaya wanafanya kazi gani?

Matokeo yake sasa wabunge wamejipachika jukumu lingine la kutoa misaada kwa wapiga kura wao. Wanajustify hizo posho wanazolipwa sio zao peke yao...wakitoka tu nje ya ukumbi wa bunge wananchi wanawangoja kuwapiga mizinga ya nauli na vocha!! Ni wapi imeandikwa majukumu ya mbunge ni kutoa misaada kwa wapiga kura wake? Pesa za mfuko wa maendeleo jimboni zinafanya kazi gani??

Kinachosikitisha zaidi wananchi watalalamika weeeeee....lakini ikifika 2015 waheshimiwa watawapelekea t-shirt, khanga, kofia na pilau watasahau yooooote na kuwapigia kura kuwarudisha mjengoni!!!

Na bado.........
 
Tukisema Tanzania is full of corrupt bureaucrat mnakuwa hamtuelewi. Mie na baadhi yetu pamoja na zitto tulilipigia kelele jambo hili siku nyingi hivi leo ndio mnastukizia. Endeleeni kushangaa but ukweli wa mambo posho ni rushwa na dhulma kwani badala ya kumpunguzia mzigo wa gharama za maisha mlalahoi kwa kumpunguzia kodi. Serikali inamwongezea kodi mlalahoi na huku wanawaongezea marupurupu wabunge. Halafu mnasema bungeni kuna la maana wanalolifanya zaidi ya kutengeneza mirija ya ufisadi tu.
 
******* sana hawa watu yaaani watu tuna..........................kumanina zao yaani...........agggggrrrrh.
 
Back
Top Bottom