On Star TV: Ipi Misingi ya Kuendeleza Amani Tanzania?

Bwana Yahya Mohmed,

Ushauri wangu ni kuwa jambo hili linahitaji mjadala mrefu na wa kutosha kwahiyo ni bora mkatenga muda maalum hata wa masaa 3 na kualika wadau wote ili watu watoe mawazo yao na kuelezea duku duku zilizoko moyoni mwao.

Mwisho Nape atueleze ni kwanini rais wa nchi mpaka leo yuko kimya kanakwamba hili tukio ni jambo dogo. Pili Nape tueleze ni kwanini mpaka leo hakuna aliekamatwa.

Naamuliza kwasababu yeye ni kiongozi wa chaman na ndo kimeshika dola. Chama kama chama kimeshauri nini serikali juu ya hatua za kuchukua. CCM ikishauri ina nafasi kubwa ya kusikilizwa ila kama mmekaa kimya basi hiyo ni ajenda ya chama na serilkali yenu.

Nape tuambie nani anaua, ni CHADEMA au polisi?

Ni kwanini mauaji yanatokea pale tu polisi wanapovamia.

Mjiulize, mbona maanadamano ya waislamu yalikuwa salama licha ya kuwa hayakuwa na kibali?

Yaani maelezo yako ni bomba sana. Magamba wote wapate nakala ya hoja zako labda watakurupuka kwenye huo usingizi wa pono!! Nchi inakwenda na maji wao wanavuta usingizi tuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kwa nini nape analalamika kuwa CDM ndio wanaosababisha mauaji wakati CDM hawana silaha,na wananchi pia hawana silaha hivyo haoni kuwa polisi wanatumia nguvu kubwa sana isivyo takikana?Iweje watu wa kada mbalimbali wanalaani polisi ila wao CCM wanatetea polisi kwa kile walichokifanya?Wassira anaposema wataifuta CDM anatoa wapi uwezo huo?yeye sio msajili wa vyama vya siasa.

CCM wanaitetea polisi kwa sababu ni serikali ya CCM imewatuma!!
 
Nilisha sema na leo narudia tena! Kikwete aliitwa chagua la Mungu, nadhani wote mmeona jinsi Mungu alivyo tupenda kwa kutuonyesha uongozi wake ulikuwaje na ukoje na ana kipeleka wapi chama chake kuelekea 2015.

Nape pia ni chaguo la Mungu liloliwekwa makusudi kwenye nafasi ili atimize mapenzi ya Mungu kwa watanzania! Mungu anacho kifanya sasa ni kuanika uozo uliopo ndani ili sisi tutumie akili zetu kuchanganua uozo huo! Mungu anatupenda sana ndio maana ana tuonyesha dhahiri! Ametuonyesha JK , akatuonyesha kwa Dr Ulimboka, akatuonyesha kwenye Epa, kwenye Twiga, kwa Mwangosi na sasa kwa kauli za Nape.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.

Ni kweli mipango ya Mungu ni ya ajabu sisi wanadamua hatuelewi. CCM inachokifanya sasa inajinyooshea njia kuondoka madarakani bila yenyewe kujitambua. Mimi naona kama JK ameamua kuitoa CCM madarakani kinyemela. Mbona mambo yote mazito amemwachia dogo Nape? Lowassa, Membe, Sitta, Nagu ( wawania urais) Mukama (KM CCM), etc. wako wapi? Angalau Sumae although retired he has rebuked this nonsense.
 
Karibuni tena siku ya leo WanaJF kwenye kipindi chetu cha Watanzania Tuongee Asubuhi.
Mada yetu ya leo inahusu ni ipi misingi ya kuendeleza amani Tanzania.

Host Mwanza: Yahya Mohamed
Host DSM: Joyce Mwakalinga

Wageni wetu Dar:
Bwn. Nape Nnauye
Bwn. Juju Danda
Mh. Tundu Lissu

Wageni wetu Mwanza:
Donald Kasongi





Napenda kuwataarifu kuwa mnaweza kufatilia mjadala huu kupitia link ifuatayo:
STARTV LIVE

Karibuni.

Ziada Video Live:

Published on Sep 9, 2012 by mwanakijijiMjadala wa matukio ya mauaji ambayo yamekuwa yakitokea mikononi mwa polisi na hasa kwenye mikutano inayohusisha CDM. Tundu Lissu (CDM) na Nape Nnauye (CCM) wanaangalia chanzo na kiini kwa mitazamo miwili tofauti sana... watch!



video kwa hisani ya Mwanakijiji wa youtube
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom