Elections 2010 On TBC1: Augustine Mrema vs John Mrema vs Meira (jimbo la Vunjo)

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Wakuu,

Muda si mrefu (saa 3 usiku) kwa mlio nyumbani kutakuwa na Jimbo kwa Jimbo ambapo hii leo mheshimiwa Augustine Lyatonga Mrema wa TLP atakuwa kwenye mdahalo na John Mrema wa CHADEMA.

Tunatarajia mtaangalia na kutufahamisha mdahalo unavyoendelea, kuna mdau ameniahidi kutuma sms ili ni-update hapa.
 
Mbona ni wagombea wa CHADEMA na TLP tu? Mgombea wa CCM kulikoni? Au baada ya mambo fulani pale Jimbo la Ubungo, imebidi CCM ikataze wagombea wake kushiriki kwenye midahalo?
 
Anaanza wa CCM. anaelezea Ilani yao inaongelea Mafanikio na yako mengi wamefanya kielimu, miundombinu jimboni
 
Miradi ya Umwagiliaji pia imefanywa kwa kiwango kikubwa.

Miaka 5 ijayo kuna vipaumbele 10
Kilimo - Oragnic Coffee imebuniwa, Kilimo kiwe cha Kisasa, umwagiliaji, kujenga maghala, soko la kisasa kama kibaigwa ili kufaidika na soko la EA
 
MiundoMbinu - Kumalizia barabara
Utalii - Wananchi wafaidike kutokana na gawiwo la Mlima Kilimanjaro kwa 25%
Elimu - Kukamilisha shule za kata ziwe na walimu na vifaa
Afya - Zahanati kila kata
Ajira za vijana - Kuongeza ajira hasa katika utalii, kuimarisha vikundi vya ujasiliamali. Ndani ya miaka 3 kila kijana awe na kikundi
Maji - Kila kijiji kiwe na miradi ya maji
 
Anajifagilia kuwa amekuwa Ubunge kwa miaka 10 ana uzoefu
Amekuwa waziri na Naibu Waziri Mkuu, mtu wa 3 toka kwa Rais
 
Jambo analokusudia ni kuondoa umasikini na ufukara
Yeye ndo liyershika dhahabu iliyokuwa inaporwa na kuruhusu mabebki yanunue dhahabu
 
Miundombinu: CCM wanasema tu . . . masuala ya barabara alianzisha yeye alipokuwa mbunge. Yeye ni kiongozi makini ataijenga.
 
Suala la Kahawa - Yeye ndo alisimamia kidedea, alienda hadi ujerumani na akasimamia bei zipande mara 3 alisimamia vizuri na watoto wanasoma
Haki za watu - Akina mama walikuwa wanaonewa kwa ajili ya kodi ya kichwa. Aliondoa fedheha hiyo na mwanamke wa kichaga akatembea kifua mbele
Tutatafuta utaratibu wa kuwezesha VIKOBA kama Mengi alivysaidia. Atawatafutia pesa
Muda wake umeisha sasa . . . .
 
Sasa Mrema wa CHADEMA

Ana miaka 30.
Mkurugenzi wa CHADEMA toka 2007 mambo ya Bunge, Mkuu wa Idara ya Utafiti
 
Sasa John Mrema ndo anamwaga sera...ana miaka 30. Anasema ana vipaumbele saba, cha kwanza ni elimu
 
Mkuu Superman ukimaliza nitakuja kuweka comments zangu, japo ningependa sana wananchi wawe wanapewa nafasi ya kuuliza maswali na hasa utekelezaji wa hizo priorities, maana nyingine naona hazitekelezeki, unless jimbo libadilishe mfumo wa ajira, mfano kuongeza walimu wa shule za kata. Walimu wa shule za kata mwajiri ni serikali za mitaa ambayo hai-train na hata yebo yebo wanaopatikana wanasambazwa Tanzania nzima, so bado uhaba wa walimu unabaki pale pale tu.
 
CHADEMA Wana Ilani Kuu na Majimbo

Jimboni:
Elimu - tumerudi nyuma, shule ya mwisho imetoka vunjo, msingi na sekondari ziko vunjo - Ni aibu. Kuna vyuo 2 vya Ualimu na Chuo Kikuu cha Tumaini
Wabunge waliopita hawakuwa na mpango - Yeye atasimamia na kuzuia ulaji. Anatoa mifano ya ulaji
 
Mbona ni wagombea wa CHADEMA na TLP tu? Mgombea wa CCM kulikoni? Au baada ya mambo fulani pale Jimbo la Ubungo, imebidi CCM ikataze wagombea wake kushiriki kwenye midahalo?

hapo mi ndo nachoka na CCM..Raisi wao wanamkwepesha kwenda kwenye midahalo wabunge wanakubali...watu wanataka JK apandishwe kwenye mdahalo atolewe jasho
 
Anatoa data jinsi pesa za TASAF nk zilivyoliwa
Afya - Atahakikisha wataalamu wa afya na dawa zinapatikana
Biashara - Jimbo liko mpakani. Akina mama wananyanyaswa. Wapewe elimu ya soko la pamoja na wasinyanyaswe
Wastaafu wengi - Umoja wa wastaafu kuanzishwa ili wazee watupe ujuzi
Miundombinu - Wengi wanatoa ahadi. Mbunge hana pesa. kazi ni kusimamia. halmashauri imekuwa ikitoa tenda kwa watu wasio na uwezo. Kuna ufisadi. Barabara hazidumu

kamaliza
 
Back
Top Bottom