Ondoa woga unapotaka kufanya kitu

ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
14,699
9,461

Uoga ni ile hali ya kupatwa na hofu kupita kiasi inayokuwa ndani ya mtu ama mwanadamu juu ya jambo, kitu, fulani ambavyo vimewahi au vinatokea kwake

Ama ni ile hali ya kusitasita kuthubutu kufanya mambo na kuweka mashaka kama matokeo ya hayo mambo uliyotarajia kutokea yasitokee

Hebu niwadokezee kitu marafiki zangu wa humu jf, mwaka ndo unakatika na kama umekwisha angalia nyuma utaona kuwa bado hujakamilishalile ulilokusudia kulifanya kwa mwaka huu, na ndo tumebakiza miezi miwili. Kwa mtazamo wako Je unaona ndani ya miezi 2 unawezakukamilisha au unaona hutaweza kukamilisha.

Usiwe na mtazamo hasi ambao unaleta shaka na hofu ya kutokuthubutu kutenda japokuwa waonahaina haja ya kufanya lile jambo/kitu ndani ya hiyo miezi. Watu wengi wamejawa na hofu/woga wa kutokuthubutu kufanya kitu.

Ushauri wangu kwenu hebu ondoa woga ndani yako unapotaka kufanya kitu. Usiangalie mazingira yaliyokuzunguka yanasema nini juu yako, wewe kaza buti angalia mbele na fanya ilile ulilokusudia kwa wakati huo.

Basi napenda kuwaambia nimetoa kitabu changu cha Woga na ningefurahi kamamtakihitaji msisite kuingia pm. Nawatakia baraka na mafanikio tele katika shughuli zenu.

"Fungueni macho yenu muone kwani mafanikio mnayo katika mikononi yenu ondoeni woga wa kutothubutu".
 
Kidogo kama inaingia akilini lakini swali mwaka huu umepata nini ukashindwa kufanyakutu?ukijicheki utakuta hakuna cha maana ulichofanya hivyo shida siyo uoga bali msunguko hamna tena
 
Uoga ni mbaya sana, mzingira yanongopa, facts zinongopa, wako wanao wamezeeka kumbe wananafasi, limiting beliefs ni mbaya kulikotunavyodhani. Kitabu bado kinapatikana
 
Back
Top Bottom