On Star TV: TCRA na majibu kwa maswali juu ya Mfumo wa Digitali

nawashangaa sana wenye dhamana na haya mambo! wanashindwa kuwa na legitimacy katika hili. tumenunua ving'amzi, ili vingamue, suala la kuuziwa antena ni la nini? wametoa antena za ndani, hazikamati..

wametufanya wajinga sana. wanatufanyia biashara kuuza bidhaa zao, kama ni antena king'amuzi tumenunua, iweje tununue antenna za nje na milingoti? technojia ipi hapo mnayosema. hamuoni mmeshindwa kurusha mawimbi?

Dah Kweli Inno Mungi Una Kazi kweli kweli kueleimisha Watanzania
 
Asante Start TV kwa mada nzuri...

Naomba niuwauliza wataalamu waliopo DSM... Wamesema Digital ni ule mfumo unaotunia MADISH. Je, STAR TIMES ambao wanauza VING'AMUZI na wanatumia ANTENA za kawaida "MWIBA WA SAMAKI" sio DIGITAL?

Mi naona ni Janja ya SERIKALI kukusanya KODI kwa Watanzania..!

Asante sana Star TV.
 
Je mpaka hiyo Disemba kutakuwa na ving'amuzi vingapi!? Maana mimi nina vitatu sasa hapo inauwaje kwanini kusiwe na king'amuzi kimoja!?
 
Swali langu ni kwamba mfumo huu wa digitali tutaendelea kutumia kingamuzi cha Star Times au mnaleta kingine?
 
Nafikiri kwa Mtanzania jambo la muhimu sio hizo faida za digital against analogue bali ni switching cost zinazoambatana na hayo mageuzi.

Ni kiasi gani atagharimika kuingia katika mfumo mpya. He/she (mtanzania wa kawaida) is not interested on the quality of voice or picture bali ni switching costs, yaani atatumia kiasi gani au itamghalimu kiasi gani kuhamia mfumo huo mpya kwa faida ambazo sio muhimu kigharama kwake.

Ni vizuri mkawaambia hizo gharama hasa ukweli kuwa mfumo mpya unahusu subscription fee au "LUKU" kwa lugha rahisi.

Je tumeangalia gharama hizo au tunaingia mfumo mpya na baadae tuanze kulalamika kuwa ni kwa ajiri ya wachache tu?
 
Kuna mkanganyiko wa terminology katika kiswahili.

1. je neno king'amuzi ni kile tu kama cha startimes, agape na zuku au hata hizi receiver ambazo tunaendelea kuzitumia kupitia antenna na madishi,au rimu za baiskeli
2. Ikiwa wenye madishi na receiver za sasa wataendelea kuzitumia je haya makampuni kama startimes, agape nk watafanyeje biashara kutoka kwa watu wachache watakaozitumia receiver aka "ving'amuzi vya makampuni haya.
3. kwenye radio hadi leo kuna MEDIUM BAND bado hadi wa leo kwa nini kwa TV tu iwe lazima.
4. Kuna suala la tofauti ya kipato duniani - ina maana tunataka kujifanya kipato chetu ni sawa na cha nchi za magharibi??
 
Mfumo huu unawahusu watu wa TV tu?

Nilihangaika sana kufungua kituo cha redio lakini usumbufu nilioupata sina hamu, kupata frequence ni kazi ngumu sana. Kuna mabadiliko tutarajie huku?
 
suala sio gharama ya kununua king'amuzi bali ni gharama uendeshaji wake.
 
Mfumo wa digital ni lazima uwe na flatscreen(600000), receiver deck(yenye mfumo wa digital=500000)، Kununua na kufungiwa vin'gamuzi(420،000 wakati wa promotion) pamoja na gharama ya kulipia(monthly payee 20000).

Je watanzania sisi tulio masikini wa kutupwa tutaweza kumudu gharama hizi!? Tcra hamuoni kwamba zaidi ya miaka 30 ijayo watanzania zaidi ya 65% watakuwa hawapati habari?

Kuna uharaka gani wakuleta mfumo huu wa gharama hizi wakati mwazijua khari za watanzania wenzenu!!? Au ndo kwamba aloshiba hamfikirii mwenye njaa!!?

Wana JF sina access ua tv pleasa naomba atakayesikia jibu langu aniwekee hapa!!

OMBI KWA MODS:- Mualikeni huyo Mungi hapa ili twende nae sambamba sisi tusiokuwa na tv!!
 
Je, wenye flat screen aina zote wana haja ya kununua king'amuzi? Naomba clarification katika hili
 
Maswali ya watu wa JF ukurasa wa Facebook:
Nelly G. Mushi Kutoka Moshi: Huu mfumo ni mzuri ila kitolewe king'amuzi kimoja kitakachoonyesha channel zote za Tz..then cost iwe chini; maana ving'amuzi vingine badala ya kuonyesha chanel za maana wanatuonyesha vikatuni tu
Elia Ramadhan wa Zanzibar: Nauliza kuhusu hivi ving'amuzi kweli hadi Decembar vitafanya kazi kwa ufanisi? Kwani vinasumbua sana, mimi naona kama ni ubabaishaji, pia mtanzania wa chini atamudu gharama?

Na star time hapa Zanzibar ipo hoi ktk frequency
Thabiti Seleman Kutoka Songea: Nauliza huu mfumo wa digital unaanza lini kutumika? Na ivyo ving'amuzi vinapatika wapi? Na bei gani?.
 
What is channel za bure? Sidhani kama zitakuwapo tena apart from TBC ambao wana ruzuku za serikali (kodi zetu). Ni vizuri wakafafanua nini maana ya channel za bure katika mfumo mpya. Maana ni wazi channel za bure ni zile ambazo hazina maanana za nje zaidi na siyo kwa credible stations hasa zenye maslahi kwa watanzania kama Star Tv.

Bado naamini kabisa kuwa kwa watanzania wengi opportunity and switching costs ni muhimu nio sawa na kumwambia mtanzania wa kawaida kuwa usafiri wa ndege ni waharaka kuliko wa basi hivyo tuwe na usafiri wa anga tu bila kuanagalai hizo switching and opportunity costs.
 
Yahya,

Hawa jamaa wanaongeleaje suala la Internet Protocol television (IPTV); au hii haipo kwenye mkakati huu?
 
Hawa jamaa nashindwa kuwaelewa!!! Kwanini wasiwe wazi kwamba wanazungumzia Startimes kuwa ndio haijafikia hiyo asilimia 24 ya population? Zuku, ting, dstv wote wanaonekana Tanzania nzima. Tofauti iliyopo ni gharama za ufungaji wa hivyo vingamuzi. Wawe wazi kuwa wanazungumzia Startimes.

Je, hao wenye madishi wanaotumia satellite nao watakosa matangazo au vipi?
 
Yahya,

Huyo mtu wa Tivoli Mwanza atafutiwe kipindi kingine maana anayozungumzia hayahusiani na kipindi. Mambo wa copy rights hayahusiani na topic ya leo.
 
Back
Top Bottom