On Star TV: Ipi Misingi ya Kuendeleza Amani Tanzania?

eeeh Nape bado haamini tu kama polisi ndo wameua! kisha kwahili naye ajiulize kwann kila polisi wanapokuwepo watu ndo wanakufa?
 
Ili kutoa maoni kwa njia ya simu punde line itakapofunguliwa, zifuatazo ni namba za mawasiliano hayo:

+255 732 782788
+255 658 782788

MLIWAHI KUWA NA NAMBA YA VODA, ILIENDA WAPI YAHAYA? 0754732732 au ya RFA?
 
Mh Tundu Lissu, ni kweli Dr Slaa alimtumia sms IGP siku moja kabla ya mauaji ya Iringa?
 
Nape anazungumziaje maandamano ya waislam yaliyofanywa juzi NA hakuna hata sisimizi aliyekufa NA hawakuwa NA kibali?

Nape amesema Tundu Lissu anahukumu kuwa police wameua wakati kuna tume inachunguza.

Swali, Nape hajui kuwa tayari kuna police watano wamekamatwa NA wanapelekwa mahakamani, kwani hawajui kuwa tuna tume inachunguza?
 
Nape atujibu tafadhali na aache upotoshaji!

Tuliambiwa na Waziri Mkuu wazanzibar waislam ni 99%, na inavyojulikana waislamu ndio walipinga kuhesabiwa, je atatuaminisha vp kuwa kule wamewahi kumaliza sensa?
 
eeeh nape bado haamini tu kama polisi ndo wameua! Kisha kwahili naye ajiulize kwann kila polisi wanapokuwepo watu ndo wanakufa?
hakika, kwani wakati mwangosi anauwawa, mwanza kulikuwa na mkutano wa hadhara ukiendeshwa na wenje. Walipeleka barua ya kutoa taarifa juu ya mkutano wao, walikataliwa na ocd nyamagana, walikaidi katazo hilo, wakafanya mkutano bila baraka za polisi, polisi iliamua kuwapotezea, mkutano ulimalizka salama, kila mtu alirudi nyumbani kwa furaha na amani.

Swali kwa nape. Haoni kuwa kuwazuia chadema kufanya shuguli zao za kisiasa ni kuwapaisha kisiasa hasa pale wanapokaidi na kuamua kufanya shughuli zao bila baraka za polisi?

Kwa nini ccm wanaogopa mikutano ya chadema na wanaamua kuiundia zengwe?
 
Kaka nifikishie swali langu kwa wahusika...

Ni sababu gani ya msingi iliyopelekea uongozi mzima wa jeshi la polisi mkoani Iringa (kwa maana ya RPC na Wafuasi wake) kuhudhuria kwa wingi pale Nyololo wakati CHADEMA wakifungua Tawi lao?
 
Swali. Je Tanzania tunayoitaka ndio hii?

Nape, historia inaonyesha kuwa chama chochote pinzani chenye nguvu na kuwa tishio kwa ccm daima huitwa chama chenye vurugu au magaidi, wauaji nk. Je hizi si dalili za wazi kabisa fitina za ccm zidi ya upinzani?
 
Hi, Mada nzuri Yahya, kwa kuwa hakuna kinachoweza kufanyika kama hakuna amani

Nadhani msingi mkuwa wa amani ni usawa na haki. Usawa katika ugawaji wa rasilimali, usawa katika demokrasia, usawa katika elimu na katika kila nyanja ya maisha na maendeleo.

Kunapokuwa na double standards amani haiwezi kuwepo, kunapokuwa na kuonewa amani ni ndoto. Kunapokuwa na wengine kuneemeka, wengine wakipunjwa amani mtaisikia kwa wenzenu.Wengine wanajichotea mapesa ya nchi na kuyaficha uswisi wengine hata mlo wa siku hakuna, amani haiwezi kuwepo. Wengine wanachukua ardhi ya nchi tena kwa kupora wengine, tusitegemee amani hapo.Chadema wananyimwa kufungua matawi, CCM wanazindua kampeni amani itapatikana wapi.Usawa na Haki ndio vitaleta amani.

Swali kwa Nape, anazungumziaje kutotii sheria kulikofanywa na CCM kule Bububu kwa kufanya mkutano licha ya katazo la Polisi? Na mbona hawakuchukuliwa hatua yoyote?

point mku kwenye blue
 
Yahya muulize Nape alisikika akisema 'Nilitoa hadhari kwa mtu yoyote atayeshiriki kwenye mkutano ule wa Iringa kuwa yatayomkuta hiari yake' sasa basi muulize yeye alilijua hilo kuwa askari wataua? pili na yeye akiwa kama nani hata atoe hadhari ile?

CHANZO ILIKUA EATV KWENYE 5CONNECT
 
nape, kusema zanzibar sensa ilikamilika ni kutudanganya watanzania, lile katazo lilikuwa la nchi nzima, halikuhusu bara pekee, kwa nini usikubali kwamba mlivunja sheria? Na hizi ndio double-standards ninazozizungumzia.


naogopa kuongezea kozi mode wamekuwa wakali siku hizi ban ban....ccm hawataki kuwa wakweli na hata siku moja hawajawahi kuwa wakweli
 
Tutamwomba Nape aje JF kujibu hoja hizi ambazo kutokana na muda ktk Kipindi inawezekana tusipate muda wa kuyauliza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom