ntagunga
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 654
- 256
Je ni namna gani jeshi la polisi na lenyewe linatii sheria bila shurti katika kudumisha amani? Nani anatakiwa kulisimamia litii sheria?
sheria za nchi yetu ndizo mbovu siku zote. Ukisoma katiba sheria mama, haki ya mtu haiombi wala haitolewi na mtu bali na katiba yenyewe. Sheria iliyoanzisha vyama vya siasa, inatambua haki ya mtu si ya kuomba, ipo na haitolewi na mtu yeyote.
Lakini Penal code, Inakataza baadhi ya mambo yaliyotambuliwa kama haki ya watu mfano kukusanyika, inatmbua kama unlawful assembley, hii ndiyo inayotumiwa na POLICE wenye kuamini watafanikiwa kimadaraka kwa kuzifinya haki hizo kwa maslahi ya CCM.
Swali kwa Tundu, sheria hizi zimekaaje na ni nini mwafaka wake?