Ongera wanaharakati kwa maandamano

JOHNKEKE

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,311
1,463
Ni ukurasa mpya baada ya baadhi ya wanaharakati kushiriki maandamano ya kuilazimisha serikali ishughulikie mgomo wa madaktari hapo jana. Nilifarijika kwani naamini ni mwanzo mzuri wa kudai haki kwa watawala wasiosikia na wasio na chembe ya ubinadamu.

Ninaendelea kusikitishwa na viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kushindwa kutoa matamko yenye uzito unaolingana na tatizo au kushinikiza kwa namna tofauti ili kumaliza tatizo hili ambalo ni dhahiri viongozi wetu legelege wameshindwa kutatua.

Ni kwa njia kama hii ya maandamano ndio tunaweza kushinikiza watawala wawajibike badala ya kujifanya miung watuna kutotaka kushiriki kutatua matatizi makubwa na ya dharura ya jamii.
 
Back
Top Bottom