Ona Upuuzi Mwingine wa Masoud Kipanya

Mi sijauona huo upuuzi, Nimjuavyo Kipanya ni mtu wa kutafakari sana. Viongozi wetu waliharakisha utekelezaji wa huduma kuelekea Loliondo tena wote walielekea huko (ajabu na kweli) na wakiumwa hawatibiwi hapa, wanakimbilia South Africa na India, madai ya madaktari wetu wanachukua muda mrefu kuyatafutia majibu ya muafaka. Kwani promo inachukua muda gani? si kazi ukaona imeanza promo mpya na kila mtu akapewa rufaa na kina P*nda kwenda kutibiwa kwa babu.
 
Kazi sana kuelimisha watu hilo neno upuuzi ndo analotumiaga kipanya mwenyewe kufikisha ujumbe wake sasa majitu mengine yanaibuka huko yalikotoka yanaanza kukoroma tu
 
Nusu ya wachangiaji humu hawaelewi hata nini kinaendelea au hawaelewi kazi za masood kipanya!!!
 
Wabongo kwa kukurupuka mnaongoza aisee!Hivi hamfuatilii vikatuni vya Kipanya hata katika gazeti la mwananchi?Yeye mwenyewe ndiyo huwa anaviita UPUUZI WA KIPANYA sasa watu asubuhi asubuhi anakurupuka tu kucomment bila kujua!Wanaomponda mtoa hoja wao ndiyo wapuuzi kwelikweli sasa!!!

Nawasilisha!!!
 
kipanya 2.jpg
Hilo gwanda la kipanya limekaa sawasawa na ujumbe umeeleweka
 
Kati ya Masoud Kipanya na wewe mleta uzi nani mpuuzi? Naamini mleta uzi ni mpuuzi zaidi
 
Aisee,fikiri kabla ya kusema..Na kama hauna cha kuongea piga kimya sio unabwabwaja tu..
 
Mtoa thrd lazima atakuwa katoka usingizini akaamua kuandika bila kupiga mswaki au ana bif binafsi na Kipanya. Nimetizama sana catoon ya kipanya sijaona upuuzi wake kbs! Ila wanasemaga ukizoea nguo za mitumba hata mtu akivaa ya dukani utahisi ni mtumba tu! Kuna mtu kazoea mambo ya ovyo ovyo na kipuuzi puuzi hapo.
 
Ndallo, kazi unayo,

ingekuwa ni mtihani huu hapo ungeniambia Great thinker wangapi wame'sink'. katiya wachangiaji zaidi ya therasini waliokurupuka ni zaidi ya nusu.
Kwa kukusaidia ili usiendelee kutukanwa weka vifunga semi kwenye headind yauzi, hususani neno UPUUZI, inaweza saidia
 
mtoa thrd lazima atakuwa katoka usingizini akaamua kuandika bila kupiga mswaki au ana bif binafsi na kipanya. Nimetizama sana catoon ya kipanya sijaona upuuzi wake kbs! Ila wanasemaga ukizoea nguo za mitumba hata mtu akivaa ya dukani utahisi ni mtumba tu! Kuna mtu kazoea mambo ya ovyo ovyo na kipuuzi puuzi hapo.

hahahaha kazi kwelikweli!
Mtihani hapa una
000000

umetaga mayai!
Inabidi mtu uwe mweledi!!!
Soma na majibu ya wenzio
nyie ni wale wa ndiooooo bungeni,
 
Mtoa thrd lazima atakuwa katoka usingizini akaamua kuandika bila kupiga mswaki au ana bif binafsi na Kipanya. Nimetizama sana catoon ya kipanya sijaona upuuzi wake kbs! Ila wanasemaga ukizoea nguo za mitumba hata mtu akivaa ya dukani utahisi ni mtumba tu! Kuna mtu kazoea mambo ya ovyo ovyo na kipuuzi puuzi hapo.

Acha kukurupuka wewe, mtoa mada yupo sahihi kabisa. Wewe ndio sio mfuatiliaji wa katuni za Kipanya....
 
Tatizo watu hawaelewi chimbuko la hilo neno "upuuzi". Sasa kazi kwako Ndallo kuwaelewesha maana wao wamedhani umemdharau/mtukana Kipanya.
 
Back
Top Bottom