Ongezeko la Mshahara: Nini maana yake?.

BIG Banned

JF-Expert Member
May 4, 2012
262
71
Wataalam wa uchumi hebu tusaidieni nini hasa maana ya ongezeko la mshahara. Napata wasiwasi sana na hizi nyongeza za mishahara kwa serikali kila mwaka. uhusiano wa ongezeko la mishahara na kupanda kwa bei ya mahitaji ya kila siku. Maana kama nilikuwa napata laki 2 na ilikuwa inanitosha kwa mwezi, halafu ifike wakati napata milioni 2 na bado ikifika mwisho wa mwezi sibakiwi na kitu, sasa hili neno la ongezeko la mshahara naona kama linatumiwa vibaya hapa!. Ongezeko ni Figure tu ya mshahara au ni value ya mshahara!!.

Nawasilisha.
 
Wataalam wa uchumi hebu tusaidieni nini hasa maana ya ongezeko la mshahara. Napata wasiwasi sana na hizi nyongeza za mishahara kwa serikali kila mwaka. uhusiano wa ongezeko la mishahara na kupanda kwa bei ya mahitaji ya kila siku. Maana kama nilikuwa napata laki 2 na ilikuwa inanitosha kwa mwezi, halafu ifike wakati napata milioni 2 na bado ikifika mwisho wa mwezi sibakiwi na kitu, sasa hili neno la ongezeko la mshahara naona kama linatumiwa vibaya hapa!. Ongezeko ni Figure tu ya mshahara au ni value ya mshahara!!.



Nawasilisha.

Inawezekana kweli tunadanganyika kwenye hili. Unaongezewa (Figure) mshahara kwa kiwango ambacho ni chini kuliko kiasi cha gharama za maisha zilivyopanda. Hii inakuwa haileti maana yoyote. Pili inawezekana kabisa kwa kupungua kwa gharama za maisha (chakula etc) unaweza ukasema vilevile umewaongezea wananchi mshahara, sababu watakuwa na uwezo wa kusave na kufanya mambo mengine.
 
Ongezeko la mishahara limekuwa ni suala la kisiasa tu, hakuna nia ya dhati kabisa kufanya watu wawe na maisha mazuri. Ukiangalia mfano kwenye hilo jedwali hapo chini ndivyo hali ilivyo hapa nchini kwetu, katika hali hiyo hatusongi wala hatutasonga mbele hata siku moja, tupo palepale au tunaendelea kuumia zaidi. Tunapotezeana muda tu......., wajiuzuru watu wenye akili wachukue nchi.

Mwaka​
Mshahara​
Matumizi​
Baki​
(ongezeko 15% kila mwaka)​
(Ongezeko 25% kila mwaka)​
2007/8​
100​
85​
15​
2008/9​
115​
106.25​
8.75​
2009/10​
132.25​
132.81​
-0.56​
2010/11​
152.1​
166.01​
-13.91​
2011/12​
175​
207.52​
-32.52​
 
nadhani mheshimiwa DASA katuonesha usanii unavyofanyika pia purchasing power of our currency nalo nitatizo kubwa na inafanya mishahara kuongezeka negatively wakati cost of living zinaongezeka positively.
 
Kwa uwezo mdogo wa uchumi wetu, kuongeza mishahara ni kuyummbisha uchuni kwa kuleta mfumuko wa bei.
Mfano upo hivi; katika kijiji (nchi) uwezo wa kuzalisha kilo 100 za unga, watu wake mf. 20 wanapata Tsh 100,000/. Mshara ukiongezeka, wale watu watakuwa na uwezo mkubwa wa kunua bidhaa, huku bidhaa hazijazalishwa, hivyo, wale watu 20 watagombaniana zile kilo 100 hatimaye, kutokana na kanuni za soko, bei ya unga inapanda.
Kuongeza mishahara kuna tija ikiwa kasi ya ushumi ni kubwa, kiwango cha mishahara kinapaswa kwenda sambamba na ukuaji wa uzalishaji.
 
Kwa level yangu ya uchumi (form six),mishahara kuongezeka ina maana serikali kuongeza money circulation in the economy na hii itapelekea more demand of goods,so kama goods are not produced enough then kitatokea kitu kinachojulikana kama goods scarce,na hii itapelekea kupanda kwa bei zaidi na zaidi na mshahara kupanda hautakuwa na maana kabisa,then matokeo yake 1.inflation 2.depreciation of money value 3.decline of demand 4.decline of firms 5.redundancy of workers 6.political instability etc,so dawa hapa kwanza nikuimarisha viwanda viweze kuproduce as much as possible then mishahara kupanda itasanifu maisha halisi ya watanzania,leo tz tuna economic growth lkn hatuna economic development,so wakuu siyo kwamba napinga kupanda kwa mishahara lkn napenda kutoa mtazamo wa kiuchumi na njia nzuri ya kuleta maana halisi ya kupanda kwa mishahara.napenda kuwasilisha
 
Back
Top Bottom